Makapuku Forum

Duniani Kuna mambo mengi ya kushangaza, babe

Endelea kutujulisha
 
4/ achana na mashindano ya kuendesha baiskeli tunayoyaona kila leo, je wamjua alievunja rekodi ya dunia kwa kuendesha baiskeli chini ya maji?



Si mwengine bali ni bw. Vittorio Innocente, huko Santa Marghenta Ligure, Liguria, Italy (loh mjini kuna miji jamani
)

Alivunja rekodi hii akiwa na miaka 62, umbali alioundesha chini ya maji ulikuwa (110 m) sawa na (214 feets) aliendeshea bahatpri ya Mediterranean alichukua dakika 9 tu kuendesha kwenye maji




Alipohojiwa kuhusiana na chanagamoto gani alipitia akiwa anaendesha baiskeli hiyo alisema, ilikua ngumu kwake kuendesha kutokana na matope mengi ambayo hakua ameyategemea kukutana nayo huko chini ya maji

Ni rekodi alieivunja kwa mara ya pili baada ya kwanza miaka sita iliyopita, na aliendesha kwa umbali wa (60 m) sawa na (197 ft)

Iliingia rasmi kwenye kitabu cha orodha za waliovunja rekodi zaidi duniani 21 July 2008 huku Bw. Lucia Sinigagiles judge kutoka huko huko World Guinness Records akishuhudia rekodi hiyo akitokea London



Madame S
 
5/ je uwamjua mtu mrefu na mfupi zaidi duniani?

He Pingping akitokea Mongolia aliweza kuvunja rekodi ya kua mtu mfupi zaidi duniani akiwa na kimo cha urefu wa (74.61 cm sawa na 29.3 inches) akionekana hapa chini kusimama katikati ya miguu nya mdada mrefu zaidi duniani



Alikua ni mtoto wa tatu akiwa mtoto wa kiume pekee kwenye familia yao

Alizaliwa akiwa mdogo na ukuaji wake ulikua wa taratibu sana



Alifariki baadae akiwa na miaka 21 mwaka 2010 kwa maradhi ya moyo

Pingping alivunja rekodi hii ya kua mtu mfupi zaidi duniani mwaka 2008

Mtu mrefu zaidi duniani
Ni mwanamama Svetlana Prankratova kutokea Russia, ana urefu wa (1.96 m) alizaliwa huko Volgograd, Russia na alishawah kucheza mpira wa kikapu kama basketball chuo mojawapo huko Virginia

Miguu yake peke yake ina urefu wa (51.9 inches) aliolewa baadae na bwana Jack Gosnell na akaacha rasmi kucheza mpira huo na kua kocha wa mpira huo shule ya wasichana iliyojulikana kama George Mason



Kabla ya kuolewa, mama huyu alipopata ushindi wa kuvunja rekodi ya mtu mrefu kwa upande wa kina mama duniani, aliukizwa ni changamoto gani anapata akasema changamoto kuu aliyokua akipata kwa wakati ule ni wanaume kumkimbia na kumwambia hawawez kusimama na mtu mrefu kama yeye mda mwengine ilikua ngumu kwake kuopata nguo sahihi za kulalia kutokana na urefu wake

Kwa leo ni hayo tu tukutane siku nyingine

Jumaa Mubaraq!

Madame S
 
Watu na rekodi zao
 
Dah
 
Huyu ana balaa
 
Asante sana wifi ake
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…