Makanisa ya kiroho mnatupeleka wapi?

Makanisa ya kiroho mnatupeleka wapi?

Sadaka Ni Ibada. Kuna Aina Kadhaa Za Sadaka, Sadaka Ya Hiari, Sadaka Ya Shukrani Na Fungu La Kumi/ Zaka. Halafu Kuna Malimbuko. Sadaka Hizi Hutolewa Kwa Imani. Kama Huna Imani Huwezi Kutoa. Utoaji Ni Moyo, Hata Kama Unacho Kidogo Kama Una Moyo Wa Utoaji Na Imani Unatoa Tu. By The Way Utoaji Si Pekee Kwa Makanisa Ya Kiroho Tu Hata Hayo Makanisa Mengine Nayo Waumini Wake Hutoa, Tena Wana Visanduku Vya Kuweka Bahasha Zenye Fedha Na Vina Namba Kabisa. Ni Rahisi Kumtambua Muumini Ambaye Si Mtoaji Na Rekodi Zake Za Utoaji Zaka Zinawekwa. Akipata Shida Itakoyohusu Msaada Wa Kanisa Rekodi Zake Za Utoaji Zitaangaliwa Kwanza Ndiyo Msaada Utolewe Kwa Kiwango Kinachostahili. Kama Si Mtoaji Unaweza Ukasusiwa Shughuli Zako Ufanye Mwenyewe. Utoaji Ndiyo Ushirika Wenyewe. Utoaji Uko Kila Kanisa Mpaka Jumuiya Zake Za Mitaani. Utoaji Ni Imani Kama Huna Imani Ni Ngumu Kutoa. Unaamini Nini Katika Kutoa ? Labda Hoja Ingekuwa Kutoa Ni Fedha Pekee Tu ? Kwa Nini Iwe Fedha Pekee Tu ? Sifa Kuu Ya Mshirika/muumini Ni Utoaji Sadaka.
Unahitaji kwenda kujisomea tena hizi sadaka zilikuwa zinatolewaje wakati huo kisha utranslate kwa nyakati hizi.
 
Unahitaji kwenda kujisomea tena hizi sadaka zilikuwa zinatolewaje wakati huo kisha utranslate kwa nyakati hizi.
Hoja hapa ni utoaji sadaka uliopitiliza kwenye baadhi ya nyumba za ibada. Zingine si sadaka ni changizo tu au mchango. Makanisa mengine hayana rasirimali za kutosha wala hawana wamisionari toka ng'ambo. Wao wenyewe ndiyo wanachangishana kufanikisha mahitaji yao.
 
Ndugu, Yesu aliwalalamika kwa wanasheria , kuwatwisha watu MIZIGO ambayo wao HATA kiduchu hawaibebi, MNAWATWISHA mama zetu na dada zetu mizigo ya sadaka, ambayo nyinyi hambebi ! HILO ni tatizo , hata kwenye mitandao ya kijamii wahubiri wazungu wanawalalamikia sana waafrika kwa mahubiri ya SADAKA na miujiza ! SISI tutawambia ukweli , HUBIRINI INJILI SIO KILA SIKU MNAWATWISHA DADA ZETU MIZIGO YA SADAKA TU. MAHUBIRI YA KUTAJIRIKA TU KILA SIKU , KUPATA KAZI NZURI UKITOA SADAKA

HAUJUI ULISEMALO,Siyo kila kitu anachosema mzungu ni sahihi!Wao hata ndoa za mashoga wanafungisha,sasa unawasikiliza hao?utakua unashida ukiwasikiliza.

Nikueleweshe kidogo tuu kua,biblia inaelezea kua siku za mwisho moto wa injili utatokea Afrika.Hivyo waambie hao wazungu wasiojua kitu watulie kimya,wao wameshachanganyikiwa waache Waafrica tuwashe moto wa Injili.

Sefania 3:10Maana toka nchi iliyo mbali na mito ya Kushi,waniombao dua,yaani binti za watu wangu waliotawanyika,wataleta matoleo yangu.

INJILI ni habari njema,hivyo kubarikiwa ni injili,miujiza na injili,kupata kazi nzuri ni injili,kutajirika ni injili na zaidi sana kutajirika ni injili na zaidi sana sadaka ni Injili.Sasa wewe kama mtu hautaki watu waambiwe haya mambo yote mazuri basi wewe hautaki Injili,na kama wewe hautaki injili utakua una mapepo.

SADAKA SIYO KWA FAIDA YA MCHUNGAJI AU MTUMISHI WA MUNGU HATA KIDOGO ,SADAKA NI KWA FAIDA YA MTOAJI.

Mtumishi wa Mungu anatunzwa na Mungu hata usipotoa sadaka yako.
 
Sikiliza wewe kipofu wa imani, MUNGU haitaji pesa, wala sadaka, MUNGU anahitaji watu kutenda mema kwa kuzishika Amri zake zote pasipo kuzivunja hata moja. MUNGU anahitaji mioyo iliyopondeka, MUNGU anahitaji UPENDO na REHEMA. Kama unatoa sadaka wakati huna upendo kwa binadamu wenzako, sadaka yako ni bure kabisa! Kama utanatoa mamilioni ya sadaka kanisani, lakini huzishiki Amri Kumi za MUNGU sadaka zako ni bure kabisa!

Soma 1 SAMWELI 15:22 imeandikwa hivi;
"Je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu sawa sawa na kutii sauti ya BWANA?
Angalia kutii ni bora kuliko dhabihu, na kusikia kuliko mafuta ya beberu".

MITHALI 21:3 imeandikwa hivi;
"Kutenda haki na hukumu humpendeza BWANA kuliko kutoa sadaka".

HOSEA 6:6 imeandikwa hivi;
"Maana nataka fadhili wala si sadaka; na kumjua MUNGU kuliko sadaka za kuteketezwa".

ISAYA 1:11 imeandikwa hivi;
"Huu wingi wa sadaka zenu mnazonitolea una faida gani? Asema BWANA".

YEREMIA 7:22 imeandikwa hivi;
"Maana sikusema na baba zenu wala sikuwaamuru kwa habari za sadaka za kuteketezwa na dhabihu siku ile nilipowatoa katika nchi ya Misri; lakini naliwaamuru neno hili nikisema, sikilizeni sauti yangu nami nitakuwa MUNGU wenu nanyi mtakuwa watu wangu mkaende katika njia ile yote nitakayowaamuru mpate kufanikiwa.

MIKA 6:6-8 imeandikwa hivi;
Nimkaribie BWANA na kitu gani na kuinama mbele za MUNGU aliye juu? Je! nimkaribie na sadaka za kuteketezwa na ndama za umri wa mwaka mmoja? Je! BWANA atapendezwa na elfu za kondoo waume au na elfu kumi za mito ya mafuta? Je! nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa kosa langu mzao wa mwili wangu kwa dhambi ya roho yangu? Eeh Mwanadamu Yeye amekuonesha yaliyo mema na BWANA anataka nini kwako; ila kutenda haki na kupenda rehema na kwenda kwa unyenyekevu na MUNGU wako!

WAEBRANIA 10:6 imeandikwa hivi;
Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo, ndipo niliposema tazama nimekuja niyafanye mapenzi yako MUNGU.

Mkuu Conspiracy theorist unapaswa kuwa na akili na busara kujua MUNGU anataka nini kutoka kwako, sadaka ni muhimu lakini siyo kipaumbele cha BWANA MUNGU, dini ya kweli na imani ya kweli siyo kutoa sadaka kanisani, dini iliyo safi isiyo na taka mbele za BABA MUNGU ni hii; kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao na kujilinda na dunia pasipo mawaa. UPENDO kwa Binadamu wenzako ni bora kuliko sadaka yako kanisani.

Mwenye masikio na asikie!

Wewe ni mwehu unayetumia maandiko kuhalalisha wehu wako,na umaskini wako,sitapoteza muda nawewe wala kusoma gazeti lako,nakupuuza tuu.after all hauna mpango wa kutoka kwenye huo umaskini hivyo wewe ni wakupuuzwa tuu.
 
Hayo makanisa yenu endeleeni nayo...... sie tupo huku kama kawa........
 
KWANI TUNATIBIWA BURE? KWANI SHULE ZAO TUNASOMA BURE? KWA TAARIFA YAKO VITEGA UCHUMI VYAO TUNAJENGA SISI THEN TUNALIPISHWA SISI TENA KWA BEI KUBWA ZAIDI BILA KUJALI MICHANGO YETU. TUMIA KICHWA CHAKO VZURI KUFIKIRI
Kwanini msijenge vyenu mkatibiwa bure bila kulipia......
 
Haya msaidie mwenzako

Maji mengi ni kiasi gani....???

Ubatizo ni nini..??
Sasa kumbe hata dhana nzima ya ubatizo huifahamu ? Ujibiwaje Wakati Unaona Ni Upuuzi Tu ?. Ni Ngumu Kumfundisha Mwanafunzi Ambaye Hana Utayari Wa Kujifunza. Wanafunzi Wasiokuwa Na Utayari Wa Kufundishwa Hudharau Somo Linalowasilishwa. Mwalimu Anaishia Kupoteza Muda Kwa Somo Ambalo Halipokeliwi Vizuri Na Wanafunzi, Huko Ni Sawa Na Kumpigia Mbuzi Gitaa Acheze Au Kutwanga Maji Kwenye Kinu Ili Unga Utokee. Mambo Ya Kiroho Hujulikana Kwa Jinsi Ya Rohoni Tu.
 
Nipe maana halisi ya ubatizo
Hivi Kama Huamini Dhana Ya Ubatizo Utawezaje Kuelewa Ubatizo Na Mukhtadha Mzima?. Uko Shambani Na Unakiwa Uvune Mazao, Sasa Kama Huna Vitendea Kazi Utavunaje ? Kuhusu Ubatizo Kama Una Nia safi ya kujifunza bila hila soma sana Biblia Takatifu na maandiko mengine yahusuyo ubatizo. Kuna Dhana Pana Sana Ya Ubatizo. Aaminiye Na Kubatizwa anafahamu mengi kuhusu ubatizo.
 
Hakuna kanisa la mtu binafsi duniani. Kanisa ni kusanyiko la waumini katika jumuiya ya kumsifu na kumuabudu Mungu
haaaaa haaaaa 😡😡, kawadanganye wasiojua, Kakobe alishindaje kesi yake kama hakuna kanisa binafsi duniani !
 
Back
Top Bottom