Makapuku Forum

tena maji ya kutoka kwenye mtungi jaman maji yakiwekwa mule ya baridiiii
 
Habarini za asubuhi.. Habarini za Jumapili... Naamini mmeamka salama wote..

Tumshukuru Mungu kwa kila jambo, hali ulonayo ni mpango wa aliye juu, mtukuze Mungu ukiwa u hai. Acha kulia, acha kulalamika, acha kuhuzunika Mungu anaenda kukutatulia yote..... Mungu Wangu hajawahi kushindwa, yeye anashughulika na kila kitu.... La mnoo ni kumshukuru kwa kila hali...

Mungu wangu awape haja ya mioyo yenu
 
Neno la leo

Wabarikini wale wanaowatesa, barikini wala msilaani. Furahini pamoja na wenye kufurahi, lieni pamoja na wale waliao.

Kaeni kwa amani ninyi kwa ninyi. Msijivune, bali mwe tayari kushirikiana na wanyonge. Wala msiwe watu wenye kujivuna kwamba mnajua kila kitu. Msimlipe mtu ye yote ovu kwa ovu. Jitahidini ili mtende yaliyo mema machoni pa watu wote. Kama ikiwezekana, kwa upande wenu kaeni kwa amani na watu wote.

Wapendwa, msilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa: “Kisasi ni juu yangu, mimi nitalipa, asema Bwana.” Badala yake: “Adui yako akiwa na njaa, mpe chakula; akiwa na kiu, mnyweshe. Maana ukifanya hivyo, utampalia makaa ya moto yanayowaka kichwani pake.” Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.

Warumi 12:14‭-‬21

MUWE NA JUMAPILI ILIYO NJEMA NA ASUBUHI NJEMA MBARIKIWE SANA
 
Ameen Mungu ni mwaminifu kwa kweli
 
Amen
Be blessed my little sister...
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…