Makanisa ya kiroho mnatupeleka wapi?

Ndo mana nitabakigi kwenye madhehehu yaliyokuwepo miaka na miaka. Nishaapa kanisa la mtu binafsi sihamii ng’oooo!!!
 

I thought wewe ni atheist..
 
I thought wewe ni atheist..
Atheists ndio wanaoongoza kutoa sadaka kusaidia watu wenzao.

Kwa sababu hawaamini Mungu atasaidia.

Wanaoamini Mungu yupo wanaweza kujibalaguza tu kwa kusema "Tuombe, Mungu atajibu na kusaidia"
 
Atheists ndio wanaoongoza kutoa sadaka kusaidia watu wenzao.

Kwa sababu hawaamini Mungu atasaidia.

Wanaoamini Mungu yupo wanaweza kujibalaguza tu kwa kusema "Tuombe, Mungu atajibu na kusaidia"

Sasa kama hawaamini Mungu how do you call it “sadaka” badala ya labda mchango au msaada wa kawaida???
Sadaka ina relate na imani. ‍♀️
 

Bado kwenye jumuiya zetu zile.......
 
 
Ndugu, Yesu aliwalalamika kwa wanasheria , kuwatwisha watu MIZIGO ambayo wao HATA kiduchu hawaibebi, MNAWATWISHA mama zetu na dada zetu mizigo ya sadaka, ambayo nyinyi hambebi ! HILO ni tatizo , hata kwenye mitandao ya kijamii wahubiri wazungu wanawalalamikia sana waafrika kwa mahubiri ya SADAKA na miujiza ! SISI tutawambia ukweli , HUBIRINI INJILI SIO KILA SIKU MNAWATWISHA DADA ZETU MIZIGO YA SADAKA TU. MAHUBIRI YA KUTAJIRIKA TU KILA SIKU , KUPATA KAZI NZURI UKITOA SADAKA
 
Kutoa kulitakiwa kuwe hiari,sio lazima. Hili La baadhi ya viongozi wa dini kumiliki utajiri kufuru hali waumini wao dhoofu hali lina ukakasi kidogo japo utajiri si dhambi.
 
Sasa kama hawaamini Mungu how do you call it “sadaka” badala ya labda mchango au msaada wa kawaida???
Sadaka ina relate na imani. ‍♀️

Kwanza tuone baadhi ya definitions zinasemaje



Upo sawa, sadaka ina relate na imani, lakini imani sio lazima iwe kwa Mungu.

Juu hapo wanaongelea kwamba sadaka ni righteousness hususan kutoa kwa ukarimu bila kulazimishwa

Mtu anaweza kuwa na imani tu kwamba jua litachomoza kesho asubuhi, hivyo anyooshe nguo za kuvaa kesho kwenda kazini, bila kuamini Mungu yupo.

Mtu anaweza kuwa na imani ya kuwa kusaidia watu wenzake, bila kutegemea malipo ya mbinguni au kuogopa moto wa Jehanam ni jambo zuri, bila kuamini Mungu yupo.

Na kwa kweli, ukifuata definition ya kwamba sadaka ni kutoa bila kulazimishwa, mtu asiyeamini Mungu yupo, halafu akatoa msaada kusaidia watu wenzake, anatoa sadaka ya kweli kuliko mtu anayeamini Mungu yupo. Kuna ma atheists wengi sana ma philanthropists.

Maana, kama sadaka ni kutoa bila kulazimishwa, huyu anayemuamini Mungu kuna uwezekano mkubwa sana anatoa kwa sababu kalazimishwa na dini, anatoa sadaka kwa sababu analazimishwa na maandiko, kwa sababu anaogopa kwenda motoni, kwa sababu ana tamaa ya kwenda mbinguni.

Unanikumbusha mazungumzo fulani nilifanya na dada yangu mmoja mdogo mlokole (sio dada yangu mdogo Rebeca 83 , huyo ni mwingine). Yeye ni mlokole sana. Tulikuwa na msiba, tuna reflect maisha na kama kuna afterlife. Mimi muda wote niko philosophical. Namjua mlokole. Nikamuuliza, wewe ni mlokole, unafanya mengi mazuri, kwa imani ya kwamba Mungu anapenda ufanye mazuri na atakuzawadia mbingu kwa mazuriu nayofanya.

Je, ukihakikishiwa kwamba Mungu hayupo na mbingu haipo, na hakuna moto, halafu ukaambiwa uendelee tu kufanya mazuri hivyo hivyo kama unavyofanya leo kwa kuamini kuna Mungu na mbingu, utaweza?

Lilikuwa swali gumu sana kwa dada yangu, nikaona nisimuulize sana maswali mazito msibani, nikamuacha hajajibu swali.

Kama sadaka ni kutoa bila kulazimishwa, hao wote wanaotoa sadaka kwa kulazimishwa na wachungaji hawatoi sadaka, wanatoa mchango wa kulazimishwa.

Kama sadaka ni kutoa bila kulazimishwa, mtu asiyeamini Mungu ambaye anasaidia watu kwa kutaka tu mwenyewe, anayesaidia bila kuamini kwamba asiposaidia ataenda motoni wala kuamini kwamba akisaidia ataongeza nafasi za kwenda mbinguni, anatoa sadaka zaidi ya mtu anayeamini Mungu na kutoa kwa kuangalia anavyolazimishwa, au kwa kutamani mbingu, au kwa kuogopa moto.

This is where the ungodly atheist can be more godly than the believers.

Kuna dhana ya kwamba ukiwa huamini Mungu wewe ni mtu mbaya, hupendi watu, husaidii, hufanyi mema etc.

Hi ni dhana potofu.

Kuna watu tumeamua kuwa atheists kwa sababu tunaona kuamini Mungu kunatoa mwanya wa kufanya mabaya, ambayo hatuyataki (kwa mfano, kuua kwenye vita za kidini, kubagua watu wa dini tofauti etc).

Kuna watu ambao tumeamua kuwa atheists kwa sababu tunaona ukiwa unasaidia watu kwa sababu unaona kusaidia kutakuongezea nafasi ya kwenda mbinguni na kukupunguzia nafasi ya kwenda motoni,huko si kusaidia watu wengine, nikujisaidia mwenyewe.

Uko sawa kwamba kutoa sadaka ni jambo la imani, lakini, hujagusia zaidi kuona kwamba imani si lazima iwe ya Mungu.

Kuna Buddhists wanatoa sana sadaka, lakini hawamini kuwa kuna Mungu. Wanaamini mtu yeyote anaweza kuwa Buddha.

Kuna article wameandika kuhusu atheist philanthropists
Atheists are the most generous—even without heavenly reward!
 
Kutoa kulitakiwa kuwe hiari,sio lazima. Hili La baadhi ya viongozi wa dini kumiliki utajiri kufuru hali waumini wao dhoofu hali lina ukakasi kidogo japo utajiri si dhambi.
Ndiyo maana wengine tunasema hizi dinini siasa tu, watu wanashikiwa vichwa kwa sababu za kiuchumi na kisiasa.

Sasa mimi masikini nakuja kanisani kujumuika na wenzangu nipate msaada wa kiroho, kwa sababu siwezi kwenda kwa therapist kulipia sessions na wala siwezi kwenda Gymkhana kupoteza mawazo nikicheza golf na hata hela ya bia bara sina.

Halafu kanisani nakuta nikijumlisha michango ya lazima, kuanzia fungu la kumi mpaka hizo sadaka zisizo na kichwa wala mguu, napigwa kuliko ada ya Gymkhana au gharamaza bar.

Ndiyo maana watu wanajaa bar tu.
 
Kazi kwako kama utaendelea kukumbalia hizo roho zidanganyazo au utaamua kutubu,nakushauri utubu na uanze kumtolea Mungu na kusimama na kazi yake.
Sikiliza wewe kipofu wa imani, MUNGU haitaji pesa, wala sadaka, MUNGU anahitaji watu kutenda mema kwa kuzishika Amri zake zote pasipo kuzivunja hata moja. MUNGU anahitaji mioyo iliyopondeka, MUNGU anahitaji UPENDO na REHEMA. Kama unatoa sadaka wakati huna upendo kwa binadamu wenzako, sadaka yako ni bure kabisa! Kama utanatoa mamilioni ya sadaka kanisani, lakini huzishiki Amri Kumi za MUNGU sadaka zako ni bure kabisa!

Soma 1 SAMWELI 15:22 imeandikwa hivi;
"Je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu sawa sawa na kutii sauti ya BWANA?
Angalia kutii ni bora kuliko dhabihu, na kusikia kuliko mafuta ya beberu".

MITHALI 21:3 imeandikwa hivi;
"Kutenda haki na hukumu humpendeza BWANA kuliko kutoa sadaka".

HOSEA 6:6 imeandikwa hivi;
"Maana nataka fadhili wala si sadaka; na kumjua MUNGU kuliko sadaka za kuteketezwa".

ISAYA 1:11 imeandikwa hivi;
"Huu wingi wa sadaka zenu mnazonitolea una faida gani? Asema BWANA".

YEREMIA 7:22 imeandikwa hivi;
"Maana sikusema na baba zenu wala sikuwaamuru kwa habari za sadaka za kuteketezwa na dhabihu siku ile nilipowatoa katika nchi ya Misri; lakini naliwaamuru neno hili nikisema, sikilizeni sauti yangu nami nitakuwa MUNGU wenu nanyi mtakuwa watu wangu mkaende katika njia ile yote nitakayowaamuru mpate kufanikiwa.

MIKA 6:6-8 imeandikwa hivi;
Nimkaribie BWANA na kitu gani na kuinama mbele za MUNGU aliye juu? Je! nimkaribie na sadaka za kuteketezwa na ndama za umri wa mwaka mmoja? Je! BWANA atapendezwa na elfu za kondoo waume au na elfu kumi za mito ya mafuta? Je! nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa kosa langu mzao wa mwili wangu kwa dhambi ya roho yangu? Eeh Mwanadamu Yeye amekuonesha yaliyo mema na BWANA anataka nini kwako; ila kutenda haki na kupenda rehema na kwenda kwa unyenyekevu na MUNGU wako!

WAEBRANIA 10:6 imeandikwa hivi;
Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo, ndipo niliposema tazama nimekuja niyafanye mapenzi yako MUNGU.

Mkuu Conspiracy theorist unapaswa kuwa na akili na busara kujua MUNGU anataka nini kutoka kwako, sadaka ni muhimu lakini siyo kipaumbele cha BWANA MUNGU, dini ya kweli na imani ya kweli siyo kutoa sadaka kanisani, dini iliyo safi isiyo na taka mbele za BABA MUNGU ni hii; kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao na kujilinda na dunia pasipo mawaa. UPENDO kwa Binadamu wenzako ni bora kuliko sadaka yako kanisani.

Mwenye masikio na asikie!
 
 
Inakatisha tamaa kwenda church unajifikiria mara 2,2. Siku hizi uwe na angalau 15000/=kwenye wallet ndo uingie church
 
Toa Sadaka kwa Yatima,Wajane,Masikini,Wasiojiweza,Wenye mahitaji maalumu,Kamwe usitoe sadaka kwa wachungaji wa kileo ambao sadaka yako anaenda kujenga Jumba la bil 1.5,anaenda kununua gari la mil 200 na vitu vinavyofanana na hivyo,mtu ambaye anaifata dini kweli hauwezi kujilimbikizia mali kwa kuwanyonya masikini.
 
Msikitini hata usipotoa hakuna anaekulaumu
yaan waislamu nawakubali hapo tu, mhubiri wa kiislamu anaweza toka zanzibar akaenda kigoma kuhubiri akajigharamia mwenyew kila kitu na akarudi zake zenhi kuendelea na shughuli zake za kujenga taifa ila kwa sisi wakristu hakuna hilo mtu hawez fanya lolote kama hakuna michango yaan kila kitu ni pesa, yaan unakuta waumin maskini wanajuhudi kweli ya kutoa mchango hata kula yao ni mtihani ila mchungaji ana mpango wa kununua private jet yaan ni mambo ya ajabu sana
 
Binafsi si mjuvi sana wa haya mambo ila ukweli ni kwamba Kanisa za leo dhana ya sadaka haiko ktk uhalisia wake tena, wakristo wa leo haswa Waafrika SADAKA tumeinyumbua sana hadi tukatoka kwenye uhalisia wake na hatima yake tunaanza kuimithilisha na wizi kwa kivuli cha sadaka.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…