Tafasiri Unavyoweza: Nje Sawa, Ndani ya Box Unapajua?
Kama kumetokea msemo unaosikika sana katika miaka ya hivi karibuni ni huu unaosema fikiria nje ya box (Thinking outside the box). Huu ni msemo ambao ni maarufu sana katika nyanja za ujasiriamali. Ukihudhuria mafunzo ya wajasiriamli utausikia sana huu msemo. Ni msemo unaovutia kusikiliza na utashangaa unaambiwa kufikiria nje ya box wakati hakuna anayekuuliza ndani ya box ulilomo kuna nini. Tafasiri unavyoweza.
Labda nipunguze kuandika mengi, kufikiria nje ya box ni hali ya kuwa mbunifu, kutambua nguvu ulizonazo na madhaifu yako katika kutekeleza jambo mahsusi. Maana yake hapa ni kuwa huwezi kufikiri nje ya box kama hauko ndani ya box na kujua kilichomo ndani ya box ni kitu gani na ufanye nini kutatua changamoto za ndani ya box.
Ukishajua kilichomo ndani ya box, na si lazima mtu mwingine akwambie nini kilichomo ndani ya box unalilomo, unayajua yaliyomo yamo ndani ya box, ni jukumu lako kuyajua haya na si mtu mwingine ajitokeze na kukwambia ufikirie nje ya box. Ukishajua kilichomo ndani ya box sasa una haki ya kfikiri nje ya box na unawezaje kufikiri nje ya box, hili ndo suala sasa.
Unaweza kufanya mambo kadhaa ya msingi kama unataka kufikiri nje ya box, mfano, siku zote unanyoa toka juu kwenda chini, haya ni mazoea, hebu leo badili unaponyoa anzia chini kwenda juu, huku ndo kufikiria nje ya box. Tafuta maarifa na taarifa sahihi, fanya uthubutu na usidharau, tafuta ushauri kwa mtoto mdogo, wanajua ya kujua na anaweza kukwambia kitu ambacho hukutegemea. Jipe nafasi ya kuwa msafi, oga na vaa vizuri kila wakati.
Hivi unajua kuota ni moja ya njia nzuri ya kupanga mpango timamu! (Dreaming is a form of planning!!). Tafasiri unavyoweza.