Makapuku Forum

Makapuku Forum

Tafasiri Unavyoweza: Hasira kwa Kundi, Tegemea Vita

Sitazunguka mbuyu, itakuwa ni jukumu lako kutafasiri unavyoweza. Taifa letu linakabiriwa na matatizo lukuki, nikianza kuyataja hapa itachukua ukurasa mzima kuyaorodhesha, ni mengi sana kuanzia miundombinu isiyo rafiki kwenye uchumi, demokrasia na utawala bora, huduma za jamii, usafiri, ajira, usalama wa raia na mali zao, kilimo na mifugo pamoja na nyanja nyingine. Haya kuyaita matatizo ni sawa lakini kama taifa tukiyaita changamoto itapendeza zaidi. Tafasiri unavyoweza.

Tuna tatizo na kauli za watawala wetu, ndiyo, kila mara ukizisikia kauli za watawala wetu ni kama kauli za kiranja mbabe wa darasa la tatu ambaye kwa kukosa kwake umakini darasani (inability to focus his/her attention) anashindwa kutia bidii darasani ili ajue sababu za yeye kushindwa kutatua changamoto zinazomkabili kuondoa changamoto. Kwa hali hii anajikuta anaaza kuonea wengine darasani, na kuwapa majina kuwa matatizo ya darasa yanaletwa na watu wanaokaa mstari wa katikati na mwisho wa darasa. Tafasiri unavyoweza.

Changamoto za kitaifa tulizonazo, nawaandikia 'watawala', tuliowapa dhamana ya kuongoza taifa letu tunalolipenda, Tanzania. Ninawaandikia kwa sababu hata siku moja kauli za kuminya demokrasia, kuweka masharti magumu kwa wajasiriamali, kutaka kusifiwa tu kwa kila jambo, na ukikosolewa unatumia polisi haziwahi kuleta maendeleo. Wananchi wanachotaka ni kuona huduma bora za msingi na si kiongozi kujipigapiga kifua kusema kuna hiki na kile wakati wananchi hawakioni.

Hakuna jambo baya kama kuhusianisha kushindwa kwako na watu wengine iwe chama cha siasa, asasi za kiraia na hata raia waaminifu. Kukosolewa ni haki za kimsingi kabisa na kama huna ngozi ngumu basi huna haja ya kugombea nafasi za kuongoza hata kama watu watakesha madhabahuni wakikuombea. Kuwafanya wakosoaji kuwa ni maadui zako kunafungua milango ya uonevu, utekaji, utesaji, udhalili, mauaji na mwisho wanaoona wanaonewa watajiunga kupambana na mbabe wa darasa la tatu na wafuasi wake, na hii ni vita. Tafasiri unavyoweza
 
Wakuu kwema ?? Hapa mmoja anajifahamu sio mkuu make sitak kesi naye kabisa
tumblr_inline_mh5phqu1hY1qiedzj.gif
 
Muziki: Endeleza Mazuri

Nilikuwa na wakati mzuri kipindi chote cha weekend, nilipumzika na kupata ugeni wa rafiki. Ilikuwa ni nzuri sana, sijui wewe ulikuwa na weekend ya namna gani. Tumeanza juma jipya na kama unavyojulikana mwezi wa tatu huwa si mwezi wa mchezomchezo, kuna kwaresma ndani yake na Pasaka.

Nilichat na anko wangu, Lyon Lee tulitumia telegram anasema anafanya majaribio ya maandamano. Huyu anko wangu kama nyie huwa mnamuelewa sawa, hivi kweli mtu alikuwa ziarani Singida kuzindua kiwanda lakini bado anatumia telegram!!!! Si bora hata angetumia TMO au money order

Muziki sasa, burudika na rhumba hili uwe na wakati mzuri

 
Tafasiri Unavyoweza: Nje Sawa, Ndani ya Box Unapajua?

Kama kumetokea msemo unaosikika sana katika miaka ya hivi karibuni ni huu unaosema fikiria nje ya box (Thinking outside the box). Huu ni msemo ambao ni maarufu sana katika nyanja za ujasiriamali. Ukihudhuria mafunzo ya wajasiriamli utausikia sana huu msemo. Ni msemo unaovutia kusikiliza na utashangaa unaambiwa kufikiria nje ya box wakati hakuna anayekuuliza ndani ya box ulilomo kuna nini. Tafasiri unavyoweza.

Labda nipunguze kuandika mengi, kufikiria nje ya box ni hali ya kuwa mbunifu, kutambua nguvu ulizonazo na madhaifu yako katika kutekeleza jambo mahsusi. Maana yake hapa ni kuwa huwezi kufikiri nje ya box kama hauko ndani ya box na kujua kilichomo ndani ya box ni kitu gani na ufanye nini kutatua changamoto za ndani ya box.

Ukishajua kilichomo ndani ya box, na si lazima mtu mwingine akwambie nini kilichomo ndani ya box unalilomo, unayajua yaliyomo yamo ndani ya box, ni jukumu lako kuyajua haya na si mtu mwingine ajitokeze na kukwambia ufikirie nje ya box. Ukishajua kilichomo ndani ya box sasa una haki ya kfikiri nje ya box na unawezaje kufikiri nje ya box, hili ndo suala sasa.
Unaweza kufanya mambo kadhaa ya msingi kama unataka kufikiri nje ya box, mfano, siku zote unanyoa toka juu kwenda chini, haya ni mazoea, hebu leo badili unaponyoa anzia chini kwenda juu, huku ndo kufikiria nje ya box. Tafuta maarifa na taarifa sahihi, fanya uthubutu na usidharau, tafuta ushauri kwa mtoto mdogo, wanajua ya kujua na anaweza kukwambia kitu ambacho hukutegemea. Jipe nafasi ya kuwa msafi, oga na vaa vizuri kila wakati.

Hivi unajua kuota ni moja ya njia nzuri ya kupanga mpango timamu! (Dreaming is a form of planning!!). Tafasiri unavyoweza.
 
Muziki: Tambua Mlango, Usiruke Ukuta

Bado tunaendelea na aneno machache ila muziki hatuwezi kuacha kuucheza kwenye kipengele hiki. Nakusalimia Kapuku na kukwambia kuwa wewe ni mtu mzuri sana na unalifanya jukwaa hili kuwa sehemu bora kabisa kuwepo.

Uwe na wakati mzuri usiku huu.

 
Muziki: Endeleza Mazuri

Nilikuwa na wakati mzuri kipindi chote cha weekend, nilipumzika na kupata ugeni wa rafiki. Ilikuwa ni nzuri sana, sijui wewe ulikuwa na weekend ya namna gani. Tumeanza juma jipya na kama unavyojulikana mwezi wa tatu huwa si mwezi wa mchezomchezo, kuna kwaresma ndani yake na Pasaka.

Nilichat na anko wangu, Lyon Lee tulitumia telegram anasema anafanya majaribio ya maandamano. Huyu anko wangu kama nyie huwa mnamuelewa sawa, hivi kweli mtu alikuwa ziarani Singida kuzindua kiwanda lakini bado anatumia telegram!!!! Si bora hata angetumia TMO au money order

Muziki sasa, burudika na rhumba hili uwe na wakati mzuri

Asante kwa burudani
 
Back
Top Bottom