Makamba: Mnyika acha Unafiki, sote tumeshindwa Bungeni!

Makamba: Mnyika acha Unafiki, sote tumeshindwa Bungeni!

Wakuu,

Mnyika kwa upande mmoja wa sarafu yuko sahihi hususani katika kushinikiza kodi ya 'Simcard Tax' ifutwe na serikali ili kupunguza mzigo kwa wananchi hasa wenye kipato cha chini.

Lakini ukija kwa upande mwingine, Mnyika alifanya maamuzi kwa jazba na gadhabu hali iliyo mpelekea kutoa namba za viongozi kwa wananchi bila ridhaa yao, jambo ambalo si la kiungwana kwa kweli.

Kwa taarifa ni kwamba mtu pekee wa kulaumiwa na inapaswa watanzania wajue ni mhe Andrew Chenge (mb), huyu ndiye amehusika katika kupendekeza kodi hii kupitia kamati ya bajeti (ambayo yeye ni mwenyekiti wake) kwa serikali.

Aidha, kiasi ambacho mhe Chenge alipendekeza kikatwe kama kodi kutoka kwenye laini za simu kilikuwa zaidi ya Tsh 1400 kwa mwezi. Jambo ambalo ni la ajabu kupendekezwa na kiongozi mwenye kujua shida za watanzania.

Niungane na Mnyika, Makamba, Zitto, Nape na wengine wote wenye kulaani na kupinga vikali tozo hii kandamizi kwa walala hoi.

Angalizo; vyanzo vya mapato vipo rukuki, ni serikali kuamua tu, na nina imani nayo katika hili la kuibua vyanzo vya mapato, ila SIO kupitia 'Simcard Tax'.
 
Kauli ya MNYIKA:

John-Mnyika-on-kodi-za-simu-July-19-2013.png



Kauli ya MAKAMBA:

January-Makamba-on-Mnyika-acha-unafiki-July-19-20131.png




MAJIBU YA MNYIKA KWA MATUSI YA MAKAMBA.

Kufuatia kauli za Serikali magazetini kuhusu mimi na kodi ya umiliki wa kadi za simu; nijibu tu kwa ujumla kwamba SITAACHA. Badala yake naomba kuwapatia namba zao: Makamba 0767783996 na Mgimwa 0754/0684765644, tunachohitaji ni kauli ya Serikali kuwa kodi imesitishwa na itaondolewa na sio siasa chafu.

Kwa mliotaka msimamo wangu juu ya kauli ilinukuliwa jana tarehe 18 Julai 2013 na Gazeti la Majira kwamba Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba kwamba “Mnyika anaangalia upepo unakoelekea, akiona watu wanalalamika ndipo anaongea namsihi aache kufanya siasa katika jambo hili”, naomba kutumia mtandao huu kutoa majibu ya ujumla kwa maswali na masuala yote kama ifuatavyo:
Nieleze kwamba sitaacha kufanya siasa kwenye jambo hili mpaka kodi hiyo itakapofutwa kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini kubaki na fedha walau kidogo kwa maendeleo.

Sitaacha kufanya siasa kwa sababu ndio kazi yangu ambayo wananchi walinichagua kuifanya ya kuwawakilisha na kuisimamia Serikali ambayo yeye Makamba ni sehemu yake. Sitaacha kufanya siasa kwa sababu Mwalimu Nyerere alisema ili nchi yetu iendelee inahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora.

Ambacho sitafanya ni siasa chafu kama hizo ambazo Makamba amefanya za kusema uongo, kwa kuwa naamini anafahamu kabisa kwamba sijaanza kuongea kuhusu suala hili baada ya malalamiko ya wananchi bali jambo hili nilianza kulishughulikia bungeni mara baada ya Waziri wa Fedha kuwasilisha jedwali la marekebisho la kuanzisha kodi lukuki za simu ikiwemo hii. Katika mchango wangu bungeni, nieleza kwamba muswada huo wa sheria ya fedha kwa kupandisha kodi kwenye mafuta na simu ni ‘muswada wa majanga ya kuwaongezea mzigo wa gharama za maisha kwa wananchi.

Aidha, sikuishia kusema tu kwa niaba ya wananchi bali nilichukua hatua kwa mujibu wa kanuni za Bunge nami kuwasilisha jedwali la marekebisho ya kupinga kodi ya umiliki wa kadi za simu pamoja na kodi nyingine zote zenye kuongeza mzigo wa gharama za maisha kwa wananchi sio kwenye sekta ya mawasiliano bali pia kwenye sekta zingine ikiwemo sekta ndogo (sub sector) nyeti ya mafuta.

Mlioniuliza kwa SMS katika simu na kwenye mitandao ya kijamii sasa ni wakati wa Makamba kuhojiwa kwa njia hizo hizo (Simu yake ya Mkononi ni 0767783996) kwa kuwa yeye ni sehemu ya Serikali na Serikali ndiyo ambayo iliingiza suala hili kwa mara ya kwanza ndani ya ukumbi wa Bunge kupitia hotuba ya Bajeti Serikali na ikalirudia kuliingiza kupitia jedwali la marekebisho ya Sheria ya Serikali; ni wakina nani hasa kwa majina ndani ya Serikali na Bunge walioingiza kodi hii? Na ni wakina nani hasa waliopigia kura ya ndio kuipitisha?

Aidha, amenukuliwa na gazeti la Mwananchi la leo tarehe 19 Julai 2013 akieleza kwamba hakubaliani na suala hili na kupita kwake ilikuwa na kuzidiwa nguvu. Hivyo, ataje kwa majina hayo waliozidi nguvu serikali kinyume na matakwa yake. Amenukuliwa akisema pia kwamba anajua kuwa suala hili haliwezi kutekelezwa na kwamba ni lazima litabadilishwa kwa kuangalia eneo lingine la kutoza kodi. Ni vizuri akahojiwa, ikiwa huo ni msimamo wa Serikali; mwenye mamlaka ya kusitisha kodi hiyo ni nani na kwanini hajitokezi kutoa agizo la kusitisha wakati maandalizi yakiendelea ya kupeleka muswada bungeni wa kuifuta kabisa kodi hiyo katika mkutano ujao?

Wakati Naibu Waziri akisema hayo, Waziri wa Fedha Dk William Mgimwa katika Serikali hiyo hiyo yeye ametoa kauli tofauti siku hii hii ya leo ambapo kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania amewataka watumiaji wa mitandao ya simu nchini na watanzania kwa ujumla kuwa na subira kuhusu tozo ya sh 1000 kwa mwezi kwa kila laini ya simu za kiganjani.

Na kwa kuwa amesema kwamba Serikali inaendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau, natoa mwito kwa wananchi kumtumia maoni kupitia namba zake za simu za mkononi 0754/0684-765644.
Aidha, ni vizuri aeleze subira hiyo ivutwe mpaka lini? Na ni wakina nani hasa kwa majina waliomfanya akaingiza kodi hiyo katika kitabu cha Hotuba yake aliyosoma bungeni kuhusu bajeti ya Serikali na wakina na hasa kwa majina waliomfanya arejeshe kodi hiyo ya kadi za simu kwenye jedwali la marekebisho ya muswada wa sheria ya fedha alilowasilisha bungeni.

Nasisiza kuwa kauli za ujumla za Serikali bila kuwataja kwa majina wahusika ni za kujivua mzigo wa lawama baada ya malalamiko ya wananchi kuhusu kodi hii na nyinginezo kwa kuhamisha mzigo huo kwa wabunge. Ni muhimu badala ya kutoa kauli za ujumla za kulaumu wabunge, Rais ama kiongozi mwingine mwenye mamlaka ajitokeze kusitisha kutozwa kwa kodi hiyo na kuanzisha mchakato wa muswada wa kufuta kodi hiyo kuwasilishwa katika mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza tarehe 27 Agosti 2013.

Majina ya wahusika yasipotajwa au mamlaka zinazohusika zisipotoa kauli katika mkutano wa hadhara nitakaoshiriki jumapili tarehe 21 Julai 2013 katika Uwanja wa Sahara kata ya Mabibo kuanzia saa 8 Mchana mpaka saa 11 Jioni nitatoa mrejesho kuhusu yaliyojiri katika mkutano uliopita wa Bunge na kueleza hatua zaidi zinazopaswa kuchukuliwa kuwezesha majina ya wabunge hao kutajwa hadharani na hatua za kuondoa kodi hiyo kuchukuliwa.

Uongozi bora na uraia mwema wenye uwajibikaji ni chimbuko na chachu ya ukuaji endelevu wa uchumi wa nchi na ustawi wa maisha ya wananchi. Twende kazi.
John Mnyika (Mb)
19 Julai 2013




Kwa humu JF hii ni ile alyosema muhindi "shitakiwa Somali,jaji Somali"

Najuuliza tu kuwa hatujawahi kumsikia Mnyika bungeni akitetea au kupinga hoja? Sasa hili la kusema alifanya chinichini naona kama si tabia yake, sijui lakini Wasomali mnasema nini?
 
Mnyika ni kichwa mbaya, January makamba ni mropokaji kama baba yake yusufu makamba....hutu January ni janga la taifa!
 
January makamba ni janga la taifa, hana kauli nzuri wala busara hata kidogo.nilidhani angalau kwa maccm January ana utu na busara..kumbe ni wale wale.ovyo!
 
na wewe mwananchi ulishindwa kupiga kelele wakati kodi inapitishwa

Na wewe raia unapiga kelele baada ya kuibiwa? mbona hukupiga muda ule mwizi anavunja dirirsha la chumbani kwako?
 
Mnyika ni -------- pamoja na wabunge wote wa CDM ukiondoa Zitto ambaye alishajua alichokosea na kukiri kuwa amefanya makosa kutii amri ya Dj Mbowe kwenda msibani na kuacha swala la simu nijadiriwe yeye akiwa hayupo bungeni na kupitishwa hivyo alishindwa kutetea wananchi wake maana wananchi wake hawakumtuma kwenda kuzika.

Hapa CDM lazima mkiri upumbavu wenu wa kwenda kuzika wakati mngeweza kutuma wawakilishi wengi tu ambao si wabunge na wabunge wakiendelea kuwakilisha wananchi wao sasa nashangaa mnaanza kulisemea swala la bungeni mitandaoni wakati Mnyika na CDM ni sehemu ya bunge huu kama si Upumbavu ni nini?

Wabunge wa CDM mnatakiwa mkue

OK CDM walienda kuzika wenzao ww wabunge wako wa CCM ni mazuzu pale hawajui mema na mabaya kwa wananchi waliowachagua hadi wa CDM wawepo ndo hoja za kijinga na kinyonyaji kama hizo zipingwe. kwa wale wabunge MAGAMBA wapo pale kama wamepooza midomo hawawezi kuongea. KWA HIYO NA WW UNAKILI KUWA WABUNGE WA CDM NI KUHIMU SANA KTK NCHI HII. wakati mwigulu, Wasira, Tendwa wanapanga kuifuta na kuisambaratisha CDM wakati ndo wakombozi wa wanyonge. mmeona wenyewe wametoka kidogo tu bungeni MAGAMBA mmeshabikia upumbavu mmepitisha hoja za kijinga za kunyonya walala hoi
 
Pamoja na kuwa na mashaka juu ya uwezo wa Mnyika lakini sijawahi kumkubali J. Makamba hata kidogo hasa toka apate ubunge kwa kubebwa (bila kupingwa) baada ya wapinzani wake ndani ya chama kutishwa na baba yake aliyekua katibu mkuu ccm wakati huo, kuwahonga wapinzani wasirudishe form. January naomba unieleze ulipigiwa kura na nani kuwa mbunge, hukupingwa sawa lakini kwa nini isipigwe hata kura ya ndiyo na hapana?
 
makamba acha siasa za mtandaoni,humu viroba ni wengi,unajibizana na mtu anajiita "mbwa kachoka" waachie kina Mnyika hapa,kwanza ukiandika against Chadema wanaondoa
Mnyika ni kichwa mbaya,
January makamba ni mropokaji kama baba yake yusufu makamba....hutu
January ni janga la taifa!
 
Mtu yeyote atakayemtetea Makamba katika hili atakuwa amekosea. Kusudi mswada wa sheria uwe sheria, wabunge wanatakiwa kupiga kura mwisho wa siku. Sasa kama Mnyika aliupinga huu mswada kwa kusema hapana, itakuwa sio sawa kwa Makamba kumuweka kwenye kundi la wabunge walioshindwa kutetea wananchi. Swali la kumuuliza Makamba, wakati huu mswada ukipitishwa yeye alipiga kura gani? Tuache kumumunya maneno hapa...
 
Cheap politics...

yaani Jmakamba na Jmnyika na Zkabwe nyote mnachosha, yaani hapa ndio pa kutokea, I don't mind paying that 1,000 tax fee mradi tuwekeane mkataba kuwa vitu vimekuwa improved sio safari za kijinga tu zinafanyika, kuna sehemu Europe actually Amsterdam free boats, wana tax kubwa but zinapeleka maendeleo, so ingekuwa vizuri kuhakikisha hayo makato yanapunguza msongamano wa magari
 
yaani Jmakamba na Jmnyika na Zkabwe nyote mnachosha, yaani hapa ndio pa kutokea, I don't mind paying that 1,000 tax fee mradi tuwekeane mkataba kuwa vitu vimekuwa improved sio safari za kijinga tu zinafanyika, kuna sehemu Europe actually Amsterdam free boats, wana tax kubwa but zinapeleka maendeleo, so ingekuwa vizuri kuhakikisha hayo makato yanapunguza msongamano wa magari

Maendeleo hayaletwi na kuongezwa kwa kodi zisizo na kichwa wala miguu. Moja ya njia ya kuongeza serikali mapato ni kupunguza matumizi yasiyo ya lazima. Katika nakubaliana na Mnyika! Kama alipiga kura ya kupinga hilo ongezo la kulipinga Bungeni then he has done his part. On the other hand, January is a deputy minister that means he knew about this issue before it was even tabled on the floor. Did he say anything to oppose this bill, in the parliament, before it became a law? Mnyika should be commended for being true to his conviction.
 
Zitto siku hizi umaarufu wake kisiasa umepungua sana cdm limebaki jina tu,na mwaka bila ile orodha ya wanaomilki mabilion uswizi tungemsahau!!samahani lakini kama nitakuwa nmemkwaza mtu ,ni mtizamo tu,ni mawazo tu wala msijenge chuki

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
hivi ni sahihi kuweka MOBILE PHONE NUMBER mtu kwenye public,facebook???J.MAKAMBA analalamika mpaka sasa kapokea sms 600 na nyingi ni matusi!!!!kweli mh MNYIKA kafanya kitu sahihi??

ni sahihi sasa tutampataje?
 
Lengo letu ni kufutwa kwa kodi hii kandamizi zaidi baada ya ile kodi ya kichwa.
Kwamba Zitto ameingilia au Lusinde au Wassira, has no meaning kwetu. Mwananchi maskini wa Mpanda akatwe kodi ya line sawa na Bakhressa? Au muuza mananasi pale Msoga akatwe kodi ya line sawa sawa na Reginald Mengi?
Kodi hii ni kandamizi.
 
yaani Jmakamba na Jmnyika na Zkabwe nyote mnachosha, yaani hapa ndio pa kutokea, I don't mind paying that 1,000 tax fee mradi tuwekeane mkataba kuwa vitu vimekuwa improved sio safari za kijinga tu zinafanyika, kuna sehemu Europe actually Amsterdam free boats, wana tax kubwa but zinapeleka maendeleo, so ingekuwa vizuri kuhakikisha hayo makato yanapunguza msongamano wa magari
simcard tax.... serious?
 
Katika kile kinachoonesha Mnyika kutojua mahala pa kupeleka malalamiko ama sehemu ya kutatulia matatizo ya wananchi anatoa mpya ya kujifanya haendeshi Siasa ya kinafiki huku anatoa Number za simu za Viongozi wenzake mitandaoni huku yake haiweki. Ndugu zangu huyu jamaa anatuchonganisha kwani sijawahi kuona ama kusikia jambo limepitishwa Bungeni kisha unakuja kumbana Waziri/Naibu Waziri wa Wizara husika eti afute. Kama ingekuwa inawezekana mambo mengi Mawaziri wasingekuwa wanawasilisha Miswaada yao Bungeni kwani wange kuwa watatua wenyewe bila kushirikisha Bunge. Mnyika usijitoe akili kwa kutoa Number za Simu za Viongozi wenzako mitandaoni ili watukanwe na kisha watakaokamatwa kwa matumizi mabaya ya simu hutawatetea.

Kama kweli wewe unasemea Walalahoi ni kwanini uje kwa mlango wa nyuma ili kutafuta sifa?. Kama haujui wamiliki wa simu ndo wanao-control makato/service charger ya mtumiaji hivyo wanaouwezo wa kujiongea makato yao kwa kila siku kukata Tsh. 34/= na sidhani kama yupo atakaegundua haya makato.

Sitetei makato hayo ila kilichotokea ni kushilikishwa kwetu ndo kumeibua haya, hivi niulize tunataka tuendelee huku hatutaki kuchangia/kushiriki maendeleo yenyewe, je itawezekana?. Libya, Gaddaf aliweka taratibu za kuwalipia watu wanaotaka kuoana kuwaoza na kisha kuwajengea Nyumba na wazee kulipwa kila mwisho wa mwezi ila mwisho wa siku wananchi walichochewa na kuona hafai. Mnyika unaagender gani kwa upande wa pili ama huwatakii wananchi wako kheri?.

Kama tutakuwa na Viongozi walalamikaji mitandaoni sawa na walalahoi sijui atakae mtetea mwenzake ni nani!. Uhuru wa bei za line Mnyika unajifanya upo kwa wananchi kumbe ni unafiki tu, je umeonyesha njia mbadala ya kupata ushuru kutoka kwa wamiliki wa mitandao ya simu. Msitusahaulishe nyinyi wenyewe ndo mlipeleka malalamiko ya wamiliki wa simu kutokatwa kodi na kushinikiza Serikali kufanya hivyo leo hii unakuja kwa mgongo wa chupa wa kudai eti uko pamoja nasi.

Je hamkujua manayoyataka yatawaghalimu walala hoi ama mliwaonyesha jinsi ya kupata mapato kirahisi bila mlala hoi kuguswa?.

umeandika waraka mreefu halafu hunapoint nakushauri usome tena majibu ya Mnyika. yeye alishatoa hilo bungeni lkn kwa sbb ninyi ccm hamkubali mawazo ya wapinzani hususani cdm basi mnaongeaongea tu ila mradi mmeongea. makamba hawezi kujitoa hapao kwa sbb yeye ndiye ni naibu waziri na ndiye aliyeleta hii kitu bungeni kama angekuwa haitaki basi asingeileta angeshauri iachwe hukohuko. amkeni kifikra ccm!
 
Ni jambo la kushangaza serkal hii kukurupuka na kufanya maamuz bila kutumia busara! kwanza niwaeleze,hakuna asiependa kutoa kiwango hicho,lakin je,iweje wazir wa tamisem atoe sawa na mpiga debe wa manzese?
kod hiyo,haitaishia mikon mwa watu wachache kama kawaida yao?
 
Back
Top Bottom