Makapuku Forum

Makapuku Forum

Nimeambiwaaa unaniitaa kaka siku hiziii

Obe au umenidanganya


...mjomba, nikisema mimi kuwa ni uongo wakati ni kweli alikuita kaka nitaonekana nawafitinisha sasa mimi nakuacha uamini ulichosikia. Tena kuna mengi acha tu, kuna siku alikuita eti wewe ni mdogo wake yaani nilijifanya sijui kusoma nikamuomba yule tolu anisomee. Sikuamini na hata wewe ukitaka unaweza kujifanya huamini ili maisha yaendelee maana aunt yangu mimi sipendi kabisa kumkosea
 
Tafasiri Unavyoweza: Shawishi Bila Maguvu

...kama kuna sifa moja kubwa ambayo viongozi wengi wanaikosa hapa kwenda ni sifa ya ushawishi. Uwezo wa kumshawishi mtu mwingine afanye unalodhani ni sahihi kwako, kwake na kwa jamii nzima. Hili linakosekana kwa wengi na tunachoona sasa ni maguvu badala ya ushawishi unaokubalika na wengi. Imezoeleka sasa na tumeona namna ushawishi wa watawala kwa wananchi unazidi kupungua kila kukicha na badala yake ni mabavu na vitiso vya kitoto. Fikiria kuhusu zile harakati za maandamano mtandaoni, badala ya kujadili hoja misuli ilitumika ya mikono na shingo iliwatoka viongozi wa dola kiasi wakajikuta wanakosa hata akili za kutoa ujumbe ikabaki ni vitisho tu.

Unamuangalia kiongozi uso wake umejikunja, hauna nuru, misuli ya shingo inamtoka kila anapotaka kuwasiliana na umma. Anataka aabudiwe, hataki majadiliano. Uoga huu kwa mtizamo mwingine ni dalili za mtu anayetaka kukuibia, hataki ufikiri, shuruti inatawala. Serikali ya kambale, kila mmoja anasharubu, dola inajipanga kukuvunja miguu, bunge limekuwa kwaya/kasuku kuimba kinachoimbwa na dola na mahakama inaambiwa kuna muhimili uliojichimbia zaidi. Umma umefungwa na wachache wanajiona wana haki na akili kuliko wengine na kila mtu anajaribu kusema tuko kwenye njia sahihi (right track), kama kasuku unarudia ulichosikia.

Kiongozi badala ya kusikiliza anajiandaa kujibu, anajiona yuko sahihi kwa sababu tu kazungukwa na vyombo vya dola na si ajabu ukimwambia asikilize atakufuata na vifaru. Ni suala la muda tu utaona kuwa kwa kuwa ushawishi ni mdogo basi msafara wa kiongozi utakuwa ukitanguliwa na vifaru na magari ya delaya ili kumfikisha kiongozi kuongea na wananchi! Tafasiri unavyoweza. Nimeandika sio kukushawishi, nimeandika usome
 
Muziki: Nipe Nikupe

...najihisi kukosa kitu na sijajua ni nini, naamini nikishakusalimia Kapuku wewe unayepafanya hapa kuwa sehemu nzuri kuwepo nitakumbuka. Sababu ni moja tu, nitake nini hapa nikose, nitapata mengi, nitajifunza mengi sababu hapa kuna watu 'exceptional' wa tofauti wanaotofautiana kwa mengi na tofauti hizi ndo zinalifanya jukwaa hili kuwa la kipekee. Asante wewe unayekuja hapa na kutuongezea ufahamu. Maisha ni kujifunza.

Muziki sasa, nisikuchoshe maana nisijifanye nina cha kuandika ilhali sina nakuacha uburudike na muziki.

 
Back
Top Bottom