Mshambuliaji wa klabu ya Tottenham, Lucas Moura ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Mwezi wa Nane (Agosti) ndani ya Premier ya England, Katika Mwezi huo Mbrazil huyo wa kwanza tokea 2011 kutwaa tuzo hiyo amefanikiwa kufunga magoli Matatu (3) na kutoa Assist Moja (1) klabu yake ikishinda Mechi tatu ndani ya Mwezi huo......
Moura amewashinda Wachezaji Marcos Alonso wa Chelsea, Neil Etheridge wa Cardiff City, Benjamin Mendy wa Manchester City, Roberto Pereyra wa Watford, Sadio Mane na Virgil Van Dijk wote wakikipiga na Liverpool.
.
•Wakati huo huo Kocha mkui wa Watford, Javi Gracia ameshinda tuzo ya kocha bora mwezi wa nane (Augosti) ndani ya Premier ya England...Katika mwezi huo, Gracia aliiongoza Watford kushinda mechi zote tatu (3) ndani ya mwezi huo Pia Amewabwaga makocha Jurgen Klopp wa Liverpool, Mauricio Pochettino wa Tottenham na Maurizio Sarri wa Chelsea.
.
•Pia Tuzo ya Goli Bora la Mwezi wa nane (Agosti) imebebwa na Kiungo wa Klabu ya Fulham, Jean-Michael Seri, ni goli ambalo alifunga katika mchezo wa Premier League dhidi ya Burnley..