Makapuku Forum

Mkuu habari za kutwaa.

Vipi mashamba yanaendeleaje?

Huku dar wazimaaa. Ila hali ngumu tuu.

Mkuu wacha tu maisha yabane ili tupate akili ya kusurvive...unajua hela iliingia kwenye mzunguko kiholela hadi watu wakabweteka na kimsingi zilizokuwa zinaingia ni hizi za kifisadi sasa ile mirija imezibwa ndo maana tunaona kama maisha yammekuwa magumu...

Samahani kidogo kama nikukumbushe kitu, Baba wa Taifa Mwalimu J. K. Nyerere alikuja na Ideology yake ya Ujamaa ambayo tunajua haikufanikiwa kama alivyokusudia,ila si lengo langu kulizungumzia kwa sasa kwa kuwa kila zama ina kitabu chake alikuja Mzee Mwinyi na transformation yake ya Ujamaa kwenda ubepari kwa kuruhusu kila kitu....Hapa ndipo nadhani tulikosea kwa kuwa kama tungekubali kuumia kidogo wakati ule wa uhaba wa bidhaa tungefufua viwanda vyetu tungezalisha kwa kuwa malighafi tulikuwa nayo, na leo hii tungekuwa na surplus ambayo tungewauzia nchi nyingine na kujiingizia fedha za kigeni! Shida ni kipimo cha akili!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…