Makamu wa Rais Samia Suluhu akishiriki katika mazoezi ya viungo

Mnasisitiza mazoezi wakati watu hawana uhakika wa milo mitatu kwa siku, sijui hayo mafuta ya ziada yatatoka wapi.
Nacheka utafikiri mazuri vile... Ninahisi msisitizo umeelekezwa kwa wale maofisa wa ngazi za juu serikalini na sio hawa kajamba nani wenzetu
 
Asante sana mkuu Phillipo Bukililo, kheri na kwako pia. Mie nadhani kwa viongozi wetu ni bora sana kuwa na Afya ya akili kuliko ya Mwili. Haitoshi kuwa na mtu anaweza kukimbia km 20 bila kupumzika, kupiga pushup 50 na kupakua Magunia 100 ya Mahindi toka kwenye Scania na kumpa uongozi kwani yuko kamili kiafya lakini kumbe ni Mirembe case. Kwamba hata sikia ushauri, anaweza kutoa maamuzi ya ajabu na hata kuaibisha.
Afya ya akili inamuwezesha kiongozi hata kama ame paralize na anatembea kwenye wheel chair bado anaweza kufanya maamuzi yenye tija kwa Taifa.
Ni hayo tuu mkuu
Hahahaha afya ya akili huku mwili ukishindwa hata kuwa na uimara wa kutengeneza tangazo la urais la dakika chache tu, ni sawa na bure mkuu.
Huyu tuliyenaye anavyo vyote, afya ya mwili na akili ndio maana wenye kutazama mambo kwa umakini wala hatukujiuliza mara mbili. Alihubiri kitu ambacho anafanana nacho.
Yule ambaye hakuwa na nuru ya mwili, hata kwenye jimbo alilokuwa akiliwakilisha hakuna hayo ambayo alikuwa akiyahubiri jukwaani tena kwa dakika tano tu.
Halafu huyo wa dakika tano tu na ajipange kweli kweli, kwa sababu kila atakapokuwa anashika ili apate cha kuongea anaweza kujikuta akionekana kichekesho.
 
Makamu wa Rais, Samia Suluhu akishiriki katika mazoezi ya viungo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi Oysterbay leo Disemba 31.
bf976ebc8cb6ba66d689aff1c5461a0c.jpg
Zoezi la usafi lilishakufa?
 
Back
Top Bottom