NUKUU YA LEO.
Everyone has their challenges.
Kila watu wana changamoto zao.
Haya maneno yaliwahi kutamkwa na Muigizaji wa kimarekani Wentworth Miller maarufu kama Prison Break.
Miller alizaliwa miaka 45 iliyopita nchini Uingireza. Miller alizaliwa June 2 1972.
Wentworth ana uraia wa marekani na wa uingereza. Baba yake alikuwa ni mtu mmarekani mweusi na mama yake ni mchanganyiko wa mrusi-mfaransa na mholanzi.
Wentworth ana degree ya fasihi ya Kiingereza kutoka chuo cha Princeton -marekani.
Wentworth miller amepata umaarufu mkubwa kupitia filamu za Prison Break na legends of tomorrow.Sasa hivi anaishi nchini Canada na wadogo zake wawili wa kike.
Mwaka 2007, Miller alikana kujihusisha na ndoa za jinsia moja lakini mwaka 2013 ndio alipojulikana kuwa wentworth ni shoga na muumini wa ndoa za jinsia moja.
Mwaka huo huo Russia ndio wakapiga vita ndoa za jinsia moja. Kitu ambacho wentworth miller aligomea mualiko Kongomano la Filamu nchini Russia.
Miller alikulia maisha ya upweke na kumfanya ajaribu kujiua mara nyingi zaidi.Sasa hivi miller ni balozi wa shirika la Active linalohusika na kuhamasisha vijana kujitambua na kufanya kitu wanachopenda wao.
Niishie hapo kwa leo.