Makanisa yachomwa moto Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makanisa yachomwa moto Zanzibar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kakke, Dec 9, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Dec 9, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [​IMG]

  Na Mwinyi Sadallah
  9th December 2011


  Makanisa mawili yameharibiwa kwa kuchomwa moto na kubomolewa na watu wasiojulikana visiwani Zanzibar.

  Tukio hilo lilisababisha polisi kurusha risasi hewani kutawanya watu waliokuwa wanabomoa kanisa usiku wakiwa na silaha za kienyeji katika eneo la Kianga, Mkoa Kusini Unguja.

  Akizungumza na NIPASHE, Mchungaji wa Kanisa la Siloam, Boniface Kalyabukama, alisema lilibomolewa wiki iliyopita na watu waliotumia nyundo za kupasulia miamba ya mawe.

  Mchungaji Kalyabukama alisema kanisa hilo limeharibika kabisa na kusababisha huduma zote za kiroho kuathirika.

  Mchungaji huyo aliongeza kuwa, kutokana na kuharibika kwa kanisa hilo, waumini wake wapatao 80 sasa wanaendesha ibada katika Shule ya Jumuiya ya Wazazi ya CCM.

  Alisema kundi la watu wenye silaha za kienyeji na tochi zenye mwanga mkali walivamia kanisa hilo majira ya saa 2:00 usiku na kufanya uhalifu huo, baada ya mlinzi, Isaya Eliah, kukimbia kwa usalama wake.

  Mchungaji Kalyabukama alisema kuwa, wakati watu hao wakiwa katika hekaheka za kubomoa kanisa, polisi waliofika katika eneo la tukio ambapo walilazimika kurusha risasi nne hewani baada ya watu hao kukaidi amri ya kuwazuia kulibomoa.

  Alisema kanisa hilo lenye uwezo wa kuchukua waumini 200 kwa wakati moja, lilijengwa kwa gharama ya Sh. milioni 25, baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Magharibi kuwaruhusu waumini hao kujenga kanisa Agosti, mwaka huu.

  "Tangu kukamilika kwa ujenzi wa kanisa na kuanza kutumika kwa ibada, kumeibuka kikundi cha watu kupinga kuwepo kwake katika eneo hilo la Kianga," alisema Mchungaji Kalyabukama.

  Alisema anaamni polisi watatenda haki kwa kuwachukulia hatua watu waliohusika kwa vile wamevunja haki ya kikatiba ya kila mtu kufanya ibada kulingana na imani yake.

  KANISA LINGINE LACHOMWA
  Wakati huo huo, Kanisa la PEFA la Mtufaani, lililoko eneo la Mwera, katika wilaya ya Magharibi Unguja, limechomwa moto na watu wasiojulikana.

  Mchungaji wa Kanisa hilo, Julius Magoho, jana alisema kuwa, lilichomwa moto wiki iliyopita majira ya saa moja usiku, baada ya kumwagwa mafuta ya taa juu ya paa la makuti.

  Alisema alipokea taarifa za kanisa kuchomwa moto kupitia simu ya kiganjani na baada ya kufika alikuta watu wanaendelea kuzima moto huo.

  Mchungaji Magoho alisema aliripoti tukio hilo polisi na baadaye siku iliyofuata wakagundua chupa iliyokuwa na mabaki ya mafuta ya taa karibu na eneo la kanisa.

  Askofu wa kanisa hilo, Daniel Kwilemba, aliomba Polisi kuchukua hatua za kisheria kwa vile tukio hilo linakwenda kinyume cha katiba na misingi ya haki za binadamu.

  Alisema kwamba vitendo vya hujuma dhidi ya makanisa vinazuia uhuru wa kuabudu na kuchochea chuki katika jamii na akaomba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kuvunja kimya na kukemea mwenendo huo.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kusini, Agustine Ulomy, alithibitisha kutokea kwa matukio hayo na kufafanua kuwa mtu mmoja tayari ametiwa nguvuni kuhusiana na tukio la kubomolewa kanisa la Siloam.

  Alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Mbaraka Khamis (60), mkazi wa Kianga na kwamba atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.

  Kamanda Ulomy alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwepo utata katika mradi wa ujenzi wa kanisa la Siloam, baada ya maelezo kuonyesha kwamba halmashauri iliruhusu walioomba eneo hilo kujenga ukumbi wa mikutano na sio kanisa.

  Alisema utata huo unatokana na kijana aliyeuza eneo hilo na baba yake ambaye ndiye anayepinga kuwepo kwa kanisa katika eneo hilo.

  Kuhusu kanisa la PEFA, Kamanda Ulomy, alisema moto ulioharibu kanisa hilo uliwahi kudhibitiwa na hivyo kuzuia madhara.


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Dec 9, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,908
  Trophy Points: 280
  tumthubutu tumeweza na tunazidi kusonga mbele
   
 3. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #3
  Dec 9, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  sijawahi kusikia nchi ya kiislam inaungana nchi yenye imani mchanganyiko,mchakato wa katiba uangalie ugaidi huu.,no wonder why america bought kigamboni to keep an eye on terrorist zanzibar..faiza foxy na malaria sugu wahojiwe na polisi.
   
 4. King2

  King2 JF-Expert Member

  #4
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 1,289
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Bora walivyozama kwenye meli.
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Dec 9, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,908
  Trophy Points: 280
  si kuna waliokuwa wanaomba sehemu ya kujenga msikiti kule ndanda? sasa mbona huku wanachoma nyumba za imani za watu wengine?
   
 6. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #6
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hii ni rekodi ya namna ya aina yake watu kusheherekea miaka 50 ya uhuru wa taifa letu!! Ni vigumu kuamini tena ni maajabu sana!!!!
   
 7. j

  janejean Member

  #7
  Dec 9, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo kunakitu hakijaelezewa vizuri. kwanini hao polisi wasiwakamate waliowakuta wanavunja kwa mahojiano?
   
 8. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #8
  Dec 9, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hakuna demokrasia kwa makafiri!!!
   
 9. M

  Molemo JF-Expert Member

  #9
  Dec 9, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  sumu ya CUF inazidi kusambaa
   
 10. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #10
  Dec 9, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Hao jamaa hawa,mbona huku Bara tunawaheshimu ila wao wakiwa huko kwao wanaleta uhuni wa namna hyo
   
 11. M

  Molemo JF-Expert Member

  #11
  Dec 9, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  tatizo la CUF wakiona kanisa wanadhani lina uhusiano na Chadema.
   
 12. M

  Molemo JF-Expert Member

  #12
  Dec 9, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  hapana mkuu usilipe kwa ubaya.Inatakiwa ifike mahala watu wa cuf waache siasa za kigaidi.
   
 13. Officer2009

  Officer2009 JF-Expert Member

  #13
  Dec 9, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 563
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Tatizo ni kuwa mtume wao *%&*§#?**()/% alikuwa ni gaidi, ndio maana na wao ni magaidi.
   
 14. M

  Molemo JF-Expert Member

  #14
  Dec 9, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  mkuu wangu ungebahatika kusikia hotuba ya hamad Rashid na Habib Mnyaa wa CUF waliyotoa bungeni ungejua chuki ya chama hiki kwa watu wa bara.
   
 15. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #15
  Dec 9, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Waefeso 6:12 imeandikwa hivi: "Kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

  Hampaswi kushangaa hata kidogo sala za kila siku zinawakera sana yale majamaa yanayofugwa au mnajifanya hamjui Zanzibar,Bagamoyo,Tanga na Sumbawanga wamebobea sana kwenye ushirikina !.Suluhu ya mambo yote wanadhani kuchoma makanisa wataishi kwa raha maombi hasa likitajwa lile jina kuu lipitalo majina yote Bwana Yesu Kristo mapepo Yanateseka,Yanatetemeka,Yanakosa raha sasa niambie suluhisho nini kama si kuchoma makanisa yanayowatesa ?.
   
 16. Beautiful Lady

  Beautiful Lady Senior Member

  #16
  Dec 9, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  makafiri ni akina nani hapo?
   
 17. M

  Molemo JF-Expert Member

  #17
  Dec 9, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  ndoa ya cuf na ccm ndio matokeo yake
   
 18. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #18
  Dec 9, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Wale waliotaka kummaliza Yesu (Isa Ibn Mariam) walikuwa nani? Acha upuuzi wako I do not support the action taken in zanzibar and I condemn it but that should not mean you should despise other people's faith ndugu chunga mdomo wako.
   
 19. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #19
  Dec 9, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Ikiandamana unapigwa risasi za vichogoni, ukibomoa kanisa unatawanywa kwa risasi za hewani.

  miaka 50 ya UHUNI wa ccm.
   
 20. M

  Molemo JF-Expert Member

  #20
  Dec 9, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  mkuu wangu hawa CUF walivyo vipofu wakichoma kanisa wanadhani wamechoma ofisi ya chadema
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...