Makapuku Forum

Makapuku Forum

Ebu tuwekeeni story basi mpaka tusahau baba d weka jaman hiyo mashine ya ujerumani na mpendwa wa binamu endelea na sahi mpaka tusahau jaman
THE DOM

Sehemu Ya 26 MWISHO

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsApp

Instagram....

Ilipoishia Jana →↓↓↓↓←

SON OF PRESIDENT GU

"Nikikosa Urais nitamuuzia mtu aliofanikiwa kupita"
"ok.. Sasa mi naona tuangalie kule jeshini, kule hatutokosa vijana"
"enheeee, umetoa wazo zuri sana... Sasa tunachukuaje kijana pale, mana sihitaji serikali ijue mipango yangu"
Aliongea waziri GU, huku mwenzie akitafakari jinsi ya kufanya,...
"mi naona tuanze na kijana mmoja kwanza"
"sawa, je ni yupi pale jeshini"
"yule mtoto wa General nyange hafai yule... Mana atakuwa na mazoezi mazuri kwasababu namuonaga sana baba yake anampa mazoezi ya private sana"
"mmmhhhh nyange ataua mtu,.. Ataua mtu nakwambia"
"sikiliza bwana mr GU,.. Hatumchukui kama tunachukuwa kuku"
"tutafanyeje sasa"
"sikiliza... Hata sisi ni wanajeshi wa kale, na unamjua vizuri General nyange ni rafiki yako... Tumchukue mtoto wake"
"sawa sikatai, ila tutamchukuaje yule"

ENDELEA.......

"njia rahisi sana.... Sisi tutafute mtu wa pale kambini, awalete wanafunzi wengi sehemu tunayotaka"
"kuna.. Jamaa mmoja pale ni mwalimu wa mafunzo ya mabomu,.. Anaitwa mr deo... Tuongee nae huyo mtu"
Aliongea mr GU wakati huo bado hajawa raisi,..
"sasa akishawaleta wanafunzi pale tunapo pataka, aanze kuwafundisha wanafunzi jinsi ya kurusha mabomu, afu amtangulize yule tunaemtaka"
"una akili wewe,... Sasa huyo deo atakubali kufanya hivyo"
"tumuahidi kumpandisha cheo kutoka kwenye ualimu kuja kwenye ugeneral"
"sawa, hebu fanya hivyo... Lakini sasa huyo kijana utampataje"
"wakisha anza kurusha mabomu, sisi tutakwenda na bomu la kweli, tunalifunga funga kwenye nguo za kijeshi, kisha tunalirusha... Baada ya bomu la kweli kulipuka mahali ambapo hakuna watu, basi huyo deo kazi yake ni kumzimisha huyo kijana, afu atatukuta sehemu tutakayomwagiza... Kwakua ni msituni hakutakuwa na atakaejua zaidi ya huyo mr deo,...na hawatoana mwalimu wao alipopita kwasababu patakuwa na wingu la moshi wa mabomu... Afu wakienda kuangalia watakuta vipande vipande vya nguo za jeshi huku kijana mmoja haonekani... Hio ndio akili yangu"
"ndio mana ukatwa majaliwa, kumbe una akili kiasi hicho"
"aahhh sisi wajeshi wa zamani bwana"

Baada ya siku tatu kweli zoezi lilifanikiwa na kweli sheby akafanikiwa kuletwa kwenye nyumba ya Mheshimiwa Waziri GU,.. Ila sheby hata yeye hakuwa akijitambua mana alibonyezwa mshipa wa fahamu ili asijue kilicho endelea kule msituni
Sasa muda huo ndio anazinduka akiwa katika chumba maalum.....
"kuanzia leo umekufa kijana sawa..."
"nini??.. Afu we si waziri wewe, mbona umeniteka"
"sikiliza kijana, nataka nikusomeshe uwe ripota wangu hapo baadae"
"kwahio ndio nimekufa"
"ndio, na pia utakwenda korea kufanyiwa plastic surgery ya sura yako, na ukirudi sitaki utambuzi wako uhusike, utabadili jina baada ya kumaliza mafunzo ya kijeshi nchini korea, na pia utakwenda kusomea upelelezi, utakwenda kujifunza mbinu za mapigano, yaani kuna option tatu zinazokupeleka kule... Gharama zote za kwenda mpaka kuishi kule ni zakwetu sisi, hivyo tunachokihitaji kwako uthubutu wa kukubali kuishi kama mtu aliekufa"
Aliongea waziri GU huku sahi akiwa kaketi katika kiti,...
"Na pia utakaporudi utakuta nyumba yako ipo tayari"
"sawa, nimekubali"
Sahi au sheby alikubali kujulikana kuwa kafa ili akasomeshwe nje ya nchi...
"sasa nataka nikutengenezee vitanzi kadi za bank, ili usiteseke kwa utambulisho"
"sawa"
Mipango ya sheby kusafirishwa kwenda nje ya nchi iliisha na sheby alikwenda,...

BAADA YA MIAKA MIWILI NA MIEZI 9 NDIO DOM IKAIBIWA BOT, NA HAPO SHEBY KABAKIZA MIEZI MITATU KUMALIZA MAFUNZO YAKE, NDIO RAIS GU AKAKUMBUKA KIJANA YUPO KULE KOREA, HIVYO AKAITWA KABLA YA KUMALIZA MIEZI YAKE MITATU ILI AFIKISHE MIAKA MITATU KAMILI.....

Siku ile sheby anarudi nadhani tunajua, mpaka akapambana na makomando,...

Walipofika Ikulu sheby alitakiwa kutoa vitambulisho vyake (VITANZI) alivitoa vyote, kisha rais GU akavichukuwa vile vitanzi (KAMA UMESAHAU KASOME SEHEMU YA PILI) Kitu alichokwenda kukifanya kwenye vile vitanzi, ni kuchapisha jina jipya katika vitanzi vile, kisha sheby akaitwa akapiga picha upya.. Kesho yake sheby anakuja akavishangaa sana vitanzi vile,... Kumbe vilikuwa vimebadilishwa majina.. Kutoka Sharbiny Rashidy Kingazi (Sheby), mpaka kuja kwenye jina, Salehe Rashidy Mohammed (sahi),.. Lakini pale pale alionywa kutosema chochote na kutomwambia mtu yeyote yule, ispokuwa mama yake tu, mana mama ni mama jamani roho inauma kumdanganya mama....

SASA HUO NDIO UKWELI JUU YA SAHI AU SHEBY....

sasa pale kila mtu anashangaa, ila rais GU akamuuliza mr deo
"wewe nawe tumekupandisha cheo kwa kazi nzuri ulioifanya, lakini sasa nawe kumbe ulikuwa na mambo yako unayafanya"
Aliongea raisi GU huku akiwaamuru makomando wawachukuwe watu hao
Sasa mr deo yeye ndio anashangaa nae, kumbe huyu ndie yule kijana aliomteka na kumpeleka kwa raisi.. Kumbe hata yeye deo hajui, mana deo anajua mpango wa kumteka na kumpeleka kwa Waziri baada ya kuahidiwa cheo, sasa ishu za kijana kubadirishwa sura hajui na ndio mana hata alivyokuja kambini hakumtilia shaka mana haijui hio sura

"lakini rafiki yangu ulichonifanyia sio kizuri ndugu yangu"
Aliongea general Nyange,
"tena nyie mna haki ya kunyongwa kwa ujinga mliokuwa mnaufanya kambini"
"sawa, umeshika mpini sisi tumeshika makali.... Mana hata mtoto wako humtaki tena"
"ebu watoeni hapa... Sitaki kujua ni General au nani, peleka sero, kesho niwatolee habari kwa wananchi wangu"

Basi mama sheby aliwahishwa hospitalini japo alikaa kwa muda kwasababu risasi haijaingia sehemu mbaya sana katika mwili wake,...

Sasa hivi leah anaishi kwa sheby ambaye ni sahi, mana tayari keshakuwa mchumba wake sasa,.. Lakini sasa alipofika nyumbani leah hamjui tena sahi, ila sauti ni sawa kasoro sura tu, mana sheby kavua lile lingozi alioshonwaga nalo usoni, sasa ana sura Original... Sheby aliingia na gari yake, ukumbuke geti linafunguka kwa remote control, sasa leah kwa furaha anatoka ndani na kwenda kumpokea baba watoto wake... Lakini alishangaa kuona mtu alioingia ni tofauti na mchumba wake anaemjua
"we ni nani mwenzangu"
Aliuliza leah huku akirudi nyuma, mana ni sura ngeni kwake
"vp baba nanii yupo"
Sasa leah aliposikia hio sauti ni ya sahi kweli lakini sura sio sahi tena,..
"wewe ni nani"
"mimi mdogo wake na sahi.... Sikia mi nataka nikuoe nitakumilikisha mali zangu, achana na sahi"
Sheby alikuja na ka njia ka kumdanganya leah ili aone bado ana tamaa au kaacha,... Kweli mwanamke ataamkiwe umilikishwaji wa mali akatae? Sijui ni nani
"ondoka zako apa,... Kwenda nitampigia simu huyo ndugu yako"
Aliongea leah huku akishika simu kweli tayari kwa kupiga, kana kwamba hajakubaliana na maneno yake... Lakini leah alishangaa simu inaitia kwa huyo huyo mtu...
"kivipi iitie kwako"
"leah, acha presha.. Mimi sahi original, ile sura ilikuwa ni sura ya kazi, sasa huyu ndio mimi, kama huamini ngoja niivae hapa uone"
Sahi kweli alilivaa lile lingozi na kumfanya leah kuamini
"waaooo lakini mbona wewe ni hensam kuliko hata hilo lingozi"
Aliongea leah huku wakiingia ndani

Kesho yake sahi na leah wakiwa hospitalini, walimkuta mama kapata kaunafuu kidogo, haijapita muda msafara wa rais unafika hospitali hapo...
"sahi si raisi yule"
"ndio hana shida"
"mmmmhh isije kuwa kuna jipu humu hospitalini"
"hapana hatumbuagi hovyo pasina sababu"
Sasa mke wa rais alipofika hapo, cha kwanza alimkimbilia sahi,..
"mwanangu hujambo"
"sijambo shkamoo mama"
"marahaba baba hali yako"
Aliongea mke wa raisi huku akimkagua shingo, mana jana ilitoka toka damu,... Sasa mama sheby aliopo kitandani, nae ana hamu ya kumuona mtoto wake,...
Sasa sheby kumuona tu mama yake kaamka akamkimbilia
"shkamoo mama, hali yako vp"
"salama tu,.. Vp baba shingo yako imepona"
Sasa mama sheby alipouliza hivyo, mke wa rais akadakia
"nimeshamuuliza mtoto wangu kuhusu shingo yake, mfuate mtoto wako kule jamani wewe mama Joseph"
Yaani huyu huyu mama Joseph ndio anamuita mwenzie mama Joseph, yaani kila mtu anamtaka sheby kuwa mtoto wake.... Hata mheshimiwa rais akaona hapa kuna utata, bora ukweli unge endelea kuwa siri...
"hebu nyamazeni, nyie si marafiki toka zamani nyie? Sasa mnagombania nini... Wacheni ujinga"
Aliongea rais huku sheby akiwa zaidi upande wa mama aliomzoea,...
Hata leah anashangaa sheby ana wamama wawili, hajui nini sababu
"huyu ni mtoto wangu"
Aliongea mama sheby, huku mke wa rais nae akasema
"mimi ndio mtoto wangu, kama huamini tumuite dokta aje"
"mimi simtaki huyo dokta wako"
"utamtaka tu hata kwa lazima"
Sasa majibizano yakawa mengi sana hapo hospitalini,... Rais kavuta kibao na kumpiga mkewe
"mke wangu angalia usije ukawa jipu, huyu mtoto kamzoea mama yake... Sawa huyo kijana ni mtoto wetu kwa ukweli unavyo dhihirisha, lakini nae ana uchaguzi wake... Mbona mimi sipigi kelele"
"sawa mheshimiwa rais, lakini huyu ni mtoto wetu"
"sawa najua, lakini hawawezi kuachana hao wameshazoeana"
"baba sheby, uje nyumbani sawa baba"
Aliongea mke wa rais huku wakiondoka... Sasa walipo ondoka leah akamuuliza sheby
"we baby, ina maana una wamama wawili"
"hapana, mama yangu ni huyu hapa"
Leah alishindwa kuelewa kitu hapo.. Basi walitoka nje kwenda kumnunulia mama matunda,
"sheby mpenzi wangu? wewe ni mtoto wa rais"
"ndivyo inavyosemekana"
Basi zoezi la kununua matunda sokoni liliendelea,... Lakini ghafla leah kawaona wale rafiki zake huku sokoni,... Leah kwa heshima akamwangalia sheby, kama vile anamuomba akawasalimie, sahi alimruhusu

"heeee leah umekuwa wa tofauti siku mbili tu"
"we acha tu jack,.. Mwenzio sasa hivi ni mchumba wa mtu"
"weweeee muongo"
"kweli"
"afu yule mkaka jana tulimuona kwenye tv, tukasema nawe huenda tukakuona"
"weeeee, Bado sijajulikana kwao, ila kwetu tayari"
"mmmhhhh umefanya haraka nawe"
"nampenda hata hivyo"
"tunajua, mana toka siku ile ulikuwa unameza mateeee"
"ni mtoto wa raisi yule, hivyo nina kibarua cha kumlinda"
"Whaaaat, ati ni mtoto wa nani"
"ina mana hujaskia au"
"leah wewe umeokota dodo kwenye shamba la miwa leah"
"bwana jack, baadae, spendi kumuuzi naombeni Niende, ila nawasihi sitaki tena muendeles na hio kazi, kuanzia leo... Nitamuomba mpenzi wangu anifungulie biashara yeyoye ile, nitakuwa nanyi pamoja.. Ila acheni hio kazi, na kuhusu kula niachieni mimi na kodi ya nyumba niachieni mimi, staki muende shivaz tena"
"leah we nenda, sisi tumekuelewa... Nenda usije kuandikwa kwenye magazeti mke wa mtoto wa rais kakutana na machangudoa.. Nenda wewe, shilawadu hawakawiii"

Hospitali wakiwa wanafikisha matunda ya mama, yena leah ndie aliokuwa akifanya kazi hio,..
"sheby mwangu... Mbona hunitambulishi"
Aliongea mama yake, kuwa mbona hamtambulishi huyo mschana
"ahahahahaa mama bwana... Bado mapema mno, ila wacha ujue tu,... Anaitwa Leah"
"najua mwanamke hana dini, lazima awe mkwe wangu huyu"
Basi ilikuwa ni furaha, lakini ukweli ni kwamba mama yake sheby ni mke wa raisi, na baba yake ni raisi GU,.. Sema keshamzoea mama yake, na mama pia kamzoea mtoto wake hivyo kukubali tu kuwa sawa ni mtoto wa raisi, hapo ndipo mahali pagumu mno.... Hawezi, hivyo ataendelea kuishi na mama yake huyu lakini wazazi wake wa kweli wapo...

Hospitalini Joseph anauguza miguu mana ilivunjwa kwa risasi, na akipona ni gerezani,.. Mr nyange yupo ndani ya kifungo cha maisha mana alikuwa akihujumu mali ya serikali na General mwenzie mr deo, hivyo wana kifungo cha maisha tena ikiwezekana kunyongwa kabisa..

Dom imeshapelekwa Germany, tusubirie noti ya laki moja ya Tanzania..... Subira huvuta kheri shekhe... Tusubirini tu

MWISHO WA SON OF PRESIDENT GU
 
Back
Top Bottom