Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mornie all
20180501_110830.jpg
20180501_110815.jpg
20180501_110800.jpg
20180501_110744.jpg
20180501_110728.jpg
20180501_110712.jpg
20180501_110656.jpg
20180501_110641.jpg
20180501_110626.jpg
20180501_110611.jpg
20180501_110557.jpg
20180501_110541.jpg
20180501_110525.jpg
20180501_110507.jpg
20180501_110452.jpg
20180501_110434.jpg
 
[emoji524]Baba yetu na Mungu wetu tunakushukuru sana kwa wema wako ,fadhili zako na Ulinzi wako hata kutufikisha siku hii njema sana ya leo JUMANNE MAY1, 2018 Baba Sifa Shukurani Heshima Utukufu ni kwako Mfalme wa Amani.

Tunakuomba, utusamehe makosa yetu yote tuliyotenda kwa mawazo maneno matendo na kutotimiza wajibu mbalimbali
Tunaomba Utulinde siku ya leo Utukinge na ajali na hatari zote za mwili na za roho Ukawatume Malaika Walinzi Kila tunapokuwa Baba na Utupe nguvu ya kukutumikia wewe.

Wabariki watu wote katika Familia zetu, Wasaidizi wetu, wanandoa ,Watoto, Ndugu Jamaa ,majirani na Marafiki Damu ya Yesu itufunike.
Walinde wenye mahitaji na shida mbalimbali Ponya Wagonjwa Fariji Wafiwa Wajane Wagane Yatima Wafungwa na wote Walioumizwa na kukata tamaa wape Tumaini Baba.

Walinde Wasafiri wote Majini ,Nchi kavu, Angani uwe Dereva Utufunike kwa Damu yako ya Thamani Tutokako na Tuendako
Bariki kazi zote za mikono yetu Ukaonekane kwetu katika Ajira ,Ujasiriamali Biashara tupate riziki halali na tukutumikie vyema.

Mungu wetu na Baba yetu tunakuomba utusaidie tuwe na Upendo wa kweli tukawe msaada kwa wenzetu kimwili na kiroho na tusipungukiwe Baba tuitende kazi yako bila kuchoka wala kukatishwa tamaa..Tunayo mipango mingi mbele yetu Baba tunaomba UKATUFANIKISHE ,kila jambo tulilopanga lifanyike kwa utukufu wa jina lako takatifu
Asante Baba kwakuwa Unatupenda na Utatutendea sawasawa na Mapenzi yako.

Tunaomba haya yote kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu amen.

Damu Takatifu ya Yesu ikanene mema siku zote.[emoji1374]

SIKU NJEMA[emoji1374]
 
Back
Top Bottom