Barcelona watatumia fedha za mauzo ya Neymar kwa kumsajili kiungo mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 26, na Philippe Coutinho wa Liverpool. (Daily Mail
Meneja wa Man Utd Jose Mourinho angependa kusajili wachezaji wengine watatu kabla ya dirisha la usajili kufungwa, hata hivyo United inaarifiwa wamekata tamaa ya kumsajili winga wa Inter Milan, Ivan Perisic. (Daily Express)
Meneja wa Atletico Madrid Diego Simione ameiambia bodi ya klabu yake kuwa lazima wamsajili Diego Costa, 28, ambaye Chelsea wanasema anauzwa kwa pauni milioni 50. (Evening Standard)
Beki wa Southampton anayenyatiwa na Liverpool Virgil van Dijk, 26, anakaribia kulazimisha uhamisho wake. (daily Mirror)Kiungo anayesakwa na Liverpool Naby Keita, 22, huenda akakataa kusaini mkataba mpya na timu yake