Makapuku Forum

Makapuku Forum

Kutana na Rais mpya wa Mongolia aliyeapishwa siku chache zilizopita, Battulga Khaltmaa. Ni mcheza mieleka na bingwa wa dunia wa karate. Ana haja ya kuzungukwa na utitiri wa mabodigadi?
20b44fa4995017dbe99a293439f4e5a8.jpg
Mganga hajigangi

....
 
HAYA NDIYO MAISHA HALISI NDANI YA GEREZA GHALI ZAIDI DUNIANI LA GUANTANAMO.

Ni gereza linaloendeshwa kwa
fedha nyingi za walipakodi
nchini Marekani. Mwanzoni mwa mwaka 2002, washukiwa wa mwanzo kabisa wa
ugaidi wa kimataifa walipelekwa
katika gereza lililojengwa katika
Kituo cha Kijeshi cha Kimarekani cha
Guantanamo nchini Cuba, kutokana
na amri ya Rais George W. Bush.

Rais wa Marekani aliyefuata, Barack
Obama, licha ya kuahidi kwamba
atalifunga gereza alipoingia
madarakani mwaka 2009, jambo hilo
halijafanyika hadi sasa.

George Bush alihisi kwamba
Guantanamo, kipande cha ardhi cha
eneo la kilomita 120 za mraba, ndipo
mahala panapofaa kabisa
kuwazuwia wale watu iliowaona
kuwa ni wakorofi kabisa na
inaowashuku kuwa ni magaidi sugu.

Utawala wa Marekani baada ya
mashambulio ya Septemba 11, 2001,
iliwaita watu wa aina hiyo,
‘wapiganaji maadui’, tofauti na
wafungwa walio wahalifu wa
kawaida.

Msamiati huo ulitumiwa kama njia
ya kuepuka kuwataja watu wa aina
hiyo kuwa ni wafungwa wa kivita,
ama sivyo wangekuwa na haki
zinazotakiwa wapewe kwa mujibu
wa sheria na mikataba ya kimataifa.

Januari 20, 2002 washukiwa wa
kwanza 20 walipelekwa Guantanamo
kutokea Afghanistan na Pakistan,
ikiashiria namna Marekani
ilivyovinjari kuingia katika kile
ilichokiita ‘Vita dhidi ya ugaidi.’

Wafungwa walioko sasa katika jela
hiyo wanaishi katika majengo ya
kisasa pembezoni mwa kituo hicho
cha kijeshi. Kuna madaktari na
wauguzi 100 wanaowashughulikia
wafungwa 132 walioko hivi sasa,
licha ya kulindwa na wanajeshi
2,000.

Walinzi katika jela hilo walisema
wamepewa amri wawafanyie “utu”
wafungwa na wahakikishe usalama
wao, lakini washukiwa hao wa
ugaidi, miongoni mwao wako
waliozuiliwa sasa kwa zaidi ya
miaka kumi, wana hadithi nyingine.
Hivyo ndivyo wanavyosema
mawakili wao.

Wafungwa kadhaa kati yao walisusia kula na ilibidi walishwe vyakula kwa nguvu.
Wafungwa hao hawaruhusiwi
kuzungumza na waandishi wa
habari. Pia, kanuni za usalama
zinawapiga marufuku walinzi
kuzungumza na vyombo vya habari.

Hairuhusiwi kuyapiga picha majengo
wanamoishi wafungwa. Hizo ni
amri, Hazina mjadala, japokuwa
walinzi wanadai hali ya mambo
katika gereza hilo ni bora kuliko
ilivyo katika magereza ya aina hiyo
huko Afghanistan na Iraq.

Guantanamo Siyo mali ya
Marekani wala siyo ya Cuba, pia ni
mali ya nchi zote mbili. Kwa miaka
mingi mahala hapo palitumiwa na
wanajeshi wa Marekani kutia mafuta
na kuzikarabati manuwari zao.

Mwaka 1903 Rais Tomas Estrada
Palma wa Cuba alilikodisha eneo hilo
lililoko karibu na bahari kwa
Wamarekani. Lakini pale Fidel
Castro alipoingia madarakani huko
Havana mwaka 1959 mambo
yalibadilika.

Japokuwa Marekani hadi sasa inalipa
kodi yake ya Dola 4,000 kwa mwaka,
lakini watawala wa Cuba
hawazipokei fedha hizo kwani
kufanya hivyo kutamaanisha
wanatambua kukaliwa ardhi yao na
Wamarekani, jambo ambalo
wanalipinga kabisa.

Kwa wenyewe wanajeshi wa
Kimarekani, Guantanamo ni kama
pepo. Ni kama mji mdogo wa
Marekani unaopendeza. Kuna
mkahawa wa McDonald, sinema
zinazoonyesha ni filamu za
Marekani, duka kubwa, uwanja wa
michezo na shule kwa watoto wa
wanajeshi.

Tangu jela hilo ilipoanzishwa,
wafungwa 780 wamezuiwa.
Mjerumani Murat Kurnaz aliwahi
kushikiliwa huko kwa miaka mitano
na kuhojiwa.
Katika kitabu alichoandika baada ya
kuachwa huru alisimulia kuhusu
kuteswa na kwamba kila alipotaka
kusali alidai kwamba zilipandishwa
sauti kali za muziki zimsumbue.

Shirika la Kimataifa la Amnesty
International linalopigania haki za
binadamu lililaumu hali ilivyo katika
jela hilo na limelitaja jela hilo kuwa
ni kashfa kubwa kwa haki za
binadamu.

Pia Umoja wa Mataifa
umeikaripia Serikali ya Marekani
kutokana na makosa yanayofanywa
katika gereza hilo.

Kuna watu walioshikiliwa
Guantanamo kwa muda wa zaidi ya
miaka kumi bila ya kusikilizwa
mashtaka ya makosa wanayoshukiwa
kuyafanya. Jambo hilo amekiri pia
Rais Obama. Siku mbili baada ya
kuingia madarakani Januari 2009
alitangaza kwamba anataka
kulifunga gereza hilo.

Jela ya Guantanamo ni mzigo
mkubwa kwa walipakodi wa
Marekani. Linawagharimu Dola 400
milioni kila mwaka kuliendesha,
yaani Dola 2.6 milioni kwa kila
mfungwa. Mtu mmoja aliyoko chini
ya ulinzi mkali ndani ya jela ya
Marekani hugharimu kutumiliwa
kiasi ya Dola 34,000 kila mwaka.

Licha ya gharama kubwa, wabunge
wa Chama cha Republican na
wachache wa kutoka Chama cha
Democratic bado wanataka libakie
hivyohivyo.

Inaaminika kwamba hata pale karibu
wafungwa wote wasiokuwa wa hatari
watakapoachiliwa wameachiliwa,
bado kutabakia wachache ndani ya
gereza hilo.

Hao ni wale wanaokabiliwa na
mashtaka kama vile Khalid Sheikh
Mohammed aliyeongoza mipango
iliyofanikisha mashambulio ya
Septemba 11 huko Marekani. Watu
wa aina hiyo watatakiwa wajielezee
mbele ya mahakama ya kijeshi.

Huenda wakabakia vizuizini maisha
yao yote. Haitarajiwi kwamba
watakuwa huru, wao wanaonekana
kuwa ni hatari mno, licha ya
kwamba hakuna ushahidi uliowazi
wa kuwafanya wapatikane na hatia
mbele ya mahakama.

Kwa wabunge wa Marekani wa
Chama cha Republican wanaamini
mahala panapofaa kwa watu hao ni
Guantanamo tu na siyo kwingine.

Habari Forums.
13c4904d3fb088477c8da360d7910186.jpg
fa4e0c1b04ff367a9d06504496e38ad6.jpg
0cb0e5cc4a643aa01c7aedb4d08bcd20.jpg
3e3e9474cea6e20b8a60529dad64fe28.jpg
ac325e96883d8ccf46540d5859178ef3.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom