Muziki: Ijumaa ya Watu Wazuri
Nilitaka nimwage salamu ndefu sana Furahiday hii lakini kutokena na ukweli kwamba imeangukia siku ya kusheherekea bia kwa wanywaji basi nitajiaminisha tu kuwa uko poa kabisa na wikend umeianza vizuri. kama imekaa ndivyo sivyo usihofu, jipange.
Ninapowataja wadau kwa kuliamsha na kulichangamsha Jukwaa hili sio kwamba napenda tu kutajataja majina kama rapper wa kikongo, la, nawashukuru
shululu kwa magazeti,
lee empire kwa BBC,
Shunie kwa Sala, mtaasisi mwenzangu
Nyagei kwa kutuspotisha. Siwez kukosa historia
Jimena ikichagizwa na picha na baadaye 10 kubwa za
Bitoz , hadithi ya komandoo
husna muba na top ten ya biere, monde, dawa ya tumbo, bia na
Transcend (BTW, miaka hiyo zamani kule US kulikuwa na kitu kinaitwa Prohibition- bia na vilevi vilipigwa marufuku na mwaka 1933, March rais FD Roosevelt akasaini sheria ya kuodoa marufuku hiyo. Asanteni wadau
Siwezi kuacha kutambua mchango wa wageni wote na ni jambo zuri kukuona tena
Mndali ndanyelakakomu ,
Clkey ,
Tumosa ,
dumejeuri dingimtoto mzeewakungoa shedede SHIMBA YA BUYENZE ,
Lyon Lee Sakayo demi ,
koncho77 ,
Madame S na wote mlioshiriki katika sogozi hadi kufikia muda huu ambapo nakuja na burudani ya muziki.
Muziki sasa, kuna ladha za muziki ambazo japo unaweza kuziita ni za zamani lakini ukizisikiza leo bado utasema huu ulikuwa ndo muziki. yeah na miaka hii sasa upate fursa kama yangu unasikiza huku pembeni una uhakika wa kufurahisha mwili na mkononi umekumbatia chupa ya safari inayoogopa ukungu, ni furahiday leo na kila mmoja wetu ni mzuri na kama huna mashaka na uzuri wako tembea mtupu
Burudika leo ni furahiday na usiifanye siku hii kuwa ngumu sana