SEHEMU YA 20
..............Hali ilitisha sana nililia mno kuona unyama ule na siku ya tatu walinilazimisha na mimi kumuingilia mdogo wangu wa kike. Niliwavaa kwa hasira punde tu waliponifungua minyororo na ndio sababu ya kovu hili unaloliona usoni. Kilikuwa ni kisu kilichokuwa na moto ambacho alinibandika nacho shavuni mmoja wa wale watesaji wa Mr. X pindi nilipotaka kwenda kinyume nao. Nilikuwa tayari kufa lakini si kumuingilia dada yangu wa tumbo moja! tena mbele ya mke wangu, mwanangu na wazazi wangu!? Aaaah Mr X ni jina nisilokuja kulisahau hadi siku ya kufa nitamshtakia kwa Mungu kwa aliyotufanyia kwenye maisha yetu.
Walipoona wamenitesa hadi nikawa hoi huku msimamo wangu ukiwa vilevile ndipo amri ya mr X ilisikika kwamba waniache. Nilijua yamekwisha lakini alichowaamrisha kilikuwa kibaya zaidi na cha kinyama. Yaani kunitesa kote wakaona haitoshi na kuitii amri ya Mr. X kuwa wamuingilie kwa pamoja dada yangu. Tena mbele yetu bila huruma. Aaaaaaaaaaagh!!!! iliniuma sana niliposikia kelele za maumivu toka kwa ndugu yangu lakini sikuweza kutoa msaada wowote zaidi ya kufumba macho na kulia kwa uchungu. Walipomaliza wale wawili akaja na yule watatu na kumuingilia tena kupitia njia iliyoharamishwa. Nililihisi hilo kutokana na harufu kali ya kinyesi iliyokuwa ikisikika na majuto ya sauti ya maumivu ya ndugu yangu. Hakuna kati yetu aliyeweza kuuangalia unyama ule wala aliyeweza kuzuia machozi kumtoka. Mke wangu tu alizimia zaidi ya mara mbili kwa uchungu wa moyo na mateso.
Ki ukweli ilituuma kupita maelezo na hatukumjua huyo Mr. X wala hatukujua kwanini aliamua kutuma vijana wake kututeka na kutudhalilisha kiasi kile. Baadae walikuja watu wengine nao wakiwa wamevaa kininja ila mmoja wao alikuwa mwanamke. Nilimtambua kutokana na sauti pindi walipofika na kuongea na wale walinzi wengine. Niliwashuhudia wakimchoma sindano ya shingo baba na baada ya muda mfupi alinyong'onyea na kuanguka. Ndipo walipomfungua na kumbeba kisha kuondoka naye sehemu isiyojulikana na hatukumuona tena kurudishwa siku hiyo.
Tulilia sana na kutilia mgomo hata chakula walichokuwa wanatuletea na kutulisha tukiwa kifungoni. Tuliamini washamuua baba basi na sisi bora watuue tu. Lakini baada ya siku mbili walikuja tena wale watu na kutuchoma sindano zilizotufanya wote kupoteza fahamu kama ilivyokuwa kwa baba. Tulipokuja kustuka ajabu tulijikuta tupo nyumbani tukiwa tumelala huku pembeni yetu tulimuona baba akiwa amekaa akilia kwa uchungu.
Ilikuwa kama sinema kwa kweli wote tulijikuta tukilia kwa nguvu kama watu waliopata habari ya kifo cha ghafla kwa mtu waliyempenda na kumtegemea. Kila mmoja alikimbilia vyumbani kwa aibu hasa majirani walipokuja kutugongea kwa taharuki. Ilikuwa ni usiku mkubwa tu. Baba alitoka na kuzungumza na majirani akiwambia kuwa tulifiwa na ndugu yetu huko Mbeya. Aliporudi ndani alituita na kutusihi tunyamaze tusije kusema kwa yeyote kwa yaliyotukuta. Kisha akatwambia tusiwe na hofu tukalale ila kesho yake kila mmoja apange vitu vyake vizuri kwa kujiandaa na safari ambayo hatukujua ni ya wapi.
Kweli tulijiandaa na usiku wa siku ya pili tulipomuuliza baba juu ya safari hiyo na kwanini tulitekwa na wale watu na huyo mr X? ni nani na yeye aliponyeka vipi mikononi mwao na kwa nini wametuacha? Maswali yalikuwa mengi na tulimuuliza ili tupate majibu kwanini pia hataki hata kutoa taarifa polisi. Chaajabu maswali yote baba alitujibu kwa ufupi sana tena alifoka na kuwa mkali mno pindi alipoona mtu akimuhoji zaidi. Alitwambia kuwa tulikuwa mateka wa Mr. X kwa sababu yake na alipochukuliwa siku ile alienda kukutana na huyo Mr. X na usalama wetu pia umepatikana kwa sababu yake. Akasisitiza zaidi tufanye na tufuate vile alivyotuelekeza huku akituonya asije kuthubutu yeyote kati yetu kumwambia mtu juu ya kilichotukuta na hata kulitaja hilo jina Mr. X kama tutapenda kuendelea kuishi.
Hatukuwa na chaguo baada ya hapo ndipo siku ya tatu lilikuja kundi la vijana waliokodiwa na baba kutusaidia kubeba mizigo na kupeleka eneo lilipoishia roli lililotusafirisha mpaka hapa Mkuyuni.
Sikujua baba amepataje pesa nyingi kwa haraka vile hata kuweza kuhama na kununua nyumba muda mfupi hapa Mkuyuni. Lakini furaha iliyeyuka ndani ya familia mawazo na unyonge ukatawala kwa kila mmoja. Baada ya mwezi mmoja mama mlezi alifariki ghafla na moja ya sababu za kifo chake baada ya uchunguzi wa daktari ni mawazo ya muda mrefu. Na hii ilitokana hasa na tukio lile la kutekwa na Mr X ambalo lilibaki kuwa siri yetu na pia vitendo alivyofanyiwa kule tulipotekwa.
Kama hiyo haikutosha kumaanisha kiasi gani Mr. X ameharibu saikoloji za familia yetu ni baada ya mdogo wangu yule wa kike aliyebakwa na kuumizwa na wale vijana, kuanza kupata maradhi ya mara kwa mara ya kichwa na kifafa. Aliugua na tukamuhangaikia kwa miaka mitatu baadae mwishowe alirukwa kabisa akili na kuchanganyikiwa. Tatizo lake nalo halikutokana na uchawi bali nina hakika ni vile vitendo alivyofanyiwa kwa Mr X.
Moyo wangu unamchukia sana tena saaana Mr X na naomba siku zote kama amekufa Mungu amzidishie adhabu kali zaidi huko alipo.
Moyoni nilieka nia ya kulipiza kisasi na mara nyingi nilipenda kumpeleleza baba apate kunambia huyo Mr. X ni nani hasa. Lakini hakuna nilichoambulia zaidi ya siku moja aliponambia kuwa namfahamu vizuri huyo mtu kwani alikuwa ni mmoja wa wateja zake wa zamani. Lakini nilishindwa kumfikiria na kujua ni nani kutokana na wingi wa wateja niliokuwa nawapokea pale kijiweni.
Hata nilipomchimba maswali zaidi baba bado alikuwa mgumu na m'bishi mno kumuanika mtu huyo aliyetudhalilisha. Sikujua kwanini baba aliogopa kiasi kile hadi kutusema, kutuonya na kutuhadharisha mara kwa mara kuwa tusahau habari za Mr. X kwasababu tutaponyanyua ulimi kuzitaja hadharani basi tutakuwa tumejihatarishia maisha yetu na hakuna atayetuokoa.
Basi mwanangu miaka ikasonga hadi hii leo maisha yanasonga kila mtu amesahau habari za huyo Mr X ingawa jina lake limebaki kuwa siri ya sisi watu wanne tulio hai japo kovu lake mioyoni mwetu bado lipo. Ukweli hakuna aliyejua siri ya kuwa Mr X ni nani zaidi ya baba mwenyewe mzee Mnyungunyungu na endapo akifariki ndio basi na ukweli unaoutafuta utakuwa umekufa rasmi.
||..........................||
* * * * * *
Alimaliza yule mzee huku akifuta machozi yaliyokuwa yamemchafua uso. Kamishna alishusha pumzi akiichekecha akilini hadithi hii iliyomfanya kwa mara nyengine adondoshe chozi na kuijenga chuki zaidi na shauku ya kujua huyo mr X. Alimpa pole yule bwana kwa yaliyowakuta. Alielewa sasa sababu za kuhama kwao hata akapata taswira ya picha kwa kuunganisha hadithi ya Hussein. Alibaini kichwani mwake kuwa baba mkubwa hakumsaliti kwa makusudi mwanae kutokana na ushahidi alioutoa pale mahakamani.
"Inawezekana alimkandamiza Hussein kwania ya kuikomboa familia yake iliyokuwa mikononi mwa Mr. X ambaye ndie alikuwa adui wa Hussein babu bubu." Alisema nafsini.
Lakini swali bado lilibaki pale pale kuwa huyo Mr. X alikuwa nani?
Jibu hili aliamini ni mtu mmoja tu ndiye analo ambaye sasa ni mzee aliye hoi taaban wa maradhi. Ingawa aliambiwa haikuhitajika kumsumbua mgonjwa lakini hakuwa tayari kusubiri. Alijua mzee Mnyungunyungu ndiye anaweza kumfunulia siri walau kidogo hata ajue jina halisi tu na kazi aliyokuwa anafanya huyo mr X. Alijua pasipo vielelezo vya uhakika hatoweza kuifufua kesi ile wala kumsaidia Hussein. Alichohitaji ni ushahidi yakinifu utaoeleweka mbele ya mahakama. Aliamini akifanikiwa kuitoa siri gizani ataonekana shujaa mbele ya serikali lakini kama atakurupuka na kushindwa ataonekana mzembe kiasi gani kwa kuyaamini maneno ya mfungwa tena wa miaka mingi juu ya kesi iliyokaribia umri.
Bado aliamini ni sehemu moja tu na ni mtu mmoja tu awezae kumpa mwanga kwenye njia ya kiza anayotaka kupita kwenda ulipo ukweli wenyewe. Aliwaza endapo atafanikiwa kumjua Mr.X na kumkuta angali yu hai basi yeye ndiye atafumbua mafumbo yote na kuutoa utata utatani.
"Hakuna ujanja wa kuupata huu mwangaza zaidi ya kuongea na Mzee Mnyungunyungu walau maneno machache tu. Nitafanya kila mbinu ili azungumze." Alitafakari kichwani mwake Kamishna Shebby.
"Mzee wangu naomba nipelekwe nikamuone tu Mnyungunyungu." Alisimama na kusema akiwa tayari kwenda huko alipo mgonjwa. Lakini kabla hajajibiwa kitu na yule bwana mara aliingia yule kijana aliyewapokea pale nje na kuita.
"Baba .. babaa.. kuna wazee wamekuja Unahitajika haraka nyumbani babu amezidiwa sana.." Maneno yake yaliustua mno moyo wa Kamishna Shebby na kukurupuka haraka nje. Yule bwana mganga naye alinyanyuka na kutoka. Wote waliishika njia kuwahi huko alipo mgonjwa huku moyoni kamishna Shebby akisali na kuomba mzee Mnyungunyungu asifariki kabla hajamwambia Mr X alikuwa nani.