Makamba sema kama utaratibu huu wa kumpata Spika hamkuvunja katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamba sema kama utaratibu huu wa kumpata Spika hamkuvunja katiba

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mwanamayu, Nov 24, 2010.

 1. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Kamati Kuu ya CCM

  Wakati wa mchakato wa kumpata mgombea Uspika kwa tiketi ya CCM, iliamua kutoa upendeleo kwa wanawake kwenye kiti hicho na kuwaengua wanaume wote akiwemo Mhe. Sitta na Chenge. Wanawake waliobaki ni Anna Semamba Makinda, Anna Abdallah na Kate Kamba na hatimaye Anna Makinda kupata fursa hivyo.

  Katiba inasema:
  Ibara ya 20
  (2) ...haitakuwa halali kwa chama chochote cha siasa kuandikishwa ambacho kutokana na katiba au sera yake:

  (a) Kukusudia kukuza au kupigania maslahi ya:
  (i) Imani au kundi lolote la dini
  (ii) Kundi lolote la kikabila, mahali watokeapo, rangi au jinsia

  [Swali la Msingi: hivi hawa CCM hawajavunja kweli kifungu cha 20(2)(ii) kwenye kipengele cha jinsia? Je, Spika huyu sio batili kwa mujibu wa ibara hii ya katiba?]
   
 2. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #2
  Nov 24, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Uhuru wa mtu
  kushirikiana na
  wengine Sheria
  ya 1984 Na.14(2) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1) haitakuwa
  halali kwa chombo chochote cha siasa kuandikishwa ambacho
  kutokana na Katiba au sera yake-
  (a) kinakusudia kukuza au kupigania maslahi ya-
  (i) imani au kundi lolote la dini;
  (ii) kundi lolote la kikabila pahala watu
  watokeapo, rangi au jinsia;
  (iii) eneo fulani tu katika sehemu yoyote ya
  Jamhuri ya Muungano;
  (b) kinapigania kuvunjwa kwa Jamhuri ya Muungano:
  (c) kinakubali au kupigania matumizi ya nguvu au
  mapamba

  @ MWANAMAYU HUJAELEWA VIZURI HICHO KIFUNGU,KINAONGELEA UANDIKISHWAJI WA CHAMA CHA SIASA,INA MAANISHA CHAMA CHA SIASA HAKITAANDIKISHWA KAMA KINAPIGANIA HIVYO VIPENGELE ULIVYO VITAJA,SASA CCM TAYARI NI CHAMA CHA SIASA NA KIMESHA ANDIKISHWA KWA MUJIBU WA SHERIA ,KANUNI,NA TARATIBU ZA NCHI,

  HIVYO KWA SWALI LAKO NI KUWA CCM HAIKUVUNJA KATIBA,ILA IMELAZIMISHA UPATIKANAJI WA SPIKA MWANAMKE

  MAPINDUZIIIII DAIMAAAAAAA
   
 3. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  katiba ya tanzania ina viraka vingi sana kiasi kwamba kila kipengele ndani yake, kina kipengele kingine cha kupinga kipengele hicho. Na hivyo huwezi ku-argue kwa kutumia kipengele fulani na kisipatikane kipengele kingine cha kukipinga kipengele unachotumia.

  It is crazy!!! U lazima wa kuandika upya katiba from the scratch uko wazi kabisa.
   
 4. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Thank you mwanamayu for tuition on Constituion.
  My stand: Kwanini wanasheria wa Tanzania wanalala? Ina maana hili hawalioni?
   
 5. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #5
  Nov 24, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Mwelekeo ukibadilika baada ya kuandikishwa, je kifungu hicho hakijavunjwa? Au hakuna kifungu kinachokibana chama cha siasa kutokubadilisha sera zake? Kama ndio, tunajua mambo yanabadilika kuendana na wakati na mahitaji, hivyo sera kubadilika ni lazima lakini pale mabadiliko sio kwa manufaa ya wote ni kuvunja misingi ya katiba yetu, je hapa inakuaje? Sio kurejea kwenye masharti ya kuandikishwa?
   
Loading...