Makapuku Forum

Makapuku Forum

International Left-Handers Day.

Tarehe 13 mwezi wa 8 ni maazimisho kwa watu wanaotumia mkono wa kushoto kufanya kazi zao badala ya mkono wa kulia. Kwa mara ya kwanza maadhimisho haya yalifanyika mwaka 1976 wezi na tarehe kama ya leo.

Haya maadhimisho yalianza rasmi ili kuonyesha uwepo wa binadamu hawa wanaotumia mkono wa kushoto katika ulimwengu uliotawaliwa na mifumo inayopendelea watumiaji wa mkono wa kulia. Wakati mwingine watumiaji wa mkono wa kushoto wanapata sana taabu kutumia vitu vyenye mifumo ya mkono wa kushoto. Mfano Kuendesha vyombo vya Moto, Kutumia Silaha,Kuandika na n.k.

Katika tafiti nyingi zilizofanyika inaaminika asiliamia 10% ya watu wote duniani ni left-handers( watumiaji mkono wa kushoto). Kwa hesabu za mwezi August mwaka 2017, dunia ina idadi ya watu 7,500,000,000 (billion Saba na nusu). Asilimia 10 ya watu 7,500,000,000 ni watu 750,000,000 ( Milion mia saba na hamsini).

Mambo ambayo hukuwahi kuaysikia juu ya Left-Handers (Watumiaji wa mkono wa kushoto), Baadhi ya mambo yako proved kabisa lakini mengine ni imani tuu juu ya watu hawa adimu.

Yako zaidi ya 10, ila nitelezea hadi pale nikapoona nimecover sehemu kubwa.

Namba.1.


Lefties, wanaaminika kuwa ni wachoraji wazuri zaidi ya right-handers, watumiaji wa mkono wa kushoto ni mahiri katika kuchora, wengi wao wanachora picha ya mtu akiwa anaangalia upande wa kulia.



Ahsante mdau
Hata home yupo left hander
Nakumbuka utotoni alikuwa anachezea bakora balaa kisa anakula na kusalimia kwa mkono wa kushoto
Matokeo yake akajilazimisha kutumia yote now anachanganya tu mokono na tumemzoea yaani mikono yake yote inapiga kazi
Ni faida !!!
.......
 
International Left-Handers Day

Namba 2

Shetani anaaminika kuwa ni left handed. Neno lyft, ndio limezaa neno left likiwa na maana ya dhaifu. Katika lugha ya kilatini neno sanister linamaanisha "left handed" au awkwardnes, mkono wa kushoto umekuwa ukihesabika kama mkono wa mkosi au wa bahati mbaya. Kubwa zaidi wachoraji wa picha ya kufikirika ya shetani yaai devil wamekuwa wakiichora na kumpa muonekano wa kuwa yeye ni mtumiaji wa mkono wa kushoto. Yaani shetani anaamikia kuwani left handed.

Hii noma
Ndo nasikia leo
.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom