Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu kesho kuanza ziara ya siku sita mkoani Tanga

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,977
Makamu wa Rais mama Samia Suluhu kesho ataanza ziara ya siku sita mkoani Tanga

Mkuu wa mkoa wa Tanga mh Shigekla amesema akiwa mkoani Tanga mama Samia atazindua miradi mbalimbali na programu za uwekezaji kwa wawekezaji wote.

Maendeleo hayana vyama!

===

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuanza ziara yake ya siku sita mkoani Tanga kwanzia kesho, Jumatatu Machi 15 huku miongoni mwa mambo anayotarajiwa kuyafanya ni pamoja na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo sambamba na kuendesha mkutano mkubwa wa wawekezaji na wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya nchi kwa lengo la kutangaza fursa zinazopatikana mkoa humo.

Mkuu wa mkoa wa Tanga mh Shigekla amesema akiwa mkoani Tanga mama Samia atazindua miradi mbalimbali na programu za uwekezaji kwa wawekezaji wote.

 
Mh mbona sielewi, hivi tangu lini viongonzi wa kitaifa kabla ya kutembelea sehem lazima kuwa na press,may be ndo mfumo mpya
 
Wengine watauliza (kwa haki kabisa), kwani mwenye ziara zake yupo wapi? Kachoka? Ama?

Kila la heri Mh. Samia Suluhu katika ziara zako. "Maneno" hayaishi.
 
Back
Top Bottom