Makapuku Forum

Makapuku Forum

Tafasiri Unavyoweza: Mzaha Wa Viwanda, Shirikisha Wote.

...tunapenda kuona Tanzania ya viwanda, ndiyo, huu ni uchu wa kila mpenda maendeleo nchini na bila shaka ukibebwa mioyoni mwa kila mmoja, kwa utashi wa wengi kwa kutambua kuwa tunajenga nyumba moja basi mchango wa sekta ya viwanda utakuwa mkubwa na viwanda vitakuwa vingi. Kwa sasa ni maneno mengi tu ndo utasikia, takwimu za mdomoni mara kila mkoa utajenga viwanda 3000+, ukitaka kuvitafuta viwanda hivi utachoka, vingine ni miradi iliyoko kwenye karatasi wala hakuna hata anuani. Tafasiri unavyoweza.

Sera nzuri na inayoweza kufanya kazi sehemu husika ni ile inayoshabikiwa na wengi, je unakumbuka zama za miradi ya umma kufa baadhi ya sehemu? Wananchi wanahitaji barabara, wanajengewa kiwanja cha ndege. Hizi zilikuwa ni zama ambazo maenedeleo ya Rukwa yalipangwa na watu wanaoishi Dar, hawaijui Rukwa, hawajui mahitaji yake na hivyo wakipeleka mradi, ile dhana ya umiliki ya wana Makanyagio pale Mpanda inakuwa haipo, wanaukanyaga mradi na unakufa maana wananchi hawakuuhitaji.

Tunapoongelea viwanda tunaongelea uchumi mkubwa, tunaongelea miundombinu inayowezesha viwanda viwepo, vimee na vichangie pato la taifa, sio masuala ya vyerehani vinne na maduka ya kunyoa nywele. Tunaongelea utayari wa serikali kujipanga na kuhakikisha umeme wa uhakika, miundombinu rafiki ya usafiri, kodi zinazobebeka na ulinzi wa tunachozalisha (smart protectionism), sio unazuia bidhaa toka nje ilhali hatuwezi kuzalisha kukidhi soko. Tuache mzaha, kauli mbiu ya viwanda, ili ifanikiwe iwe ya kitaifa na sio kichama, tafasiri unavyoweza
 
Muziki: Sina Cha Kuandika

...nimeanza kwa kusema sina cha kuandika lakini kusema sina hakumaanishi kuwa niko tupu kabisa. Hapana, nina machache tu ya kaundika na hasa kukushukuru wewe unayenifanya nije hapa kila muda huu sababu unalifanya jukwaa hili kuwa sehemu nzuri kuwepo. Asante

Muziki sasa, sina mengi just burudika na uwe na wakati mzuri

 
Nasisitiza tuu kuwa England wanatoka leo..


..tayari safari ishawakuta
996428990.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom