Salaam Team,
Natumai mu-wazima.
Kuna jambo ambalo limenishangaza kidogo, ambalo ningeomba ku-share nanyi.
Kuna hii thread
Dada, uliza lolote la msingi kuhusu sisi wanaume, nitakujibu
Baada ya kuona kumekidhiri nyuzi za wadada/wanawake wengi wakiuliza maswali kuhusu sisi wanaume, maswali ambayo majibu waliyoyapata hayakujitosheleza
Hivyo, Mimi kama mwanaume, nikajitolea kuwapa fursa wanawake/wadada waniulize maswali nami ningewajibu nikiamini kwamba, majibu yangu yatawakilisha Wanaume.
Na kwenye majibu yangu nilijikita zaidi kufafanua tofaUti iliyopo kati ya sisi "Wanaume" na wavulana.
Kuna pahali nikakejeliwa, mmoja alikisema "hakufungua hata huo uzi, baada ya kuona kama una maudhui ya makapuku forums.
Nikajiuliza, kwani kuna shida gani lwenye nyuzi za makapuku forums?
Sijawahi ona tatizo nimeanza kufuatilia makapuku forum kwa muda mrefu sana.
Jambo la pili ambalo limenishangaza, ni kulaumiwa kuwa sijajibu maswali ya watu, kitu ambacho naamini kuwa sio kweli.
Kama patakua na mwenye muda, naomba ajaribu kupitia huo uzi na aniambie wapi ambapo sijajibu swali la msingi.
Ama kipi kibaya nilichoongea.
Naamini kuwa, humu watu ni wamoja, na kupitia huo umoja na ndio maana leo makapuku ipo hapa.
Natanguliza shukrani