5. Kodi hii inatakiwa ufutwe. Sio kodi ya serikali, ni kodi ya wabunge! kwa hiyo wabunge wote waungane, waache siasa za mitandaoni, warudi bungeni kufanya kazi yao. Inasemekana kua pesa za posho la kitako (seating allowance) za mwaka ni nyingi kuliko simcard tax za mwaka mmoja. Kama kweli wabunge wana uchungu na watanzania basi wafute simcard tax na badala yake watumie pesa za seatting allowance kuongeza kwenye bajeti.
cc:
nngu007 na
EMT
Asante kwa ufafanuzi wako. Bado ninaukokotoa taratibu.
Napenda kuelewa tunapoongelea Serikali ina maana gani?? Kwa jinsi ninavyoelewa hiyo serikali mmoja wa kiongozi wa juu ni PM. Na kwa bahati nzuri Tanzania Serikali yetu inaongozwa na CCM.
Katika suala hili PM ana maelezo yanayotofautiana na viongozi wengine (Mfano J. Makamba, NAPE nk.)
Ina maana hapa ni kwamba hili jambo siyo la Kitaifa bali ni maamuzi ya baadhi ya watu fulani???
Waziri wa Fedha anaopsoma Bajeti Bungeni, huwa anawashukuru mawaziri mbalimbali kwa ushirikiano katika kuiandaa bajeti. Ina maana kuwa siyo Waziri wa Fedha peke yake au Kamati ya Fedha peke yao wanaotengeneza bajeti. Mawaziri husika pia wanashirikishwa. Kwa mtindo huo hapo Waziri J. Makamba alishirikishwa katika Wizara yake.
J. Makamba anasema kuwa hata wizara yake waliipinga kodi hii. (FINE i AGREE..)
NAPE anasema hata CCM wanaipinga kodi hii (FINE I AGREE)
Wabunge waliokuwepo Bungeni siku ya kupitishwa bajeti wote walisema NDIOOOOOOOOOOO (FINE I AGREEE...)
PM anasema wanaopinga kodi hii hawana jema, ina nia nzuri ya kupeleka umeme vijijini.. (FINE I AGREE)
TAFAKARI:
Tanzania tuna vyanzo vingi vya mapato ambapo tunategemea vikitumiwa vizuri basi tutaishi kama tupo peponi.
Kwa takwimu za wasomi wanasema kuwa kuna watanzania ambao wanaishi maisha ya Chini ya Dola ya Kimarekani kwa siku (below 1630/=) Sas huyu huyu ambaye amemiliki simu ili imsaidie mawasiliano apate hiyo mlo wa chini ya $, na serikali inataka Tshs. 1,000/= (ATAZIPATA WAPI)
Serikali inatoa misamaha ya kodi kwa wawekezaji wakubwa katiak migodi ya madini, ambao wanaiba rasilimali zetu na kujinufaisha wao...... hapo bado Serikali hailioni hilo na kumbebesha mzigo mllalahoi wa chini ya Dola $.
Wafanyabiashara wanakwepa kulipa kodi.......hapo bado Serikali hailioni hilo na kumbebesha mzigo mlalahoi wa chini ya Dola $.
MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!