
TUOMBE:
Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu Bwana Mungu wa majeshi Asante kwa wema na Upendo wako kwetu kwa kutupa neema hii yakuiona siku ya leo JUMAMOSI 13 JANUARI 2018
Asante Baba unastahili kuabudiwa Mfalme wa Amani
Wapo wengi walitamani kuiona siku ya leo hawakuweza Baba kuamka kama tulivyo sisi leo .
Baba tunakuja mbele zako leo tukiomba toba Baba Utusamehe makosa yetu tuliyotenda kwa mawazo kwa maneno kwa matendo na kwa kutotimiza wajibu wetu kwa nafasi zetu zote tulizonazo kwa kujua au kutojua
Tunaomba pia kuwasamehe wote waliotukosea walioomba msamaha hata wasioomba msamaha
Tunakuja mbele zako tukiomba Utulinde Utuokoe katika ajali mbalimbali za kimwili na kiroho Uwalinde watu wote wa familia zetu wasaidizi majumbani wake Waume Wanandoa Wachumba watoto Ndugu Jamaa na marafiki
Baba tunaomba Roho Mtakatifu akae nasi atufundishe kukujua kukupenda kukuheshimu na kukutii wewe tu
Baba Waponye wagonjwa majumbani na mahospitali
Baba wewe ndie mponyaji wa kweli waponye wagonjwa wote watie nguvu ndugu wazazi na walezi onekana kwao waamini Uponyaji toka kwako
Baba tunaomba ponya d awa wanazotumia wagonjwa wote wabariki madaktari na manesi watie nguvu wanaoguza wasipungukiwe
Wafariji Wafiwa Wajane Wagane Yatima Wapweke Walea pekee wenye mahitaji mbalimbali
Wape utulivu na majibu Baba wanaotafuta watoto ,wenye madeni wanaotafuta kazi, wanaotafuta Ada , wanaotafuta kodi za nyumba wenye mitihani na wote wenye uchungu na kukata tamaa Waliokataliwa Wafungwa waoneshe ukuu wako Baba kuwa unawapenda siku zote za maisha yao wawe na amani wakupende na wakuone wewe katika kila pito.
Tunaomba kila tunapotoka na tunapoenda Uwe dereva na kiongozi wetu tulinde Nchi kavu Majini na Angani Damu ya Yesu itufunike tuangalie kwa wema tufike salama katika safari zote siku ya leo Mfalme wa Amani
Tunaomba uwabariki Viongozi wote wa Dini waweze kutuongoza vema kiroho na tuwe na hofu ya Mungu
Walinde viongozi wa serikali na wenye mamlaka waweze kuongoza vema na kuwa na mwenendo bora Nchi iwe na amani na utulivu.
Ponya kazi za mikono yetu Biashara Ajira Ujasiriamali uonekane Mfalme wa Amani tupate riziki kihalali
Baba tunayo mengi unayajua tunaomba uyapokee na utupatie sawasawa na mapenzi yako utupe kuvumilia katika Mapito mbalimbali kwani kwako yapo majibu huchelewi wala huwahi Mfalme wa Amani
Asante Baba kwa kuwa unatupenda na hujawahi kutuacha kila tukuombapo utatujibu sawasawa na mapenzi yako
Tunaomba Tunashukuru na kuamini katika jina la Yesu Amen.
DAMU YA YESU ITUFUNIKE,SIKU NJEMA





SIKU NJEMA
SHALOM