Makapuku Forum

TOP TEN
Week end huanza ijumaa ila kwa huku Uswahilini kwetu kila siku ni week end ila siku hizi gongo/pombe mchana marufuku,bangi nayo ishakuwa dawa ya kulevya,kucheza pool table nako kuna masharti bila kusahau vigodoro vishapigwa marufuku....stress tupu
Kama kawaida yetu week end hakuna siasa wala nini ni kush lawadu zaidi
Tuangalie wacheza filamu 10 matajiri wa kiume(actor)
Ieleweke utajiri wa mtu ni tofauti na umri hivyo hupanda na kushuka pia hutofautiana kwenye source/vyanzo vya habari hivyo niandikacho ni kutokana na chamzo kimoja nilichokichagua
Hivyo mimi sio auditor ......niandikacho sio sheria

karibuni
.........
 
Asante
 
10/Adam Sandler Ana umri wa miaka 50
Alizaliwa Brooklyn jijini New York....mama yake alikuwa ni mwalimu halafu dingi mhandiesi wa umeme
Ana asili ya Urusi na Uyahudi Alianza kuwika akiwa na miaka 17 kwa kuanza na yale mambo ya Masanja na Joti
Kacheza filamu kibao na hivyo kuingiza mpunga wa maana na kubeba tunzo

Anakadiriwa kuwa na utajiri wa USD 350 milioni
.......
 
9/Clint Eastwood
Huyu ni babu haswa yule Le Mutuz mnamsingizia tu mwacheni ale bata....Eastwood ana umri wa miaka 87
Ni mzaliwa wa San Franciscoaba take alikuwa ni mfanyakazi wa kiwandani wakati mama yake ni mama wa nyumbani yaani golikipa Huyu ni nguli haswa kacheza filamu kibao pia ana vitega uchumi vya kueleweka piga hesabu tangu enzi hizo jamaa alikuwa anapiga tu hela

Anatajwa kuwa na mpunga wa USD 370 Milioni
.......
 
8/Bill Cosby Babu mwingine kwenye list .....ana umri wa miaka 80
Tofauti yake ni Eastwood ni tabia tu,Bill Cosby anTajwa kwenye kashfa kibao za kunyanyasa watoto wadogo min nsia(kubaka/kulawiti Nafikiri mnakumbuka vipindi vyake zamani pale ITV jamaa anachekesha kivhizi ila elewa yupo kikazi zaidi

Anakadiriwa kuwa na mkwanja wa USD 380 Milioni
......
 
7/Tom Hanks
Ana. Umri wa miaka 61
Babayake alikuwa ni mpishi akati mamaye alikuwa ni mjanjamjanja sijui alijishughulisha na nini
Filamu yake ya The Da Vinci Code ilikuwa matata na kumuingizia mpunga wa maana
Ila pia ana michongo kibao na majumba ya kifahari

Anatajwa kuwa na mpunga unaofikia USD 390 Milioni
......
 
6/Jack Nicholson
Ana umri wa miaka 80
Ni mcheza filamu,mwongoza filamu na mwandika script mahiri
Kacheza filamu kibao ikiwapo ya The Shining ambayo ilivuma
Ni mshindi wa The Academy Award na tunzo zingine kibao
Anatajwa kuwa na utajiri wa USD 400 Milion
..................
Zitaendelea baadaye
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…