Makamishna wa ardhi wasaidizi kuanza kuchukuliwa hatua za kinidhamu

Apr 9, 2022
66
32

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi ametakiwa kuhakikisha anachukua hatua ya kinidhamu mara moja kwa Makamishina wasaidizi wa ardhi Mikoa ambao wanafanya kazi kwa mazoea na wameshindwa kukidhi matarajio ya Wizara.

Maagizo hayo yametolewa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula alipokuwa akifungua kikao kazi cha Makamishna wasaidizi wa Ardhi wa Mikoa amesema wamekuwa wakifanya kazi kwa kuogopana, kulindana na kuathiri utendaji wa kazi.

Pamoja na hatua za kinidhamu ambazo zimekwisha kuchukuliwa Waziri amesem ni pamoja na kuwaachisha kazi kwa baadhi ya Watumishi wa Mikoa ya Mbeya (3) na Dodoma (4), pia ameagiza hatua zaidi zichukuliwe kwa Mikoa mingine.

"Kwa mashauri ya kinidhamu ambayo yanaendelea, naelekeza yakamilishwe haraka, Mikoa ambayo tunakamilisha taratibu za kinidhamu kwa watumishi siku za hivi karibuni ni Mbeya, Arusha, Mwanza, Dar es Salaam na Lindi" amesema Waziri Mabula.

Hata hivyo Dkt. Mabula amesema wamebaini kuwepo kwa Watumishi ambao wamekuwa wakihusisha na vitendo vya udanganyifu katika zoezi la uthamini wa mali ambapo majina yao wameisha yapata na watachukua hatua za haraka.

"Siridhishwi kabisa na utendaji wa Mkurugenzi wa TEHAMA, naelewa katibu Mkuu analifanyia kazi; naelekeza lifanyiwe kazi kwa haraka na kwa muda mfupi" amesema Dkt. Mabula.

Eidha Dkt. Mabula amewaonya makamishna wasaidizi wanaotoa vibali vya ujenzi wa vituo vya mafuta bila udhibiti na utaratibu mbele ya macho yao kama wasimamizi wa sekta katika Mkoa yao, hivyo amewataka likasimamiwe ipasavyo na kwa nguvu zote.
 
Na Tanga kuna ukiritimba mkubwa. Makamishina wasaidizi waliletwa mikoani ku expedite process za kutoa hati nk. Sasa ni kama hakuna makamishina. Nobody cares. CC Mh. Mabula, Waziri wa Ardhi tembelea tanga usikilize kero za watu!
 
Na Tanga kuna ukiritimba mkubwa. Makamishina wasaidizi waliletwa mikoani ku expedite process za kutoa hati nk. Sasa ni kama hakuna makamishina. Nobody cares. CC Mh. Mabula, Waziri wa Ardhi tembelea tanga usikilize kero za watu!
Kuna nini tena huko
 
Back
Top Bottom