Makapi ya CCM yanapokuwa ngano kwa CHADEMA

Nimekuwa nikisema more or less the same thing hapa, wanaotoka CCM sasa hivi waangaliwe mpaka at least 2015, kama wameonekana kwamba wamefuata kazi ya chama -na sio kutafuta ubunge kwa sababu wameshindwa kura za maoni CCM- ndipo wapewe nafasi hizi.

Vinginevyo CHADEMA itakuwa inaalika chaos.

Ningependa nikukumbushe kuwa Dr Slaa alionekana kuwa kapi ndaniya CCM lakini akageuka kuwa ngano kwa Chadema mpaka sasa anaweza kugombea urais. Kama Chadema wangemkataa kwa kigezo hicho, huenda pasingekuwa na Celebrated Slaa leo. Mimi naona waje tu, Chadema ni ya watz wote, nani ajuaye tunaweza kumpata Slaa mwingine.
 
Time alone, ooh time will tell.
You think you're in heaven while you're living in hell
You think you're in heaven while you're living in hell
Time alone, oooh time will tell

Kwa nini tunaandikia mate na wino upo, ngojeni uchaguzi uishe tutaweza kuongea vizuri zaidi, zaidi ya vilivyokwishasemwa sioni jipya . Mark my words, mamluki hawa watawa cost CHADEMA hata kama wakiingia bungeni.
 
Tafsiri ya makapi ni pana sana. Ukipembua mchele yale mapumba yanayotupwa ambayo huwa ni kiasi kidogo na kubaki mchele mwingi hii ni tafsiri moja. Pia ukichukua udongo na kupembua dhahabu ambayo ni kidogo na kutupa udongo ambao ni mwingi hapa makapi ni huu udongo.

Hawa watu wanaohama CCM ni dhahabu, hawakutumia rushwa ndio maana hawakupata kuteuliwa CCM. Ukitaka ubunge kupitia CCM ni lazima uwe tajiri (yaani uwe na hela nyingi za takrima). kama huna hutapata haijarishi wewe ni Malechela au Ntagazwa.
Dr. Slaa alitokea CCM ni kapi sasa, Wassira ameshahama mara kadhaa na Rais Mutharika wa Malawi alishahama chama chake ni kapi sasa. Wanaohama CCM wote si makapi kwani wengine wanahujumiwa na mafisadi na hata waaminifu waliobaki CCM bado wanaandamwa na mafisadi kwa kutumia fedha wazotuibia.
 
You think you're in heaven while you're living in hell

Think you're in heaven, but ya living in hell;

"ngojeni uchaguzi uishe" should mean you're holding off politicking on the subject altogether
 
Think you're in heaven, but ya living in hell;

"ngojeni uchaguzi uishe" should mean you're holding off politicking on the subject altogether

Yeyote anayekwambia ana hold off politicking anaogopa kutoa maoni yake tu, holding of politicking hata kina Hubble iliwashinda.

Data na uzoefu havidanganyi mwakwetu. Mimi nawaambia wangoje uchaguzi waone watakavyoadhirika na delusions zao, sio kwamba na hold off politicking.Kwa sababu tukibishana sana hapa kila mwamba ngoma atavutia kwake, tusubiri dakika 90 kujua kama kweli hao CHADEMA watapata majority bungeni na katika urais kama wanaodevela wanavyoota hapa.
 
Yeyote anayekwambia ana hold off politicking anaogopa kutoa maoni yake tu, holding of politicking hata kina Hubble iliwashinda.

Mimi nawaambia wangoje uchaguzi waone
wao wangoje uchaguzi wewe uendeleze politiking? "hata kina Hubble iliwashinda" Hubble aliahidi kivipi kwamba ata hold off politicking?

Mkubwa, ume bet for CCM kushinda, huo ni mteremko not worth your name taunting people for. Who u betting against? who will bet their handkerchief that incumbency won't return?
 
Yeyote anayekwambia ana hold off politicking anaogopa kutoa maoni yake tu, holding of politicking hata kina Hubble iliwashinda.

Data na uzoefu havidanganyi mwakwetu. Mimi nawaambia wangoje uchaguzi waone watakavyoadhirika na delusions zao, sio kwamba na hold off politicking.Kwa sababu tukibishana sana hapa kila mwamba ngoma atavutia kwake, tusubiri dakika 90 kujua kama kweli hao CHADEMA watapata majority bungeni na katika urais kama wanaodevela wanavyoota hapa.

Kweli kabisa Kiranga

Na kwa kwenda steps zaidi, mimi naona uchaguzi wa mwaka huu ufutwe ili kuokoa gharama za uchaguzi. Wewe unaonaje?
 
wao wangoje uchaguzi wewe uendeleze politiking? "hata kina Hubble iliwashinda" Hubble aliahidi kivipi kwamba ata hold off politicking?

Mkubwa, ume bet for CCM kushinda, huo ni mteremko not worth your name taunting people for. Who u betting against? who will bet their handkerchief that incumbency won't return?

I am betting against all hallucinators.
 
Wakowapi waliosema Shibuda ni nutrient na sio kapi la CCM ?
 
wanachama wengi wanaojitoa ccm hukimbilia cdm hii inatokana na chama cha cdm kutokuwa na makada wazuri, hata ukiangalia wagombea ubunge wengi uchaguzi uliopita walitoka ccm, na hii leo ndio inayopelekea chama hicho kuyumba kwa wengi wanaowapokea huwa hawana itikadi ya chama hicho mf. shibuda, safari, kahigi etc. na leo wameishaanza kuwatolea macho mapacha wa tatu wajiunge na cdm, wakumbuke nccr mageuzi nayo ilikuwa na mwenendo kama huu wa kuokota makapi ya ccm.
 
Hapo lazma CHADEMA wajitafakari wasikizane kujaza mashabiki lazma ichukue watu wenye strong commtment. u
 
CCM ikichukua wanachama wa CDM mnasema CCM yaibomoa CDM, wa CCM wakienda CDM wameokota makapi what is what, unamaanisha nini ndg yangu mleta thread? Kimsingi sijakuelewa hapa.
 
Chaguzi zinaendelea ndani ya Chama Cha Mapinduzi, wale waliotarajia majina yao ama fedha zao zitawabeba wamejikuta wakiangukia videvu, sasa wengine wanawaza kuhamia Chadema, si kwa sababu ya ukereketwa ni uroho wa madaraka(NINAYAKINI), Chadema jifunzeni kwa Mhe Shibuda...........!!!!!
 
nakubaliana nawe mkuu, watokao magamban hawana nia nzuri isipokuwa uroho wa madaraka wakipewa nafac hawa watakuja kukiua chama,tunahitaj kuijenga cdm kama taasis imara ambayo haitoweza kuyumbishwa so hata ikichukua miongo kadhaa kukamilisha hilo ni sawa sio kuchukua makapi yatakayokuja kukigharimu chama kama ilivyotokea kwa nccr mageuzi,tlp n.k
 
MOJA ya kosa kubwa watakalolirudia viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015, ni kukubali mtego wa kuwapokea na kuwapatia uongozi wafuasi wa CCM waliobwagwa kwenye uchaguzi wa ndani unaoendelea.

Nasema hilo ni kosa kubwa na natabiri mapema kuwa yatakayowafika watajuta akini wakati huo haitakuwa na faida tena kwao maana watakuwa wamepigwa mweleka tayari.

Ni kweli kila mtu ana haki ya kujiunga na chama chochote wakati wowote anaoona unafaa lakini kwa wanachama hawa wa CCM wanaongojea kwanza kukosa ushindi ndani ya chama chao ndipo watafute hifadhi CHADEMA, hawafai.

CHADEMA wanatambua ninachokisema kuwa kwenye uchaguzi mkuu wa 2010 katika maeneo mengi walifanya makosa makubwa kama hayo kwa kuwapokea wana-CCM waliojeruhiwa kwenye uchaguzi wa ndani kisha wao wakawapokea na kuwapa nafasi ya kugombea udiwani na ubunge na matokeo yake wameyaona.

Leo wako baadhi ya watu hao ndani ya CHADEMA wameshinda ubunge na udiwani lakini matendo yao ni ya kutaka kukiyumbisha chama kwani hawana cha kupoteza. Wanajua mkakati wao ukifanikiwa CHADEMA ikapasuka watapongezwa na CCM kwa kupewa vyeo hata serikalini.

Uchaguzi ndani ya CCM unaendelea na tayari vigogo wenye majina makubwa wameangukia pua, sasa wanahaha kurejesha heshima zao kwenye taswira ya kisiasa. Hawa eti wanataka kuhamia CHADEMA. Hivi kweli wana nia ya dhati?
Kwangu nasema hapana. Hawa si wanasiasa wenye mapenzi mema na Taifa wala CHADEMA,bali kiu yao ni madaraka. Hivyo iko siku hata ndani ya CHADEMA wakishindwa watakimbia tena.

Kwangu mimi mwanasiasa makini na mkomavu ni yule anayekubali kuwa wako watu wengine ndani ya chama chake wanafaa kuongoza kama yeye. Hivyo hata akishindwa kwenye uchaguzi hatakimbia ila atazidi kujipanga kwa uchaguzi mwingine.

CHADEMA kwa sasa ndilo tumaini pekee la Watanzania wapenda mageuzi.

Hiki ndicho chama pekee mbadala kimeweza kuikabili CCM na hivyo kinastahili kupewa dola lakini kamwe kisikubali kutegwa kupokea majeruhi wa CCM na kudanganyika kuwapa uongozi.

Anayeipenda CHADEMA na kutaka kuleta mageuzi hapaswi kungoja mpaka chama chake kimfukuze au ashindwe uchaguzi, isipokuwa anapaswa kuamua mapema kwa hiari yake na kjiunga na makamanda wapambanaji.

Hawa wanaotaka kukimbilia leo kwa sababu tu wamenyimwa uongozi CCM ni wabinafsi, wasio na uvumulivu, wepesi wa kuhadaika. Kama CHADEMA itainia mkenge wao ikawaona wa maana na kuwachukua basi tujipe muda mfupi nayo itakuwa imegawanyika mapande kama CCM.p
Kama wafuasi hawa wanahama CCM kwa vile makundi yao ya kusaka urais 2015 hayajashinda, ina maana hata ndani ya CHADEMA watakwenda kutengeneza makundi hayo hayo.

Chonde chonde tuachane nao na hata wakiingia tuwaone kama wanachama na kawaida.

Wako wana-CHADEMA wamepifia chama tangu kinaanzishwa hadi leo hawajapata madaraka makubwa, sasa kwanini wakimbilie kuwachukua walioshindikana CCM na kuwapachika madaraka pasipo kujihoji endapo wametumwa kukisambaratisha chama?

Kwa mwaka 2005 CHADEMA tunaweza kuwatetea kuwa walilazimika kuokoteza kila mtu hata wakawapokea wale waliotemwa CCM na kuwasimamisha wagombee lakini majibu waliyapata mapema kwani wako waliopewa fedha wakajitoa na kurejea CCM na wengine wakafanya kila aina ya hadaa na mwishowe CHADEMA ikala mweleka.

Tangu mwaka huo hadi leo, CHADEMA imefanya oparesheni za kila aina mijini na vijijini, imejiongezea mtaji wa wafuasi wenye sifa za kuwania nafasi zozote zitakazotakiwa, hivyo hawa ndiyo wanapaswa kupewa kipaumbele badala ya kukimbilia kupokea wale wenye sura mbili.

Kama itabidi kuwapokea wafuasi hao walioangushwa ndani ya CCM, dawa ya CHADEMA inapaswa kuwa laini kwamba wabakie wanachama wa kawaidi ila wakirogwa kuwapa vyeo wakafika juu na kuzisoma siri zao hakika kutakuwa na kilio cha kusaga meno.

Mifano iko mingi sana ya watu wa aina hii ambao mwaka 2005 walinyimwa uteuzi CCM wakakimbilia CHADEMA na kupewa nafasi kugombea ila waliposhindwa wakarejea tena CCM. Sasa hawa tunawaitaje kama si 'wasaka madaraka'?

Wanasiasa wetu wanapaswa kujifunza jambo moja kubwa kwamba nje ya madaraka kuna maisha. Hivyo kushinda ama kushindwa katika uchaguzi ni jambo la kawaida lisilowalazimu kuhama vyama kwa vile hawakuchaguliwa.

Orodha ya wana-CCM walihama kwenda upinzani ni ndefu sana tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, lakini watu hawa ebu tujiulize wengi wao wako wapi? Si hawa walipewa fedha na kuahidiwa madaraka ndani ya CCM na serikalini wakakimbia upinzani. Sasa hawa wanaotaka kuja CHADEMA baada ya kushindwa uchaguzi wanatofauti gani na hao wengine?

Tafakari!

Chanzo: Tanzania Daima
 
Shoo gap,
Nimeupenda sana mtazamo wako - Makapi ya sisiemu yanapokuwa ngano kwa chadema.

Ni kweli kabisa kwa mswahili, mswahili ngano ni ile ilikwisha kuwa processed na unga wake mweupe ndio bora na chakula, pasipo kufahamu kwamba ni Makapi ya ngano ndio yenye high in fible na nutrition zaidi ya huo unga mweupe.

Pili, ikiwa hawa wanaopokelewa ni makapi ya ngano, ni ubora gani wa hiyo ngano ilobakia CCM umeutazama kama sii kwa ubora wa kutengeneza chakula ulokizoea?...yaani Chapati na Mandazi!. ina maana unazungumzia kitu kilichokuwa bora kulingana na ufinyu wa ubunifu wa chakula bora kiasi kwamba unayaona makapi hayawezi kupika Chapati wala mandazi.

Well Chadema wanakuiletea mapishi ya kitu kinaitwa - Cereals.. Ni ngano yote inatumika hakitupwi kitu.
Wadhungu wanasema A brand natural of whole grain wheat with high fiber.... Ushindi ni Lazima

Katika tawala dhalimu za kifisadi watu wakweli, waaminifu na wazalendo ndio huitwa makapi. Mwanzo wa ufalme wa mtawala mathubuti Daudi mfalme wa Israel watu waliokimbia utawala wa Sauli (makapi) walitajwa kuwa wenye madeni, wasiokubalika na hohe hahe 1 Samweli 22:1-2. Lakini walipoungana na Daudi ambaye naye alikuwa mtuhumiwa wa ukorofi na mtawala dhalimu wa wakati wake Sauli tunaona hatimaye ndio walikuwa mashujaa wakuu wa nyakati hizo. Walimpatia Daudi kupanuka kwa himaya yake na akawa mtu mkuu sana. 2 Samwel 23:8
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom