Makapuku Forum

Makapuku Forum

Umeelewa lakini "kimombo" cha Kolomije hicho? Wewe ni mtani wangu wa wapi? Nilikuwa na bidii sana ya kujifunza lugha na tamaduni za watu kila nilikoenda shule (kasoro Kizaramo nilipokuja kusoma Dar) hivyo usishangae hata lugha yako nikawa naimanya kidogo. I wish ningekuwa najua Kisambaa kidogo nimwongeleshe "dadako" kwa Kisambaa...Nalimhola nkoyi!
Osie.... Ukunda uonge kishambaa? Ha ha ha ha ha.
 
Muziki na Urembo.

Ni jumatatu na ndiyo inaishiria, haijarishi unaimalizaje, tabasamu kwa sababu kesho ni siku nyingine tana Kapuku mwenzangu. Nilikumiss humu ndani.

Wikend yangu ilienda vizuri kiasi, Ijumaa na Jmosi zilikuwa sawa ila Jpili kuna jamaa ananidai, nilimkopa mavumba nikiahidi kumrudishia jtatu. Sasa tangu mornie hadi mawio simu hazikatiki, nikajiuliza, huyu si nilimwambia nitalipa jtatu, mbona anapapara wakati jtatu niliyomwambia sikumwambia ni ya tarehe ngapi. Yeye alidhani ni ya leo, kumbe huu mwaka una jtatu za kumwaga na hata 2018 kuna jumatau, hivyo awe mpole.

Kuna raha ya kudaiwa na pale unapomkwepa mdai wako kwa busara kama zangu basi unajipa nafasi nzuri ya kutokopeshwa wakati mwingine tena ukiwa na uhitaji. Ila huyu anayenidai ni ndugu yangu, usiniige mimi, utalost. Hongera kwetu tunaowapiga chenga wanaotudai. Yaani tuko kama ACACIA na makinikia.

Turudi kwenye muziki, madeni pembeni gitaa mkono wa kuume. Last wiki yaani wiki jana nilimpandisha Oliver Ngoma na wadau mlionekana kuvutiwa naye, asanteni. Baadaye nikaenda kujichimbia kidogo kuhusu huu muziki anaoucheza. Kifupi unaitwa Afro-Zouk.

Huu ulikuwa maarufu sana miaka ya 80 na 90s na ulienea zaidi toka katika visiwa vilivyokuwa chini ya Mfaransa na hata hapa Afrika muziki huu unachezwa zaidi katika nchi zinazoongea Kifaransa (Francophone) hususani Ivory Coast na majirani zake. Wao walitaka kuufanya kuwa na kasi fulani hivi ya ndombolo.

BTW, muziki na urembo na hapa tuelewane kabisa urembo sio kwa wanawake tu, hata wanaume tumeuboresha urembo tukauita utanashati na mimi kwa kuonekana smart ninavaa saa na kuchomeka ipasavyo huku ijumaa ni casuala na malapa sio ya kuogea lakini ni yale ya bei mbaya.

Tumwangalie Monique Seka, malkia wa Afro-zouk toka kwa kina Didier Drogba na alitamba na nyimbo kadhaa nzuri kama Misounwa, Baye na nyingine.

Binafsi naupenda sana Misounwa na ule alioimba na Meiway, utafute na unaweza kushara nasi bila kujali kama ulizaliwa miaka yangu ambapo shuleni tulikuwa tunahesabu namba na ukichelewa magoti yako yatakomaa kama ya mbuzi

Hadi wakati mwingine tena mdau wa nguvu unayetumia muda wako kuleta na kupokea maarifa humu Makapuku na zaidi sana, nakupenda sana

Asante sana Obe, ukweli nimekumbuka mbali sana hasa nikikumbuka jinsi Zouk isivyoisha fashion ni raha tupu, ubarikiwe

Sent from my itel it1406 using JamiiForums mobile app
 
Asanteee mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom