Makapi ya CCM yanapokuwa ngano kwa CHADEMA

Huwezi kujua hili kwa hakika bila kuwapa muda wa kutosha kujionyesha true nature yao ndani ya upinzani. Inawezekana wamekuwa mzigo hata CCM ndiyo maana wakatoswa.

Ndiyo maana wengine tunapendekeza wapewe muda mpaka 2015 waangaliwe.

Hiki ndicho Kiranga anataka...... CCM iendelee kutawala mpaka 2015. Atafanya kila anachoweza hapa kumbakiza KIkwete madarakani (huku akisingizia kuwa anajaribu kusaidia upinzani).
 
Nimekuwa nikisema more or less the same thing hapa, wanaotoka CCM sasa hivi waangaliwe mpaka at least 2015, kama wameonekana kwamba wamefuata kazi ya chama -na sio kutafuta ubunge kwa sababu wameshindwa kura za maoni CCM- ndipo wapewe nafasi hizi.

Vinginevyo CHADEMA itakuwa inaalika chaos.

Nimegundua na nina ushahidi wa wazi kabisa kuwa hoja nyingi za Kiranga ama zimejikita kwenye ushabiki wa CCM au hazina hata chembe ya maslahi kwa wana mageuzi!

Kama kuchunguzwa watu wanao hama vyama ungeanza na kuwaambia kwanza CCM maana wao ndiyo walioanza kuchukua watu toka kwenye vyama vya upinzani na wengine hadi ikawapa hadi mamlaka ya kuongoza dola!

Tukianzia toka kwa Mbunge wa zamani wa chadema Aman Kaburu,Mbunge wa zamani wa CUF Msabaha,Mwenyekiti wa sasa wa Mkoa wa Dar Mzee Guninita na wengineo wengi waliopewa madaraka ya kidola hawa walikuwa upinzani;Je CCM iliwachunguza lini kabla hawajapewa vyeo?

Kiranga,anza kuishauri kwanza CCM ambayo ina dola kuliko kuja sasa kuiona CHADEMA kama haifai wakifanya vitu hivyo hivyo usivyovikemea CCM ikifanya!
 
Kama ungekuwa unasoma posts zangu bila bias, ungegundua kwamba mimi ninaongelea universal first principles, ninaongelea rules kwa vyama vyote vya kisiasa na nimesema hivyo several times, it just so happens kwamba CHADEMA ndicho chama mbadala ndiyo maana tunakizungumzia sana, na kuichambua system iliyo irredeemably corrupt -as some would say- kama ya CCM ni beating a dead horse.

Kwa hiyo, ukinipa hii cowboy mentality ya "if you can't say nice things about us you are with the enemy" unanionyesha tu jinsi ulivyo simpleton. Mbona sijaona wafuasi wa CCM kunishutumu kwamba mimi ni goon wa CHADEMA ninapowashambulia?

Au mnataka niamini kwamba CHADEMA ni watu wa kulialia na hawawezi ku stand criticism ?
 
Sikubaliani nazo kabisaaaaaaaaaaa.... lakini ukitaka kuremba kama unavyosema wewe hutafika popote. Huo ustaarabu unaotaka Afrika bado haijaufikia. Inabidi na Chadema nao wacheze kata funua.... ni hali halisi....

Una confuse mambo mawili tofauti kabisa.
 
Utawaangaliaje wakiwa nje acha waingie wapewe kazi zitakazoifanya Chadema ione ubora wao.

Sawa, na mimi sitaki kuwangalia wakiwa nje, nataka kuwaangalia wakiwa ndani. Kazi zitakazoifanya CHADEMA ione ubora wao si lazima ziwe za ubunge, wapeni ukada wa chama wilayani waongeze wanachama, kujenga network, kukubalika kwa wanachama, kujifunza falsafa ya CHADEMA wilayani, in five years kama wameweza kupita hii process bila matatizo mnawapa uwakilishi.

Sio mnataka kuwapa uwakilishi hata test hamjawapa, mtaonekana desperate, na wananchi hawapendi vyama desperate trust me on that.
 
Sikubaliani nazo kabisaaaaaaaaaaa.... lakini ukitaka kuremba kama unavyosema wewe hutafika popote. Huo ustaarabu unaotaka Afrika bado haijaufikia. Inabidi na Chadema nao wacheze kata funua.... ni hali halisi....
Umenena kiongozi.....hii ndiyo njia ya kututoa hapa kwenda kule!
Ghana ndivyo walivyoweza kutoka...kupitia strongman Rawlings. Nina uhakika Rwanda wanaelekea huko pia. Kuna casualties watu watasema, yes.... hiyo ni inevitable kwenye ukombozi uwao wote.
Katika vitabu vitakatifu imeandikwa kulikuwa na mitume walioteswa na kufa kwa ajili ya kuwakomboa wengine kuepukana na hasira ya Mungu dhidi ya uovu wao.
Hata baba wa taifa katika kuitengeneza TZ kuwa taifa lenye umoja kulikuwa na casualties. Ona leo yuko wapi? Yuko lined up kuwa St Nyerere!
Kuna baadhi ya watu humu jamvini wanataka kutuaminisha bookish and theoretical approach zao ambazo it'll take ages to translate them into practice. Zinanikumbusha zile hotuba (sic) ndefu za JK...ngonjera tupu. Matokeo yake? Do I need to say more?
 
Kwa hiyo, ukinipa hii cowboy mentality ya "if you can't say nice things about us you are with the enemy" unanionyesha tu jinsi ulivyo simpleton. Mbona sijaona wafuasi wa CCM kunishutumu kwamba mimi ni goon wa CHADEMA ninapowashambulia?

Au mnataka niamini kwamba CHADEMA ni watu wa kulialia na hawawezi ku stand criticism ?

Bado hujasema kuwa, kwa vile wapinzani hawako tayari (unadai kuwa labda watakua tayari mwaka 2015) kuongoza nchi mwaka huu (kwa hiyo wasipewe kura) nani apewe uraisi wa Tanzania mwaka huu?
 
Bado hujasema kuwa, kwa vile wapinzani hawako tayari (unadai kuwa labda watakua tayari mwaka 2015) kuongoza nchi mwaka huu (kwa hiyo wasipewe kura) nani apewe uraisi wa Tanzania mwaka huu?

Unaweza kunionyesha hapo niliposema wapinzani wasipewe kura ? Mimi naweza kukuonyesha wapi nimesema wapinzani wapewe kura, post moja kati ya nyingi nilivyosema hivi ni hii hapa , naomba wewe unionyeshe wapi niliposema wapinzani wasipewe kura.

Wewe unataka niseme mara ngapi na kwenye threads ngapi ndiyo uridhike?
 
makapi maana nini kwani kuna watu ambao ni safi wana uzalendo ambao hawakuhonga wapiga kura bado wanahitajika kwa wananchi na taifa kwa ujumla hivyo haya si makapi mfano thomas nyimbo ameshinda na akaondolewa kwa mizengwe je hili ni kapi?
 
Umesema hapa (emphasis is mine):

Kiranga said:
Mazee ningependa watu wengi zaidi wa vote CHADEMA, only because naamini tunahitaji mabadiliko.

Lakini at the same time siamini kwamba CHADEMA watashinda urais au kuwa na majority ya viti vya bunge. Nisingependa kuona CHADEMA wanashuka chini kutoka asilimia za kura za urais walizopata 2005 (11%) wala kupunguza viti vya bunge.

Lakini for sure CHADEMA nao bado hawako ready for prime time, ndiyo maana naona ni bora kuwe na gradual change, wapate tough love hapa, kama wana moyo wa kujifunza waweze kujifunza, labda 2015 au 2020 wataweza kuchukua nchi with confidence.
 
Right,

Na kwa kuwa mwamba ngoma huvutia kwake, na kila mtu atakwambia yeye ni safi na kakataliwa kwa sababu hajaonga wananchi, ndiyo maana tunasema wapewe miaka mitano kufanya kazi za kuhamasisha shughuli za chama wilayani, tuwaone kweli kama ni safi kama wanavyosema au ni longolongo tu. Huwezi kuwajua hawa watu bila kuwapa muda, wengine ni wajanja sana kuficha makucha.

Kama wanapenda CHADEMA kwa nini hawakutoka CCM kabla ya kukataliwa katika kura za maoni ? Inaonekana wengi wao ni opportunist tu wanataka ubunge zaidi ya kukubali sera za CHADEMA. Miaka mitano ya kazi za chama wilayani itakuwa muafaka kujua nani anahitajika na nani mnafiki.
 
Umesema hapa (emphasis is mine):

Sasa wapi nimesema wasipewe kura hapo?

Uliona nilivyosema hivi hapa chini, note the emphasis, yaani nimesema clearly kabisa nataka kura ziende wapi lakini nikawa pragmatic kwamba CHADEMA hawawezi kushinda, unaweza kuwa na nerve ya kusema nimesema watu wasipigie kura CHADEMA ?

Kama si uongo ni nini sasa ?

Mazee ningependa watu wengi zaidi wa vote CHADEMA, only because naamini tunahitaji mabadiliko.

Lakini at the same time siamini kwamba CHADEMA watashinda urais au kuwa na majority ya viti vya bunge. Nisingependa kuona CHADEMA wanashuka chini kutoka asilimia za kura za urais walizopata 2005 (11%) wala kupunguza viti vya bunge.

Lakini for sure CHADEMA nao bado hawako ready for prime time, ndiyo maana naona ni bora kuwe na gradual change, wapate tough love hapa, kama wana moyo wa kujifunza waweze kujifunza, labda 2015 au 2020 wataweza kuchukua nchi with confidence.
 
Kama ungekuwa unasoma posts zangu bila bias, ungegundua kwamba mimi ninaongelea universal first principles, ninaongelea rules kwa vyama vyote vya kisiasa na nimesema hivyo several times, it just so happens kwamba CHADEMA ndicho chama mbadala ndiyo maana tunakizungumzia sana, na kuichambua system iliyo irredeemably corrupt -as some would say- kama ya CCM ni beating a dead horse.

Kwa hiyo, ukinipa hii cowboy mentality ya "if you can't say nice things about us you are with the enemy" unanionyesha tu jinsi ulivyo simpleton. Mbona sijaona wafuasi wa CCM kunishutumu kwamba mimi ni goon wa CHADEMA ninapowashambulia?

Au mnataka niamini kwamba CHADEMA ni watu wa kulialia na hawawezi ku stand criticism ?

Hoja zako toka ile ya "Dada Regina na Ubunge wa Kilombero" na hii ya "Uchakachuaji wa Wagombea wa CHADEMA wanahohamia toka CCM" zote sio tu ni legelege mno bali pia ni "baseless and meaningless"kwa sababu haujaonyesha hata point moja hai ku-back up your claims

Kimsingi hoja zako nimezitupilia mbali!
 
Kiranga,
Mkuu wangu mbona hivyoooo!
Hata kipofu asiyeweza kusoma akasikia tu mazungumzo yako atajua ni mshabiki wa Yanga oooh samahani TTC chang'ombe..kama alivyo Mwafrika na Chadema. Kinachonishinda mimi kuelewa ni kwamba mbunge ni mwakilishi wa wananchi iweje wewe usipende uwakilishi wao ikiwa hawa waliotupwa na CCM ndio wenye mvuto mkubwa kwa wananchi wa jimbo husika..

Na kwa nini usiwapime na wananchi wa jimbo hilo na kusema kwamba Chadema wamelamba dume au laa na kwa sababu kadhaa wa kadhaa mtu huyo hawezi kushinda jimbo hilo.. Hii utakuwa unawasaidia zaidi kimawazo kuliko kupinga tuuu ili mradi ni Chadema.

Kumbuka kura za maoni ndani ya chama zimefuatiwa wanachama wa CCM ambao hawafiki hata asilimia 10 ya wapiga kura. Inawezekana CCM wamefanya makosa na pengine makosa makubwa kuwaengua hata wale wanachama wao walifikiria wana nafasi nzuri ya ushindi, na Chadema wameliona kosa hilo wakalifanyia kazi mapema..

Mkuu wangu uchaguzi ndani ya CCM hasa ktk hiyo kamati yao inashangaza sana kumwona mtu kama Lowassa ndio ake meza kubwa kupitisha majina ya wagombea.. hivi kweli wewe na akili yako unadhania hapakuwepo na hila za kuwaangusha baadhi ya wapiganaji!.

Kwa hiyo kama CCM ilifikia kumwamini Lowassa kama walivyofanya baada ya JK kushika nchi akachagua mawaziri woote bomu ndio kilichotokea tena mwaka huu na Chadema hawakupoteza muda kutumia nafasi hiyo kujazia.

Hivyo tusubiri matokeo na hakika nawaona ni CCM wakihaha kila siku na maneno mazito kuhusiana na haya makapi.. sasa kama kweli hawa watu ni makapi lini mtu akazungumzia pumba au makapi hali yeye ana ngano bora kama sii ndio hadithi ya Sungura na zabibu?
 
Hata Bwana Yesu alipokuwa anatafuta wafuasi asingeweza pata isipokuwa wale waliokuwa wamekandamizwa na shetani. Na vyama vya upinzani member wake wote ni kutoka ccm. Walikua wanachama wa CCM ama kwa hiari au kwa kushurutishwa. Na kama hawa mafisadi wa CCM na corrupt mind wake wanahesabiwa kuwa ngano basi lugha kwetu haina maana. Hii ngano ya CCM mfano wa kina Rostam, Lowassa, Karamaji, Chenge na wote wanaofanana nao ambao ndio majority ndani ya ccm haya ndio haswa makapi ya taifa letu.

Huwezi kamwe kuwafananisha na ngano halisi kama kina Selelii, Shibuda, mpendazoe na wengine wengi wa jinsi yao waliokimbia kuwa chini ya mgandamo wa kifisadi ndani ya CCM. Ninapotafakari eti Chenge yule aliyeficha pesa za masikini wa tz ughaibuni, yule aliyewagonga wanawake na kuwaua saa tisa usiku huku akiendesha gari ambayo haina insurance wala yeye hana leseni, ndie mwenyekiti wa maadili ndani ya CCM, jibu linanijia kuwa maadili ndani ya CCM yana tafsiri ya uharamia dhidi ya ubinadamu.
 
Hoja zako toka ile ya "Dada Regina na Ubunge wa Kilombero" na hii ya "Uchakachuaji wa Wagombea wa CHADEMA wanahohamia toka CCM" zote sio tu ni legelege mno bali pia ni "baseless and meaningless"kwa sababu haujaonyesha hata point moja hai ku-back up your claims

Kimsingi hoja zako nimezitupilia mbali!
Malafyale....usije kufa kwa pressure bure ku-argue na huyu ndugu. Sidhani kama hata yeye mwenyewe anakijua kwa dhati anachokipigania na kukisema.
 
Kiama cha Kikwete kimefika, Nani amesema Chadema hakitapata wabunge wengi? ni mwendawazimu tu ndiye anaweza kuamini hivyo. Kuna watu wengi wako na wengine walikuwa ccm si kwa sababu wanaamini kilichopo huko, bali ni kutokana na woga wa kufuatiliwa, sasa wamegundua Chadema kina nguvu kubwa na wameamua kujiunga huku na ninasema bado mapema Chadema inachukua nchi, hili litakuuma sana wewe fisadi kwani unaishi kwa kudhulumu wengine.

SASA BASI KUONEWA HUKU AMBAKO KIKWETE KUMEMSHINDA KUONDOA SLAA NI CHAGUO SAHIHI, SEMA NDIO KWA DR. SLAA SISI WAFANYAKAZI TUMEANZA JE WEWE
 
Malafyale....usije kufa kwa pressure bure ku-argue na huyu ndugu. Sidhani kama hata yeye mwenyewe anakijua kwa dhati anachokipigania na kukisema.

Tatizo lenu mnataka a simplistic approach, CCM mafisadi, kwa hiyo yeyote anayetaka kuitoa CCM rafiki yetu, yeyote anayekuwa critical kwa yeyote anayetaka kuitoa CCM ni adui yetu na rafiki wa CCM.

Hamuwezi kujiuliza kwamba hata katika vita hii ya kupigana na ufisadi kuna mafisadi wanachukua nafasi na kujifanya ni wapinzani, na kama mtakubali kila kitu bila kuuuliza mtajikuta mnamtoa fisadi mmoja na kumuweka fisadi mwingine.

Kuwa critical ni lazima, kama tunakuwa critical kwa CCM, kwa nini tusiwe critical kwa CHADEMA ?
 
Kiama cha Kikwete kimefika, Nani amesema Chadema hakitapata wabunge wengi?

Unaposema "wengi" unamaanisha nini? katika system nyingine za kuhesabu kuna moja, mbili na nyingi, kwa hiyo unaposema "wabunge wengi" unamaanisha wengi zaidi ya wawili au wengi majority (51 + %) ?

Kwa wagombea wenyewe hawa kina Regia Mtema CHADEMA hakiwezi kupata wabunge wengi in the sense of majority, ninachotumaini - not very confidently either- ni kwamba wataongeza idadi ya wabunge na hawatapunguza.

Kama unabisha sema hapa tusubiri uchaguzi turudi kwenye hii thread, tusitake kuandikia mate wakati wino upo.

Habari za kuamini miujiza ya kidini mimi nazipiga vita long time, na CHADEMA usawa huu inahitaji muujiza wa kidini kupata majority.

Mmapenzi yetu kwa upinzani na passion ya kutaka kuona CCM inaondoka isitupofushe tuache kuona ukweli kwamba bado tuna kazi kubwa mbele ya upinzani Tanzania.

Nipe ukweli mchungu anyday badala ya uongo mtamu.
 
Unaposema "wengi" unamaanisha nini? katika system nyingine za kuhesabu kuna moja, mbili na nyingi, kwa hiyo unaposema "wabunge wengi" unamaanisha wengi zaidi ya wawili au wengi majority (51 + %) ?
Duh! mkuu wangu umeogopa kuwa mmoja wa wendawazimu au?
 
Back
Top Bottom