Makampuni ya Mawasiliano tunaomba mzindue huduma ya kubadili vocha kuwa muamala wa pesa

Sanja one

Member
Feb 13, 2018
9
19
Hoja yangu hapa ni kutaka kuwepo na mfumo matika simu utakaomuwezesha mtumiaji wa simu aliyeko katika eneo ambalo halina wakala wa huduma za kifefha aweze kununua vocha na kuzibadili kuwa
M pesa,Airtellmoney,Tigopesa n.k na hivyo kumtumia mtu anayehitaji.

Mfano Umeenda kijijini kwa shuguli zako aidha kilimo,biashara,kazi au shughuli nyingine ya kijamii na wakati upo kijijini unapigiwa simu kutoka nyumbani wakiomba pesa ya mahitaji fulani muhimu kama vile umeme umeisha au maji n.k na hapo kijijini kwa bahati mbaya hakuna wakala wa pesa wa mtandao wowote ila maduka yapo na yanauza vocha za mitandao mbalimbali.

Kwa hiyo kwa sababu vocha zipo mteja aweze kununua vocha na kuibadili ndani ya simu yake na kuwatumia nyumbani hiyo pesa wanayohitaji.

Jambo jingine, Kuna wakati mteja anakosea kununua muda wa maongezi badala ya kununua muda wa maongezi wa 500 ananunua wa 5000 au 1000 ananunua 10000 na ukiwapigia watu wa mtandao wanakwambia hawawezi kukusaidia lakini kama kungekuwa na mfumo wa kubadili muda wa maongezi kuwa muamala wa pesa basi ingekuwa ni rahisi na msaada mkubwa sana.

Mwisho; Asanteni sana na karibuni kwa ushauri na maoni na Mungu awabariki
 
Back
Top Bottom