Makapuku Forum

nakuonaaaa unarembuaaa au ushagongA balimi?
 
1 SAMWEL 25

6.Na hivi ndivyo mtakavyomwambia huyu aishie salama,Amani iwe kwako,na amani nyumbani mwako,na Amani kwao wote ulio nao

Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu BWANA MUNGU wa Majeshi asante kutufikisha umbali huu,umetulinda mchana kutwa umetuepusha na hatari mbalimbali na ajali mbalimbali ,BABA tunaomba tusamehe yote tuliyotenda kwa mawazo,maneno na matendo kwa kukusudia au kutokusudia..tunawasamehe wote waliotukosea ili tuweze fanya toba ya kweli maana BABA tunakiri udhaifu sisi ni watu tu kuna wakati tunaghafilika..nyoosha mkono wako BABA uturehemu twakusihi BABA mwema ili tuende vitandani tukiwa salama na amani toka kwako.Asante kwa kuwa unatusamehe kila iitwapo leo.

BABA tunakualika usiku wa leo tuma malaika wako walinzi watuzingire,watulinde,tuzingire na ukuta wa moto wa damu ya Yesu,utukumbatie kama kuku anavyokumbatia vifaranga vyake.

Usiku waleo endelea kutuponya mioyo iliyopondeka,magonjwa,dhiki,taabu na kukata tamaa..tusaidie tuzidishe upendo kwa wale tunaodhani ni maadui wetu ili tuweze kuuona ukuu na utukufu wako
Asante Baba maana utatupa kushinda,utatuamsha salama na tutakutana tena kesho mahali hapa tukiwa tumeachilia mambo yote ya leo kesho iwe siku mpya na ya kukupendeza
Tunaomba yote katika jina la Yesu Mpatanishi na mwokozi wetu Amen Asante

MUNGU ANATUPENDA SANA,NAMI NAWAPENDA SANASANA MBARIKIWE USIKU MWEMA MAKAPUKU WOTE
 
na kwako pia mama
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…