Ninashangaa sana jinsi ambavyo CHADEMA inapoteza umakini wake. Swala la members wa CCM kuhamia CHADEMA linachukuliwa kirahisi sana lakini halipaswi kuchukuliwa hivyo. Taarifa zisizo rasmi ni kuwa kuna mamluki lukuki wametumwa kuibomoa CHADEMA, wengine wameshawapokea na kuwakubali kuwa wagombea wa ubunge na udiwani. Time will tell. Washinde wasishinde lengo lao ni moja tu "kuhakikisha CHADEMA sio tishio tena kwa CCM kwa gharama yeyote".
Ni lazima CHADEMA wakubali kuwa ili kuleta mabadiliko ya kweli ni lazima kuwaandaa wanachama wao muda mrefu ili kuongoza sio chama tu bali dola pia. Sio mtu anakurupushwa huko akiwa na ngeu, anahema na amekunjwa suruali, kisha anawatupia kadi ya CCM wakati hamkumpa nyie, na kumkabidhi kadi ya chama bila ya yeye kujua hata sera ya CHADEMA inasema je. Kisha kesho yake mnampa barua inayoonesha kuwa ndie mgombea wa CHADEMA. This is nonsense kwa chama makini na chenye nia ya kuleta mabadiliko ya kweli.
Sikatai kuhusu uzalendo wa baadhi ya waliohamia CHADEMA, na wala sitathubutu kuuhoji, ila ninahoji ukosefu wa subira. Mambo mazuri huivishwa kwa moto wa muda. Naogopa pale CHADEMA itakapogeuka ccmb, kama ambavyo TLP ya Mrema imegeuka.
Kwa ushauri wangu CHADEMA wawekeze zaidi kwenye wanachama vijana, wawape mafunzo ya Uzalendo, Uadilifu, Ubunifu na hali ya kuthubutu. Itachukua muda mrefu lakini itakuwa na matokeo ya kudumu na ya muda mrefu yenye kukijenga chama na Taifa kwa ujumla.
I love my country & i respect patriotism & intergrity.