Makapuku Forum

Makapuku Forum

VITU KUMI AMBAVYO NI LAZIMA UJUE KUVIFANYA. NA KAMA HUWEZI KUFANYA VITU HIVI JIFUNZE HARAKA!

1.Unatakiwa kujua mbinu kadhaa fupi za kuokoa maisha yako au mwingine mfano, kuogelea kumpa mtu pumzi aliyepata ajali nk. (kujua kutoa Huduma ya kwanza)

2. Unatakiwa kujua njia mbadala ya kuwasha moto hata bila ya kutumia kiberiti, gesi wala umeme hasa vinapokuwa havipo. Mfano, porini


3. Unatakiwa kujua namna ya kutumia mashine ya kutolea fedha ATM


4. Unatakiwa Kujua Kuendesha angalau chombo kimoja cha usafiri na kuwa na uwezo wa kuziba pancha au kubadili gurudumu (baiskeli, pikipiki, gari nk)
 
5. Unatakiwa Kujua Kuongea vizuri Lugha zaidi ya Mbili tofauti


6.Unatakiwa ujue kuchora


7. Unatakiwa ujue kutumia, simu, kompyuta, ramani na internet


8. Unatakiwa ujue kutumia sindano ya kushonea, jembe, fyekeo, nyundo, shoka, na msumeno


9. Unatakiwa ujue kusema “samahani”, “nilikosea” , na ujue Kuomba msaada


10. Unatakiwa Kujua kupika
 
MAAJABU 10 YA MANENO HAYA KUMI YA KIINGEREZA
1.”Almost”
Ndilo neno refu zaidi la kiingereza ambalo kila herufi imetokea mara moja, yaani hakuna herufi iliyo jirudia

2.”Rhythm”
Ndilo neno refu zaidi la kiingereza lisilo na irabi (a, e, i, o, u) hata moja

3.”The quick brown fox jumps over a lazy dog”
Ndiyo sentensi Pekee ya kiingereza inayobeba herufi zote 26 za kiingereza.


4. “Are you as bored as I am”
Ndio Sentensi pekee ya kiingereza inayoweza kusomwa kinyume na ikaleta maana
 
5. “Swims”
Ni neno refu zaidi la kiingereza ambalo hata ukiligeuza juu chini, bado litasomeka hivyo hivyo

6. Neno “listen” na neno “silent” yana herufi sawa

7. ” pneumonoultramicroscopicsilicovolcanoconiosis'”
Ndilo neno refu zaidi kwenye lugha ya kiingereza! Ni jina ugonjwa wa mapafu unaosababishwa na vumbi

8. “set”
Ndilo neno lenye maana nyingi zaidi katika maneno yote ya kiingereza

9. Ni maneno mawili tu ya kiingereza yanayoishia na –ngry.. Hungry na angry

10. Herufi “S” ndio inayotumiwa kwenye maneno mengi zaidi kuliko herufi nyingine yoyote
 
Inapendeza sana ndugu yangu,,,yule mtt wa daslamu Shunie utamsalimia akija bila kumsahau Tumosa na ABJ

...salamu zimefika usikonde, tena bila kuchelewa, labda na huyu ABJ akija atakuja na namba niliyomuomba. Umefanya vizuri kumuita.

Kuna mdau anaitwa Numbisa anashusha nondo za maana, pita usome, mimi siwezi kuzisoma saa hizi maana nakula vyombo hapa na kuburudika na sebene
 
...salamu zimefika usikonde, tena bila kuchelewa, labda na huyu ABJ akija atakuja na namba niliyomuomba. Umefanya vizuri kumuita.

Kuna mdau anaitwa Numbisa anashusha nondo za maana, pita usome, mimi siwezi kuzisoma saa hizi maana nakula vyombo hapa na kuburudika na sebene
Hahahahah ulimuomba namba kumbe?atakuwa bado anashungulikia hyo namba..
Kuhusu Numbisa...huyo binti mkorofi kuwa nae makini hahahah
 
images%20(15).jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom