Makapi ya CCM yanapokuwa ngano kwa CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makapi ya CCM yanapokuwa ngano kwa CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shoo Gap, Aug 19, 2010.

 1. Shoo Gap

  Shoo Gap JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 236
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ninashangaa sana jinsi ambavyo CHADEMA inapoteza umakini wake. Swala la members wa CCM kuhamia CHADEMA linachukuliwa kirahisi sana lakini halipaswi kuchukuliwa hivyo. Taarifa zisizo rasmi ni kuwa kuna mamluki lukuki wametumwa kuibomoa CHADEMA, wengine wameshawapokea na kuwakubali kuwa wagombea wa ubunge na udiwani. Time will tell. Washinde wasishinde lengo lao ni moja tu "kuhakikisha CHADEMA sio tishio tena kwa CCM kwa gharama yeyote".

  Ni lazima CHADEMA wakubali kuwa ili kuleta mabadiliko ya kweli ni lazima kuwaandaa wanachama wao muda mrefu ili kuongoza sio chama tu bali dola pia. Sio mtu anakurupushwa huko akiwa na ngeu, anahema na amekunjwa suruali, kisha anawatupia kadi ya CCM wakati hamkumpa nyie, na kumkabidhi kadi ya chama bila ya yeye kujua hata sera ya CHADEMA inasema je. Kisha kesho yake mnampa barua inayoonesha kuwa ndie mgombea wa CHADEMA. This is nonsense kwa chama makini na chenye nia ya kuleta mabadiliko ya kweli.

  Sikatai kuhusu uzalendo wa baadhi ya waliohamia CHADEMA, na wala sitathubutu kuuhoji, ila ninahoji ukosefu wa subira. Mambo mazuri huivishwa kwa moto wa muda. Naogopa pale CHADEMA itakapogeuka ccmb, kama ambavyo TLP ya Mrema imegeuka.

  Kwa ushauri wangu CHADEMA wawekeze zaidi kwenye wanachama vijana, wawape mafunzo ya Uzalendo, Uadilifu, Ubunifu na hali ya kuthubutu. Itachukua muda mrefu lakini itakuwa na matokeo ya kudumu na ya muda mrefu yenye kukijenga chama na Taifa kwa ujumla.

  I love my country & i respect patriotism & intergrity.
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,193
  Trophy Points: 280
  Nimekuwa nikisema more or less the same thing hapa, wanaotoka CCM sasa hivi waangaliwe mpaka at least 2015, kama wameonekana kwamba wamefuata kazi ya chama -na sio kutafuta ubunge kwa sababu wameshindwa kura za maoni CCM - ndipo wapewe nafasi hizi.

  Vinginevyo CHADEMA itakuwa inaalika chaos.
   
 3. B

  Big Dady Member

  #3
  Aug 19, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaap! inawzekana kweli Chadema hawajawa makini katika kuamua nani wamchuke kutokana na harakati zilizopo sasa za uchaguzi. Lakini sikubaliani na kuwaita binadamu wenzenu, MAKAPI. Yamkini ninyi ndio makapi zaidi.

  Suala la wanachama wa chama kimoja kuhamia kingine halijaanza leo, kwa hiyo tuseme akina Lamwai, Guninita, Tambwe Hiza, na wengine waliohamia CCM nao ni makapi?

  Kuweni waungwana katika kujenga hoja. Ndio maana narejea kwamba yamkinini nyie ndio MAKAPI zaidi.
   
 4. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,193
  Trophy Points: 280
  Big Dady

  Mazee unafahamu matumizi ya lugha katika tamthiliya? Unafahamu "similes and metaphors" ?

  Ukifahamu vitu hivyo utafahamu kwamba makapi ni vitu visivyotakiwa baada ya kuchagua nafaka, na kama mtu anawaita watu kama kina Shibuda walioshindwa chaguzi za primaries za CCM "Makapi ya CCM" artakuwa sawa kabisa, maana CCM wamewapigia kura ya "no confidence". Sioni kwa nini wasiitwe makapi.

  Na kuhusu kupewa nafasi za kuwakilisha chama, hatukatai wapewe, lakini inabidi wakae kwenye chama kwa muda fulani ili wakijue chama na chama kiwajue wao kwa ukaribu zaidi, na watu waondoe shaka za kwamba hawa watu wameingia katika CHADEMA kwa sababu tu wamekosa jinsi nyingine ya kutafuta ubunge. Tunataka mtu akijiunga na chama ajiunge kwa ajili ya kufuata sera, sio kwa sababu tu anataka kukitumia chama kupata ubunge bila kujali sera wala falsafa. Sasa ili kuhakikisha vitu fulani fulani, muda unahitajika, mtu hawezi kujiunga na chama leo, kesho akawa mgombea ubunge, yatakuwa mauzauza hayo.

  CHADEMA ikitaka kula kila kitu itakula mpaka sumu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. fige

  fige JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2010
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watu kuhama vyama ili wapate ridhaa ya kugombea bila kujali itikadi ya vyama ni ishara nyingine kuwa kuna haja ya kuwa wagombea binafsi .
   
 6. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mbona Mwera wa Tarime kaenda CUF na wamempa ugombea ubunge? Au ni kwa CCM tu kwenda Chadema? Any way by the way chadema hamna kitu hiyo ni nguvu tu ya soda.

  Nasikitika sana kwa muda wa miaka mitano ijayo slaa hatakuwepo kwenye siasa kama ilivyokuwa kwa mbowe miaka mitano inayoisha. Inauma.
   
 7. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #7
  Aug 19, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  ndio maana wachambuzi wa siasa wanasema Dr Slaa anafaa lakini ataundaje dola kwa watu wa kuazimaazima bila ya kuwajenga wafuasi wao muda marefu?

  Kila siku CHADEMA wanasema CCM ni mafisadi lakini ajabu wanapokea wagombea CCM bila hata kuwajua kwa undani.Bado naamini CHADEMA ni chama kizuri lakini hakijakomaa kukipa nchi.

  Kama leo Dr Slaa atashinda kuwa Rais hana watu wa kuunda serikali kwani kama CHADEMA wanathubutu kuokoteza wagombea wa nafasi mbalimbali bila mpangilio bila shaka wataokoteza watu wa kuunda serikali yao. Tuwape muda wa kujijenga zaidi.
   
 8. T

  Tata JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2010
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,735
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Haya ni madhara ya kutokuwa na utaratibu wa wagombea binafsi. Kwa utaratibu wa sasa watu wanalazimishwa kugombea kupitia kwenye magenge-maslahi ya wateule wachache wanaojiita vyama vya siasa. Wakikosa kwenye genge moja wanahamia kwenye jingine kwani ndio njia pekee ya kuweza kupata haki ya kuchakuliwa nchi hii.

  Suala la itikadi ya chama, imani ya mwanachama, sera chama na mwelekeo wake kwa ujumla katika mfumo wetu si mambo ya msingi (primary) bali ni mambo yanayoangaliwa baadaye (secondary). Mfumo huu umegeuza uchaguzi kuwa soko holela (siyo huria) la kura za wananchi maskini na wasio na ufahamu ambao kwao huu ni msimu wa mavuno ya vijipesa vya wagombea wa ubunge na udiwani. Kwani baada ya hapo hawatawaona tena mpaka baada ya miaka mitano.

  Sishangai watu hawa wa CCM kuhamia Chadema kwa sasa kwa sababu upepo unaonyesha kina dalili za kukubalika kwa sasa. Na kwa sababu hawa wahamaji wa sasa ni watu wanaolenga maslahi zaidi "opportunists" siyo ajabu wao kufanya maamuzi hayo. Nilimsikiliza Ndugu John Shibuda alipokuwa akieleza sababu za kuhama CCM. Kimsingi yeye bado ni mwana CCM kwa sababu hana matatizo na sera na mwelekeo wa CCM.

  Tatizo lake ni rushwa na rafu nyingine zilizotumika wakati wa kura za maoni ambazo zilikuwa ni zaidi ya zile alizotumia yeye. Pia hakuwa na imani na mfumo wa rufaa wa CCM ambao hautoi mwanya kwa walalamikaji kusikilizwa. Tutaona huyu muumini wa CCM atakitumikia vipi chama cha CHADEMA ambacho kinajinadi kuwa na sera tofauti na CCM.

  Sitashangaa pia kusikia hawa jamaa ama wamerudi CCM kabla ya uchaguzi wa 2015 ama wamehamia chama kingine ambacho upepo unaelekea kukipa uwezekano wa kukubalika na wananchi (Mpendazoe case).
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  Aug 19, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Shoo gap,
  Nimeupenda sana mtazamo wako - Makapi ya sisiemu yanapokuwa ngano kwa chadema.

  Ni kweli kabisa kwa mswahili, mswahili ngano ni ile ilikwisha kuwa processed na unga wake mweupe ndio bora na chakula, pasipo kufahamu kwamba ni Makapi ya ngano ndio yenye high in fible na nutrition zaidi ya huo unga mweupe.

  Pili, ikiwa hawa wanaopokelewa ni makapi ya ngano, ni ubora gani wa hiyo ngano ilobakia CCM umeutazama kama sii kwa ubora wa kutengeneza chakula ulokizoea?...yaani Chapati na Mandazi!. ina maana unazungumzia kitu kilichokuwa bora kulingana na ufinyu wa ubunifu wa chakula bora kiasi kwamba unayaona makapi hayawezi kupika Chapati wala mandazi.

  Well Chadema wanakuiletea mapishi ya kitu kinaitwa - Cereals.. Ni ngano yote inatumika hakitupwi kitu.
  Wadhungu wanasema A brand natural of whole grain wheat with high fiber.... Ushindi ni Lazima
   
 10. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #10
  Aug 19, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Hata mimi nina mashaka kama nyota ya Dr Slaa itaendlea kung'ala kwani MBOWE ni mjanja anajua kabisa kwamba Dr Slaa hawezi kumshinda Kikwete lakini kampeleka kummaliza kisiasa baada ya kuona DR. anamfunika mwenyekiti wake kwa umaarufu. NI wakati mbaya kuliko wote kumtoa Dr Slaa kugombea Urais.

  Wananchi makini hawawezi kumpa kura Dr Slaa kwa hofu ya jinsi atakavyounda serikali endapo CHADEMA hakitakuwa na wabunge wa kutosha kuweza kupitisha mishwada/sheria kwa mujibu wa chama chake. Rais asiye na bunge sio Rais mwenye mamlaka hatakuwa tofauti na KIBONZO. Ndio maana mara kadhaa CHADEMA wameshauriwa kuongeza wabunge badala ya kukimbilia Urais ambao kwa sasa sio size yao. haya ndio makasa aliyofanya Mrema, Mbowe na Lipumba na sasa ni zamu ya Dr Slaa kujimaliza.

  Kama chama kinashindwa kuongeza wabunge yamkini wapiga kura makini hawawezi kukipa chama hicho URais.Kwanza Chama kikubalike katika ngazi ya uwakilishi wa wananchi ndipo kipewe Ikulu na hivyo kuunda serikali imara. Serikali legelege inaundwa na chama legelege kinachokosa uwakilishi mpana wa wabunge bungeni.
   
 11. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #11
  Aug 19, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,193
  Trophy Points: 280
  Bob,

  Kuna makapi ya kusema tunaweza kupata nutrition kama za dona, halafu kuna chuya za kupalia watu na kuwaua.

  Ndiyo maana nikasema CHADEMA - na kwa kweli chama chochote kile- kinahitaji muda kupembua nafaka wapi, makapi yanayoweza kufaa kwa kutoa virutubisho wapi, na chuya zinazoweza kuwapalia watu wapi.

  Kazi ya kuchambua haitaki papara na kuharakisha, ama sivyo CHADEMA "wataula wa chuya".
   
 12. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #12
  Aug 19, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Ndio kujimaliza kisiasa kwenyewe makapi ya chama kingine bila kuyapembua yanakuwa chakula halisi kwa chama kingine. mantiki hapa sio tu mtu kutoka CCM kwenda chama kingine bali kuingia katika chama chochote cha siasa na hasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi na kisha kupewa uongozi moja kwa moja. Hawa wote watarudi walikotoka endapo watakosa walichofuata wakati huu wa kuelekea uchaguzi.

  Hapa tunaona kwamba vyama vya upinzani bado havijakomaa. sio vibaya kupokea wanachama kutoka vyama pinzani lakini ni lazima kuwapika upya kulingana na matakwa ya chama husika ndio hapo suala la muda linapoingia ili kuwatambua kwa ubora wanachama waliojilipua wenyewe kwenda vyama vingine wameiva au la.


   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Aug 19, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Bahati mbaya huwezi kupata dona kutoka ktk ngano! Ktk ngano hakitupwi kitu hata zile pumba za majani yake hupewa farasi wakala.
   
 14. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #14
  Aug 19, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  hivi huwa wanachukua makapi kwa sababu chama hakina uwezo wa kuzalisha ngano yake wenyewe?

  sijaona bado mantiki ya kuchukua makapi kisha ukayapa thamani ya zaidi ya ngano yenyewe hata kama yanafaida.
   
 15. J

  Jafar JF-Expert Member

  #15
  Aug 19, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tafsiri ya makapi ni pana sana. Ukipembua mchele yale mapumba yanayotupwa ambayo huwa ni kiasi kidogo na kubaki mchele mwingi hii ni tafsiri moja. Pia ukichukua udongo na kupembua dhahabu ambayo ni kidogo na kutupa udongo ambao ni mwingi hapa makapi ni huu udongo.

  Hawa watu wanaohama CCM ni dhahabu, hawakutumia rushwa ndio maana hawakupata kuteuliwa CCM. Ukitaka ubunge kupitia CCM ni lazima uwe tajiri (yaani uwe na hela nyingi za takrima). kama huna hutapata haijarishi wewe ni Malechela au Ntagazwa.
   
 16. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #16
  Aug 19, 2010
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,724
  Likes Received: 1,213
  Trophy Points: 280
  Ha ha haa! Chadema imebana korodani za watu humu.

  Hakukaliki, hakulaliki.
   
 17. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #17
  Aug 19, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mtetezi wa mafisadi ya CCM Kiranga naona naye hakuchelewa hapa. Akiona anything anti-chadema anakimbia kama hana akili nzuri.
   
 18. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #18
  Aug 19, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Huwezi kuiona kwa vile wewe ni mtetezi wa chama cha makapi oooppss mafisadi
   
 19. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #19
  Aug 19, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 2,004
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  ....au Selelii
   
 20. M

  Mkandara Verified User

  #20
  Aug 19, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu kiswahili safi makapi ni mabaki ambayo kwao wote hayana faida lakini inategemea na mtu unayataka makapi hayo ili kutengeneza kitu gani..hapa tunazungumzia CCM na ngano yao na hakika aMakapi ya ngano ndiyo yenye fible zaidi ya hjuo unga mweupe (kina Rostam).. makapi ya ngano are brown na hakika yana nutrition kwetu ktk mapishi mapya kuliko hizo chapati na mandazi za CCM.

  Nitarudia kumkumbusha huyu Kiranga kwamba mbinu zote za wao CCM haziwezi kuondoa ukweli kwamba ni baada ya wao kuyatupa hayo makapi sasa wanataka kuyadai kwa mbinu za kusingizia ni makapi hali roho zinawauma sana. Mbona Chadema haijawahi kusema kina Kabourou ni Makapi.. hakuwa na faida na Chadema lakini alionekana kuwa na faida na CCM..Na mbona Dr.Slaa mwenyewe ni makapi ya ngano vile vile leo amekuwa mwiba kwenu...
   
Loading...