Takriban watu 50 wameuawa baada ya trela ya kusafirisha mafuta kugongana na gari ndogo katika barabara kuu magharibi kwa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo.
Ajali hiyo ilitokea karibu na mji wa Kisantu, kati ya mji mkuu Kinshasa na bandari ya Matadi.
Watu 100 walipata majeraha mabaya ya moto kwa mujibu wa Atou Matabuana, gavana wa mkono wa wa Kongo Central. Mwaka 2012 watu 220 waliuawa wakati trela ya mafuta ilipopinduka na kuteketeza vijiji kadhaa
Je utafanyaje ukigundua kuwa dereva wa basi la mwendo kasi uliloabiri si binadamu ?
Amini usiamini, kampuni moja inayomiliki mabasi ya uchukuzi wa umma nchini India imelazimika kuomba radhi baada ya abiria mmoja kuvujisha video inayoonesha dereva wa basi alimokuwa amemuachia tumbili usukani wa basi huku basi hilo lililokuwa limejaa likifululiza kwa kasi katika barabara kuu katika jimbo la Karnataka Kusini.
Ajabu ni kuwa huyo alikuwa amemakinika kikamilifu ,,,akidhibiti basi kwenye kona na hata kupisha magari mengine kwa utulivu na umakini wa kipekee
Dereva huyo amesimamishwa kazi mara moja ili kuruhusu uchunguzi kufanyika licha ya video hiyo kuonesha mkono mmoja wa dereva huenda ulikuwa kwenye usukani.