Makapuku Forum

Baada ya kuchukua taarifa zako + alama za vidole, ulifuata utaratibu wa kuwatambua raia wema na wabaya. Walio kuwa clean Bila ya makando kando awamu ya kwanza tu majina yao yalitoka wale wengine ilibidi waangaliwe ili wajiridhishe vizuri.

Nyagei
Kwahiyo sisi wa awamu ya kwanza ni wasafi
 
Tafasiri Unavyoweza: Elimu Inasafiri Zingatia Machache

Kama kuna kitu huwa napenda kuandika na kujifunza sana ni kile kinachohusu elimu, nina sababu nyingi za kufanya ninavyofanya. Mojawapo kubwa ni kuwa elimu ni mkombozi, inakufungua macho na kuzipa nguvu zako za kimwili nguvu nyingine ya kufanya jambo la manufaa kwako, jamii inayokuzunguka na taifa kwa ujumla. Elimu ni kila kitu na hapa ninaongelea zaidi elimu inayopatikana kwa mtaala maalum na huhusisha mitihani na kupata cheti. Tafasiri unavyoweza

Ni jambo muhimu kuisaka elimu, hili linajulikna na hata kwenye misahafu usemi huu unazungumzwa sana. Elimu ukiipata, maarifa yanaongezeka na uwezekana wa kufanikiwa maishani ni mkubwa, usiidharau elimu ambayo ukihitimu unapewa cheti. Hivi ulishajiuliza kwanini wababe (gangsters)hujichora chata (tattoos) mwilini? Jibu ni rahisi tu, kuonesha kwa wengine namna walivyo wababe na hivyo wewe isake elimu pata vyeti ndo chata zako.

Elimu inasafiri (elimu masafa) kwa sababu sasa huhitaji muda wote kuwa darasani, kuonana na mwalimu. Sasa unapata elimu masafa na maisha yanaendelea. Ukisoma elimu masafa (mfano OUT na vyuo vya nje ya nchi) zingatia mambo yatakayokufanya ufaulu hata kama huonani na mwalimu wako uso kwa uso. Jali ratiba ya kujisome, tenga muda wa kwenda maktaba na wasiliana na mkufunzi wa kozi unayosoma ili akupe mwongozo wa nini ufanye ukamilishe kinachotakiwa. Usione uko mwenyewe, huonani na mwalimu ukadhani ndo muda wa kufanya uzembe (slacker), elimu inayosafiri ina mitihani. Tafasiri unavyoweza.

Nikutakie mapumziko mazuri ya weekend na tukutane tena wiki ijayo panapo majaliwa.
 
Muziki: Tutajuana Tu

Weekend imeanza na muziki wa kutofikirisha ukiamua kucheza sawa, ukiamua kukaa ukitingisha mguu nalo sawa. Burudika na muziki na salamu zangu kwa anko wangu Lyon Lee ambaye yeye mahudhurio yake kwenye muziki wa aina hii ni kwa sababu ya kumpata yule dada wa Kikojani walikutana kwenye semina ya wenye viwanda.

Uwe na wikend njema

 
Binamu asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…