Makapuku Forum

Muziki: Ijumaa ya Kufurahi

U khali gani mdau mwenzangu wa Jukwaa hili tunalolipenda KF, ninakusalimia nikiwa na furaha sana leo. Furaha yangu haijaja kama ajali sio kama mjomba wangu ambaye yeye jana alifurahia simu kuisha chaji. Anajitafutia sababu ya kujitekesha na apate kisingizio cha kujitetea kwa aunty yangu. Nitamshauri shangazi kumnunulia power bank.

Mnajua wote Ijumaa sio siku ya kuleta mambo magumu magumu maana kuna vichwa vya treni vinauzwa na mwenyewe hajulikani sasa itabidi tujipange tuvinunue tukishamaliza kulipwa hela za makinikia. Wale wote mnaosubiri Noah msahau, tushahamisha magoli, tunanunua vichwa vya treni. Yaani tulivinunua na re-nunua tena. Unashangaa, hii ndo furahiday

Muziki sasa, mambo ya bakulutu leo huku naangusha mojamoja na wewe kama sio mlipa kodi jiagizie Azam painapo. Nwa kwa hisani ya mpendwa wangu tunaburudika hapa

 
Na hayupo wa kunitoaa labda anko obe


Makaveli yuko wapi mshikaji wangu hanaga makuu

...mimi na wewe anko ni mambo ya ukoo, ukitoka wewe naandamana Jumapili naenda kwa mwadhama Pengo namwambia awasute wanaotaka katiba mpya, no wanaotaka kukufananisha na anko mkubwa.

Nikitoka hapo naenda kwa Sheick Ponda bin Issa tufanye press conference
 
Asante mpenzi wangu nakupenda sana ujue
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…