Makapuku Forum

1 Wakorintho 13

1.Nijaposema kwa lugha za wanadamu na malaika,kama sina upendo ,nimekuwa shaba ilayo na upatu uvumao.

2.Tena nijapokuwa na unabii,na kujua siri zote na maarifa yote,nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima,kama sina upendo,si kitu mimi.

3.Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini,tena nikijitoa mwili wangu niungue moto,kama sina upendo ,hainifaidii kitu.

4.Upendo huvumilia,hufadhili,upendo hauhusudu,upendo hautakabari,haujivuni.

5.Haukosi kuwa na adabu,hautafuti mambo yake,hauoni uchungu,hauhesabu mabaya.

6.Haufurahii udhalimu,bali hufurahia pamoja na kweli.

7.Upendo haupungui neno wakati wowote,bali ukiwepo unabii utabatilika,zikiwapo lugha ,zitakoma yakiwapo maarifa yatabatilika.

TUOMBE

Baba Asante kutuamsha salama,tunakushukuru kwa yote unayotutendea umekuwa mwema kwetu hakika wema wako na fadhili zako hazichunguziki.
Tunajikabidhi mikononi mwako Baba tulinde,tuongoze,tuponye,tufundishe Upendo Wa kweli ,kujaliana,kuthaminiana,kuchukuliana katika kila jambo ili dunia iwe mahali pazuri pa kuishi kwa kila mmoja wetu,tutenge na ubinafsi,chuki zisizo na sababu,tujenge katika misingi ya upendo kwa kila mmoja wetu,Upendo kwa jirani.
Baba asante kwakuwa utafanya sawa na mapenzi yako.

NEEMA YAKO YATOSHA

NAWATAKIA SIKU NJEMA MBARIKIWE
 
Asante mama mchungaji Mungu azidi kukubarikiii
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…