Makapuku Forum

Makapuku Forum

Wakuu kwema ??

Obe nakusalimiaa binamu make najua fika wewe sio mkuu bali ni binamu wangu wa faida kufa na kuzikana japo ntakuzika kwanza wewe
 
44ab22d2324398d1ec51d066a4f3082b.jpg


Cc: Sakayo
Shunie
Nyagei
Linamo
Lyon Lee
ABJ
Tumosa
 
Tafasiri Unavyoweza: Kunuka Sio Kuoza

Unakumbuka mambo ya kuchanganua sentensi kwa njia ya matawi na njia nyingine, muda umepita sana lakini kujikumbusha ya zamani si mbaya na hasa kama yanakuongezea maarifa. Unaweza kulichambua neno/kitenzi kunuka utakavyo na ndiyo maana hiki kipengele kipo hapa, unatafasiri unavyoweza, na si lazima wote tuwe na tafasiri moja juu ya jambo au kitu fulani. Wengine tafasiri hutegemeana na mazingira, tafasiri ya juzi si ya jana na haiwezi kuwa na ulazima kuwa hivyo hivyo kesho na kesho kutwa, tafasiri unavyoweza.

Wengi wetu ni watumiaji wa bidhaa tunazonunua madukani au magengeni, baadhi ya bidhaa hizi huwa zimeandikwa muda wa matumizi ambao kwetu tumeupa umaarufu wa expire date. Leo nitakufanya utafasiri tofauti kidogo na hata ukibaki na tafasiri yako sio mbaya maana ndiyo lengo la makala haya. Hivi unajua kuna tofauti ya sell-by, use-by, best-by na expire date? Yes, nimeandika haya maneno kwa kiinglish maana ndiyo huwa tunaona kwenye bidhaa nyingi tunazonunua.

Tumekuwa na kawaida ya kutupa bidhaa tulizonunua baada ya kuona tarehe kwenye bidhaa husika ikionesha muda wake umepita. Hii inaweza kuwa ni sawa na au isiwe sawa, nitafafanunua;
Tumia kabla ya- hii ni ilani inayoonesha mnunuzi anaweza kuupata ubora wa bidhaa aliyonunua kwa kiwango kizuri kabisa (freshness) na tarahe ikipita haimaanishi kuwa bidhaa hiyo imeharibika. Uza kabla ya- hapa mlengwa ni muuzaji, auze bidhaa hii na muda ukiisha aitoe kwenye makabati na wauzaji wengine hu-markdown- kuuza kwa punguzo bidhaa husika, bidhaa kama mayai, maziwa, maua, ni maarufu kwa hili. Ubora kabla ya- hapa bidhaa unayonunua inatajwa kuwa ni bora kwa kipindi kilichooneswhwa kwenye karatasi.

Usitupe tu bidhaa kisa umeona maneno hayo hapo juu, ila ukiona imeandikwa expire date- basi hiyo tupa. Harufu ya nguru haimaanishi kuoza bali ndo ubora wake. tafasiri Unavyoweza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom