Mabadiliko ya vocha yaendane na uhitaji

analgesic

JF-Expert Member
Jul 27, 2013
677
987
Kutokana na uanzishwaji wa VAT katika muda wa maongezi, imekuwa hauna uwezo tena wa kununua vocha na kuweza kujiunga moja kwa moja vifurushi vya mitandao. Mfano ukinunua vocha ya 500 ukiingiza inakatwa, hivyo haiwi 500 tena wakati vifurushi vya mitandao bado vipo vilevile 500, 1000 nakadharika.

Hivyo, kwanini mitandao ya simu isiendane na wakati kwa kuweka vifurushi vinavyoendana na thamani ya vocha inayobaki kwa mteja baada ya kukatwa VAT? Mfano kifutushi cha miatano sasa kiwe 400, ila wapunguze kama ni dakika, mb, sms Ili kuondoa usumbufu.
 
unatumia mtandao gani ambao ukiweka vocha inakatwa na huwez jiunga?
Nijuavyo ni kwamba inakatwa juu kwa juu ila ww unakua na uwezo wa kujiunga kama kawaida kwa 500 yako au 1000 yako watakutumia txt yenye mchanganuo wa makato ila bado utaweza kujiunga kama kawaida mm nimetoka kuweka vocha muda si mref na nimejiunga vizur tu kwa 1000 langu nililoweka
 
Kutokana na uanzishwaji wa VAT katika muda wa maongezi, imekuwa hauna uwezo tena wa kununua vocha na kuweza kujiunga moja kwa moja vifurushi vya mitandao. Mfano ukinunua vocha ya 500 ukiingiza inakatwa, hivyo haiwi 500 tena wakati vifurushi vya mitandao bado vipo vilevile 500, 1000 nakadharika.

Hivyo, kwanini mitandao ya simu isiendane na wakati kwa kuweka vifurushi vinavyoendana na thamani ya vocha inayobaki kwa mteja baada ya kukatwa VAT? Mfano kifutushi cha miatano sasa kiwe 400, ila wapunguze kama ni dakika, mb, sms Ili kuondoa usumbufu.
Sio kweli ,fatilia mkuu unajiunga na 500 yako bila shida ,kua mpole hili nalo TUTALIANGALIA
 
Back
Top Bottom