ShikamooTafasiri Unavyoweza: Maktaba Si Vitabu na Utulivu Pekee
.....library offers more services, they are more than just books. Nimeanza na kiinglishi kuonesha mazingira tuliyozoea kuitafasiri maktaba. Tafasiri unavyoweza. Tumekuwa na mazoea ya kuhusisha maktaba na elimu, well, kuna ukweli katika hili. Maisha yetu tunayoishi yamejaa kila aina ya 'machafuko' na changamoto (chaos and challenges) ambazo inabidi tuzitatue. Na ujue kabisa si kila changamoto unayokutana nayo maishani utategemea mwingine akutatulie, nyingi unatatua mwenyewe.
Tafasiri unavyoweza, utulivu unaokutana nao maktaba una maana moja kubwa, watu wanatulia kufikiri. Kelele unazokutana nazo maktaba zina maana kubwa, watu wanatoa mawazo yao kupitia ushairi, sinema, ghani na ngano. Umestuka eeh, kuona nimeongeza kelele maktaba!! Eeh, maktaba sahihi ina sehemu maalum kwa wewe kwenda na kupiga 'makelele'. Na hapo ndo hoja yangu ya kutafasiri ninavyoweza inakuja. Maktaba ni zaidi ya vitabu.
Changamoto na machafuko tunayokutana nayo ni darasa tosha la kuturudisha maktaba kujua wengine walikabiliana nayo vipi. Kumbuka wewe si wa kwanza kwenye kila tatizo au changamoto. wewe si wa kwanza na hautokuwa wa mwisho hivyo jitahidi kutumia muda kidogo kutembelea maktaba ujifunze mengi. Na kama huwezi kutembelea basi unaweza kusaidia maktaba iliyo karibu nawe kwa kuchangia muda na rasilimali. Tafasiri unavoweza, nchi huru hii.
Shikamoo
Tunamshukuru Mungu tunaendelea kulijenga taifa kwa kukosoa na kupongeza na kulitumikia pia kama katiba ya nchi inavyotakaNi njema kabisa pole na majukumu
Wkend yetu ilikuwa poa msalmie husobeMarhaba hujambo wewe mama JJ.
wikend yenu ilikuwaje? Yangu ilikuwa poa sana, asante kwa kutouliza japo umeanza na salamu ya shikamoo
[emoji120] [emoji120] [emoji120]Tunamshukuru Mungu tunaendelea kulijenga taifa kwa kukosoa na kupongeza na kulitumikia pia kama katiba ya nchi inavyotaka
Wacha nijiwekee wimbo mwenyewe....
Cheeeer it up! Up in the air!
AsanteObe ubarikiwe usiku mwemaMuziki: Kuna Tofauti
Asante sana Transcend kwa kunikumbusha kuweka muziki, ujue nini, tangu nimeanza kuandika Tafasiri Unavyoweza nimekuwa na wakati mgumu wa kuwa ndani ya wakati kutupia kipengele cha muziki. Anyway, hakijaharibika kitu na kwa kutoharibika huku ninakusalimia sana kapuku wewe unayetumia muda wako kuwa hapa na kulifanya jukwaa hili kuwa sehemu nzuri kuwepo. Asante Tumosa kwa kunisalimia.
Yeah, nilikuwa naongea na anko wangu huyu huyu Lyon Lee ambaye kwa kweli amekuwa na safari nyingi kuzidi safari lager yenyewe. Ila kila tukiongea kama kawaida yake haachi kunipa elimu ambayo nami kwa kupenda kushare knowledge siwezi kuacha kutowaambia. Kuna tofauti, ndivyo alivyoanza kusema, tofauti ya kuoga na kuogelea, tofauti ya huyu na yule, bure na bila malipo, kupendwa na kuachwa, bangi na bangili moja uikalie mbali kwani inakaa nawe miaka saba.
Muziki sasa, nakupenda sana wewe kapuku na sioni uchovu kukwambia hili kila wakati. Na kwa kutambua hili nakuacha na muziki huku ukitafakari tofauti zetu zinaztufanya kuwa wamoja
Asante TWacha nijiwekee wimbo mwenyewe....
Cheeeer it up! Up in the air!
Ubarikiwe sanaTafasiri Unavyoweza: Maktaba Si Vitabu na Utulivu Pekee
.....library offers more services, they are more than just books. Nimeanza na kiinglishi kuonesha mazingira tuliyozoea kuitafasiri maktaba. Tafasiri unavyoweza. Tumekuwa na mazoea ya kuhusisha maktaba na elimu, well, kuna ukweli katika hili. Maisha yetu tunayoishi yamejaa kila aina ya 'machafuko' na changamoto (chaos and challenges) ambazo inabidi tuzitatue. Na ujue kabisa si kila changamoto unayokutana nayo maishani utategemea mwingine akutatulie, nyingi unatatua mwenyewe.
Tafasiri unavyoweza, utulivu unaokutana nao maktaba una maana moja kubwa, watu wanatulia kufikiri. Kelele unazokutana nazo maktaba zina maana kubwa, watu wanatoa mawazo yao kupitia ushairi, sinema, ghani na ngano. Umestuka eeh, kuona nimeongeza kelele maktaba!! Eeh, maktaba sahihi ina sehemu maalum kwa wewe kwenda na kupiga 'makelele'. Na hapo ndo hoja yangu ya kutafasiri ninavyoweza inakuja. Maktaba ni zaidi ya vitabu.
Changamoto na machafuko tunayokutana nayo ni darasa tosha la kuturudisha maktaba kujua wengine walikabiliana nayo vipi. Kumbuka wewe si wa kwanza kwenye kila tatizo au changamoto. wewe si wa kwanza na hautokuwa wa mwisho hivyo jitahidi kutumia muda kidogo kutembelea maktaba ujifunze mengi. Na kama huwezi kutembelea basi unaweza kusaidia maktaba iliyo karibu nawe kwa kuchangia muda na rasilimali. Tafasiri unavoweza, nchi huru hii.
Leo katika historia...
1945>Alizaliwa Bob Marley mwanamuziki maarufu kutoka Jamaika