Makapuku Forum

Amen
 
YESU ANAFAHAMU SHIDA YAKO LAKINI HAIONDOI MPAKA UMWAMBIE AKUSAIDIE*

Math 20:32 Yesu akasimama, akawaita, akasema, Mnataka niwafanyie nini?

33 Wakamwambia, Bwana, twataka macho yetu yafumbuliwe.

34 Yesu akawahurumia, akawagusa macho yao; mara wakapata kuona, wakamfuata.

Yesu hajawahi kumponya mtu asiyehitaji kuponywa
Unaweza ukabaki na shida ndani yako huku ukisema Mungu ananiona ni kweli anakuona lakini umemwambia kuwa akusaidie?
Nakwambia utabaki na shida yako maana Mungu hatakusaidia maana yeye anasikiliza Maombi mathayo 7:7-8
Mungu anataka uombe
Ukisoma mathayo 6:8 inasema kabla hujaomba tayari Mungu anajua shida yako

Kujua shida yako hakumfanyi Mungu akusaidie bali yeye anasikiliza Maombi yako

Ndiyo maana ukisoma unaona wale watu walikuwa vipofu tena walikuwa wanalia kwa sauti lakini Yesu bado aliwauliza mwataka niwafanyie nini?

Hebu jiulize inamaana Yesu alikuwa hawaoni kuwa ni vipofu?

Jibu aliwaona lakini alikuwa anasikiliza Maombi yao na haja ya mioyo yao


YESU ANAKUONA LAKINI HAKUGUSI MPAKA UOMBE

UBARIKIWE
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…