Makanisa yavunje MoU na Serikali...

Serikali imeshindwa kujenga hospitali na shule kukidhi mahitaji ya nchi ndio maana kuna ongezeko kubwa sana la hospitali na shule binafsi. Rejea hotuba ya JK kwa Wauslamu huko Dodoma.
Serikali haijashindwa, tatizo ni kwamba haijaamua.

Kama imeweza kujenga kilomita elfu 18 za lami kwa miaka 8 tu dhidi ya efu 11 tangu tupate uhuru iweje ishindwe kujenga hosptl na shule?

Msiitetee serekali kwavile mnanufaika na MoU. Mbona kwenye kuwaongeza mishahara madaktari na waalim nyie ndo mlikuwa mkiilaumu serekali kuwa haitaki kuwapa madokta na waalim stahiki yao wakati uwezo inayo?

Iweje kwenye hili muitete serikali kama sio kwa vile mnanufaika?
 
Mbona hiyo sasa itakuwa ni biashara nzuri sana kwa kanisa? Maana bila pesa hakuna matibabu. Watajipangia gharama kubwa wanayotaka. Aliye maskini shauri yake!!!
hilo la gharama kubwa mbona lipo siku zote,upo nchi gani?makanisa mmezidi na hamjui kula na kipofu.
 
Makanisa hayawezi kufanya hivyo sababu huo ni utaratibu kati yao na serikali katika kutoa huduma kwa jamii. Kwani wanapotoa huduma wanabagua, si wananchi wote wanahaki sawa ya kupata huduma hizo?

Serikali haina dini, hivyo inachukulia makanisa ni kama taasisi/mashirika yanayotoa huduma pasipo kujijengea faida.

Pia serikali haiwezi ikaruhusu tu organisation flani ikaja kutoa huduma kwa wananchi wake kiholela, hivyo ni lazima kuwe na MoU.
 
Bora tusiyachoma makanisa, kwa sababu kodi itaongezeka na ufisadi utaongezeka ili wakuu wakina Edward na wakiristo wengine wezi wakachangie makanisani

mbona vyuo wanavyosoma hawazungumzii? Tuweke limitation shule, vyuo walipe kwa ada ya kibiashara na vya serikali uwe mfumo ulliopo ili tuone kama watasoma. Pumbafu kabisa hawa wapenda misaada. Bahati mbaya wanaohitaji huduma hizi hawasemi na wasiohitaji ndo wanapiga kelele.
 
Kutokana na kulalamikiwa saana na Waislaam kuwa Makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Makanisa (MOU) yanafanya nchi hii iwe na "Mfumo Kristo" na hivyo kuwanyanyasa Waislaam na hata kuwatawala, inabidi ifike wakati Makanisa yaanze kufikiria jinsi ya kuvunja mkataba huo na kurudi kama ilivyokuwa zamani.

Kwa sababu hili swala limeonakana likichochea sana vurugu, mie napendekeza lifuatalo:

- Wavunje mkataba wa MOU na Serikali.

-Waislaam wawe wanalipia gharama kwa bei ya kawaida ya kutibiwa kwenye Mahospital ya Kanisa.

-Waislaam wawe wanalipia gharama kwa bei ya kawaida ya kutibiwa kwenye Mashule ya Kanisa nk.

-Makanisa na vitengo vyake, viwe vinalipa kodi kwa kufanya biashara ya Hospitals, Shule nk.

-Gharama kwa walio Wakristo, ziwe zinapunguzwa kwa wingi kwa sababu wao hutoa michango mingi tu ya kuendeleza kanisa na sadaka za kila Jumapili.

-Kwa wasio Wakristo na hapo wanapoishi hakuna hospital ya Serikali au ya dini yao, basi itabidi wailazimishe Serikali MPYA ya Tanzania ambayo haitakuwa na Mfumo Kristo tena ili wawajengee Hospitals za Serikali.

Kama Serikali ikishindwa basi wajiandae kulipa gharama kubwa kwenye huduma hizo za jamii au KUBADILI DINI. Kama siyo hilo basi na wao na dini zao wajenge hizo huduma za jamii ili kushindana na za Makanisa.

Nafikiri muda umefika wa kuonyesha kuwa Viongozi wa Makanisa ni Wasomi wa hali ya juu na siku zote "Akili kubwa hutawala akili ndogo......" Vinginevyo, akili zao zitakuwa kazi bure kama hawawezi kutatua matatizo yaliyowazunguka.

Kama kuna kundi jingine au Serikali litakuja na mbinu mbadala na kuweka huduma hizi za jamii katika bei nafuu zaidi, basi ina maana huduma za jamii kutoka kwenye Makanisa tutakuwa hatuhitaji tena. Maendeleo yanakuja kwa mashindano. Muda umefika Makanisa kutangaza mashindano kwa kutoa huduma za JAMII VS dini nyingine au Serikali.
--

Red: Mawazo ya kipumbaavu kabisa,yaani hamtaki MOU afu mnataka huduma chee,jengeni ya kwenu mafirauni wakubwa nyie.

Blue: Haiwahusu,sadaka za wakristo hazikopwi kwa waislam.Shenztype.
 
Kuna haja ya kutafakari yale tunayoyawaza kabla ya kuyaandika hapa jamii forum. Tanzania si nchi pekee ambako vurugu za kipuuzi na ugaidi zinaendelea duniani kote. Kila mtu mwenye akili timamu na asiyemtumwa wa fikra atakubaliana nami kwamba katika karne hii ya 21 usalama wa dunia uko mashakani kwa sababu ya wahuni wanaojidai kumtetea Mungu.

Je ni kweli dunia yote imesaini MOU? We need to think in a broader context on what is happening in Tanzania and the world at large! Anayesema kuwa MOU ni chanzo cha upuuzi huu huyo ni mnafiki kama walivyo wanafiki wengine ulimwenguni kote.

Ukitaka kujua kuwa ukweli wa upuuzi huu fanya tathimini ndogo ya nini madai ya vikundi kama hivi katika nchi zote ulimwenguni na conclusion yako itakuwa kwamba tatizo si MOU wala misamaha ya kodi.

Dini zote zimepewa haki sawa katika misamaha ya kodi na milango iko wazi kusign MOU na serikali provided that MOU hiyo itakuwa na manufaa kwa jamii ya watanzania wote, wenye dini na wasiokuwa na dini.

Badala ya kufikiria mambo ya maendeleo kuhusu waumini wa dini husika, muda mwingi na rasilimali zinapotea kupanga mikakati ya kupambana na aliyeshinda mauti! Kwa maoni yangu: Global strategies are needed to fight against such inhuman behavior spreading all over the world!
 
malaria Sugu, nawaislam ni ruksa kuwa na makubaliano/ mkataba na serikali... Tatizo ni nini?
 
Ninaipenda dini ya kiislam, lakini mambo wafanyayo dunia nzima inanifanya nisiwaelewe.

Tanzania waislam hawajui wanalalamika kwa lipi, leo wanakuja kwa hoja ya MOU, kesho watakuja na mambo ya kuonewa kwenye elimu, keshokutwa kunyang'anywa uwanja n.k. Mambo huibuka kila siku za ijumaa. Yaani mchanganyo tupu.

Misri japo watu milioni 10 hadi 14 kati ya milioni 80 ni wakristo, lakini bado wanalalama wakitaka kuua wakristo.

Nchi nyingine za kiarabu kanisa halirihusiwi, ole wako uwe mkristo. Nipo Misri hapa, katikati ya jiji, leo ijumaa sijui Tahrir square kutaibuka nini.

Sasa sielewi kama shida ni MOU kote huko, au ni kwamba uislam hautatengamaa mpaka dunia nzima wawe waislam.

Nachoshangazwa zaidi, ni waislamu wetu wa bongo ambao hunywa pombe, na bado wanaenda msikitini wakati nchi halisi za kiislam hata kuipata pombe ni shughuli. Jamani sisi ni waTanzania kwanza, hayo madini tuliyoletewa yaje baadaye.
 
napita tu nilichangia nikapigwa
ban mbaya, nilijuta ila 2015 kitaeleweka
tu, ameni
 
mbona vyuo wanavyosoma hawazungumzii? Tuweke limitation shule, vyuo walipe kwa ada ya kibiashara na vya serikali uwe mfumo ulliopo ili tuone kama watasoma. Pumbafu kabisa hawa wapenda misaada. Bahati mbaya wanaohitaji huduma hizi hawasemi na wasiohitaji ndo wanapiga kelele.

jibu hoja acha jazba.
kwani kwenye vyuo kuna mou? Wangeendesha hosptl na shule kama wanavyo enyesha vyuo, kibiashara na sio kutegemea ufadhili wa serekali.
 
Sikonge

Ni hospital gani hapa nchini ukienda kutibiwa unaulizwa dini yako. Ni shule za wakiristo mnasoma kwa Karo sawa na wakristo usipokuwa seminar.

Nyie wakati wenzenu wanawekeza kwenye kujenga mfumo nzuri wa elimu nyie mmewekeza kuoa WAKE WENGI HAMUONI CHANZO CHA UJINGA NA UMASIKINI WENU WA FIKRA BA FUTURE ULIPOANZIA.??
 
Last edited by a moderator:
Hawa jamaa wanafahamika dunia nzima kwa ulalamishi, fujo, roho mbaya,..... Je huko kwingine duniani nako kuna ma-MoU kama hapa? Wanatamani hata Vaticano igeuke kuwa ya kislamu.

Kutekeleza kila wanachodai ni hatari sana. Mano mzuri ni pale walipovamia makao makuu ya Wizara ya Mambo ya ndani...wakatekelezewa madai yao; matokeo yake wakaja na lingine, na lingine, na lingine......hawaishiwi ulalamishi hawa, pengine ndio maundisho ya imani yao.
 
Bwana Sikonge post yako haina mashiko wala chembe ya fikra tatuzi ya migogoro inayoendelea kwa sasa nchini.

Hivi ikatokee leo wewe unaenda hospital unaulizwa dini yako ili utozwa pesa nyingi sindiyo kila siku maandamano yatakuwa yameboresha kwa kasi mpya, angalia post zako, jua zinasomwa na watu weng unapotuma unashilikisha ubongo angalau kidogo na siyo ushabiki kama wa simba na yanga, unapoongelea Udini ni swala serious mno na mnapolichukulia kishabiki nikutoa fulsa yakutawaliwa nakufanyiwa maamuzi kila siku, maana we unaweka ushabiki mwenako yupo serious!
 
Last edited by a moderator:
.Si kweli kwamba Serikali haipangi maendeleo yake kwa kuzingatia dini kwa sababu Serikali haina dini. Ukweli ni kwamba Serikali inapanga maendeleo yake kwa kuzingatia sana dini lakini ni ya kikristo.

Mfano ni ule mkataba wa maelewano baina ya Serikali na Kanisa (MOU), ahadi ya Serikali ni "Kushirikiana na Makanisa kupanga sera na maendeleo ya sekta ya Elimu, Afya na huduma za Jamiii." Je hii si mipango ya maendeleo.

Mkataba huo (MOU) umetoa mamlaka ya kuundwa kwa tume ya kikristo ya huduma ya Jamii (CSSC) kwa lengo la kuunda sera zinazofanana kwa huduma za makanisa na afya na elimu wa makubaliano na Serikali ya Tanzania.
Pia mkataba huo umelenga kuwa na utekelezaji sawa kwa Serikali na makanisa katika maendeleo ya jamii. Je, huu si mpango wa maendeleo baina ya Serikali na Wakristo.

Katika kifungu cha 11 cha mkataba huo kinasema:
"Serikali ni lazima itoe nafasi za ajira katika vyuo vyake vya Ualimu (TTC) kwa Wakufunzi wa kikristo kufundisha watu wataofuzu kama Walimu kwa ajili ya shule za Makanisa zilizoanzishwa."

Je, hii si mipango ya maendeleo kwa kuzingatia dini?


Kutokana na makubaliano hayo baina ya Serikali na kanisa, imelazimika Serikali kuyapa makanisa mabilioni ya fedha za wa-Tanzania kila mwaka katika utekelezaji wa mkataba huu. Mfano mwaka 2008 Serikali iliyapa makanisa jumla shilingi bilioni 170 (Gazeti la Jambo Leo la Jumapili 20/03/2011) liliandika hivi:

"Mwaka 2009 Serikali iliyapa makanisa shilingi bilioni 45. Mwaka 2010 iliyapa shilingi bilioni 61.9."

Kwa maana hiyo Serikali kuanzia 2008 hadi 2011 imeyapa makanisa na taasisi zake shilingi billioni 331. Jee Waislam na taasisi zake wamepewa nini?


Pia iweleweke kwamba zaidi ya asilimia 54 ya bajeti ya Wizara ya Afya inakwenda kwenye vituo vya Afya, zahanati, mahospitali na taasisi nyingine za afya za kikristo. Je fedha hizi zinaweza kutoka bila ya Serikali kuwa na mipango ya maendeleo?
Nimekopi hiki kipande tu ili wote mnaopiga blah blah kuhusu MOU bila kufaham imekusanya nn ndani yake mpate kufunguka - Waislam hawapigi kelele za bure tu.

Kwa bilioni 300 mlizopewa so far, mnaweza kujenga dispensary 600 kila moja ikigharimu milion 500; Mnaweza kujenga shule za kisasa 300 kila moja ikigharimu bilion moja. Mapaka serikali itakapokiri hadharani na kuwafidia waislam, fujo hazitaisha... zitapungua na kuibuka upya. Hiki ni kidonda kinachotuuma waislam.

Mnatoa majibu mepesi kama eti waislam nao hawjakatazwa kuomba, Mou ndo inaleta fujo Naijeria na kwingineko; Hili ni suala gumu na si la majibu ya kianti kama hayo.
 
Tatizo ni kufunika nywele muda wote na kuvaa pekosi hakuna hewa hakuna akili kufanya kazi vyema.

hivi kwani masista hawafuniki vichwa kwa vilemba na mapadri na maaskofu kwa kofia?
Acha kejeli mkuu, unaidhalilisha imani yako mwenyewe.
Kama huna la kuchangia kaa kimya.
 
Serikali haijashindwa, tatizo ni kwamba haijaamua.

Kama imeweza kujenga kilomita elfu 18 za lami kwa miaka 8 tu dhidi ya efu 11 tangu tupate uhuru iweje ishindwe kujenga hosptl na shule?

Msiitetee serekali kwavile mnanufaika na MoU. Mbona kwenye kuwaongeza mishahara madaktari na waalim nyie ndo mlikuwa mkiilaumu serekali kuwa haitaki kuwapa madokta na waalim stahiki yao wakati uwezo inayo?

Iweje kwenye hili muitete serikali kama sio kwa vile mnanufaika?

Kama unakili kwamba tulikuwa tunatete walimu na madaktari hamna WAISLAMU katika hizo kada? Au unaongea kwa kutumia masaburi.
 
jmushi1

Mkuu hizo NSSF, NHC na nyinginezo zenye MoU na serikali ni taasisi za umma na hakuna asiyelijua hilo. Ziko pale kwaajili ya watanzania na hazina uhusiano wowote na dini.

Suala la kujiuliza, siku zote malalamiko ya MoU ya kanisa na serekali yametolewa lakini sio kanisa wala serekali lililotoa ufafanuzi, wanategemea watanzania tuamini nini kama sio kusadiki yanayosemwa na tunao ipinga MoU?

Tukisema kuvunja MoU kutaleta shida kwa watanzania wa kipato cha chini hiyo sio kweli kwasababu watatibiwa kwa kutumia bima ya afya ya NHIF kwa watumishi au CHF kwa watu wengine.

Mbona ukiwa na kadi ya NHIF unaenda hospital yoyote ya private kama Agakhan na unatibiwa?
Unachekesha kweli. Bima ya afya sio hospitali bali ni njia ya kuwezesha wewe kulipiwa gharama za hospitali baada ya kuwa umelipa premium. Sasa kama hakuna hospitali za kutoa huduma, utatibiwaje hata ukiwa na Bima ya afya kutoka makampuni 10?
 
Mkuu RICH OIL SHEIKH, shukran sana kwa ufafanuzi mzuri, hapo ndo utajua hawa jamaa walivyo wanafik.
Wanajifanya wapenda amani kumbe wanadhulumu kodi za watanzania na wananufaika wao wenyewe.
 
Back
Top Bottom