Nimekuwa nikisema more or less the same thing hapa, wanaotoka CCM sasa hivi waangaliwe mpaka at least 2015, kama wameonekana kwamba wamefuata kazi ya chama -na sio kutafuta ubunge kwa sababu wameshindwa kura za maoni CCM - ndipo wapewe nafasi hizi.
Vinginevyo CHADEMA itakuwa inaalika chaos.
Hii ni kweli. Kwa sasa muamko wa vijana na watu wengi kutafuta ubunge au udiwani si kwa nia ya kulikomboa taifa bali ni kwa nia ya kutafuta ajira yenye umaarufu na hela za haraka. Hivyo wanapokosa CCM hukimbilia chadema kwa kuwa wanasema ccm imewaonea kumbe sivyo hawa wanatafuta ajira kwa sababu wengi ni wataalam wa kupiga domo na siyo kufanya kazi. Katika hali ya sasa ya kushindana soko la ajira vijana wengi wavivu na wasiokuwa na CV nzuri hukuimbilia siasa kwani huko hata la saba anaweza kupata uwaziri.
Na ieleweke kuwa vijana wadogo ambao hawajafanya hata kazi au miradi fulani kukimbilia siasa ni janga la taifa. Si kwamba wana akili sana bali ni wazuri kuongea hadharani tu kama kina zito na wenzake ambao hupewa taarifa na watu au makampuni kuja kuongea bungeni kwa nguvu ambazo at the end hatuoni matunda yake.