kwa jinsi mfumo wetu wa bunge ulivyo wabunge wa vyama vya upinzani hawawezi kuzuia serikali isipitishe uamuzi wowote bungeni, kwenye masuala mengi yanaopitishwa na bunge tunaona kabisa wanavyopitisha bungeni, wabunge wa vyama vya upinzani hususani cdm partuculary j mnyika wasilaumiwe kwa hiliahaa wa@@@@@ wameacha kututete huko bungeni wanakuja huku mtandaon ili tujue nini watuchefue huyo mnyika pamo ja na makamba wote wako bungeni nawalikuwa na uwezo wotee kwa pamoja kutetea maslai ya wananch wao kutafuta sifa za kijinga
Aliyekuwa Waziri wa Maendeleo Uingereza, Bi Claire Short, alipinga kwa nguvu zote BA kuiuzia Rada Tanzania. Na ilipotokea kwamba hoja yake ilishindwa, basi, waziri huyo alijizulu.
Kama kweli January Makamba anasema hakubaliani na kodi hii ya sim card na kwamba hoja yake ya kukataa imetupiliwa mbali, basi out of principle Makamba alitakiwa ajizulu. Very simple.
Na kwa hili Makamba anatakiwa achague moja, ama aungane na wanaopinga hiyo kodi- kwa kujiuzulu, au aungane na Mgimwa and eat the money. Hawezi kuendelea kuiongoza wizara ambayo anaamini 'inanyonya' wananchi kupitia SIM card. Ama anakubaliana na kodi au anakataa. He cannot have it both ways.
chadema ni wajinga yaani mtu kaweka namba ya mtu bila ridhaa yake mijitu inachekelea na kukenua meno mpaka mimate inawatoka mdomoni kama mazuzu
Katika kile kinachoonesha Mnyika kutojua mahala pa kupeleka malalamiko ama sehemu ya kutatulia matatizo ya wananchi anatoa mpya ya kujifanya haendeshi Siasa ya kinafiki huku anatoa Number za simu za Viongozi wenzake mitandaoni huku yake haiweki. Ndugu zangu huyu jamaa anatuchonganisha kwani sijawahi kuona ama kusikia jambo limepitishwa Bungeni kisha unakuja kumbana Waziri/Naibu Waziri wa Wizara husika eti afute. Kama ingekuwa inawezekana mambo mengi Mawaziri wasingekuwa wanawasilisha Miswaada yao Bungeni kwani wange kuwa watatua wenyewe bila kushirikisha Bunge. Mnyika usijitoe akili kwa kutoa Number za Simu za Viongozi wenzako mitandaoni ili watukanwe na kisha watakaokamatwa kwa matumizi mabaya ya simu hutawatetea.
Kama kweli wewe unasemea Walalahoi ni kwanini uje kwa mlango wa nyuma ili kutafuta sifa?. Kama haujui wamiliki wa simu ndo wanao-control makato/service charger ya mtumiaji hivyo wanaouwezo wa kujiongea makato yao kwa kila siku kukata Tsh. 34/= na sidhani kama yupo atakaegundua haya makato.
Sitetei makato hayo ila kilichotokea ni kushilikishwa kwetu ndo kumeibua haya, hivi niulize tunataka tuendelee huku hatutaki kuchangia/kushiriki maendeleo yenyewe, je itawezekana?. Libya, Gaddaf aliweka taratibu za kuwalipia watu wanaotaka kuoana kuwaoza na kisha kuwajengea Nyumba na wazee kulipwa kila mwisho wa mwezi ila mwisho wa siku wananchi walichochewa na kuona hafai. Mnyika unaagender gani kwa upande wa pili ama huwatakii wananchi wako kheri?.
Kama tutakuwa na Viongozi walalamikaji mitandaoni sawa na walalahoi sijui atakae mtetea mwenzake ni nani!. Uhuru wa bei za line Mnyika unajifanya upo kwa wananchi kumbe ni unafiki tu, je umeonyesha njia mbadala ya kupata ushuru kutoka kwa wamiliki wa mitandao ya simu. Msitusahaulishe nyinyi wenyewe ndo mlipeleka malalamiko ya wamiliki wa simu kutokatwa kodi na kushinikiza Serikali kufanya hivyo leo hii unakuja kwa mgongo wa chupa wa kudai eti uko pamoja nasi.
Je hamkujua manayoyataka yatawaghalimu walala hoi ama mliwaonyesha jinsi ya kupata mapato kirahisi bila mlala hoi kuguswa?.
Kauli ya MNYIKA:
![]()
Kauli ya MAKAMBA:
![]()
MAJIBU YA MNYIKA KWA MATUSI YA MAKAMBA.
Kufuatia kauli za Serikali magazetini kuhusu mimi na kodi ya umiliki wa kadi za simu; nijibu tu kwa ujumla kwamba SITAACHA. Badala yake naomba kuwapatia namba zao: Makamba 0767783996 na Mgimwa 0754/0684765644, tunachohitaji ni kauli ya Serikali kuwa kodi imesitishwa na itaondolewa na sio siasa chafu.
Kwa mliotaka msimamo wangu juu ya kauli ilinukuliwa jana tarehe 18 Julai 2013 na Gazeti la Majira kwamba Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba kwamba Mnyika anaangalia upepo unakoelekea, akiona watu wanalalamika ndipo anaongea namsihi aache kufanya siasa katika jambo hili, naomba kutumia mtandao huu kutoa majibu ya ujumla kwa maswali na masuala yote kama ifuatavyo:
Nieleze kwamba sitaacha kufanya siasa kwenye jambo hili mpaka kodi hiyo itakapofutwa kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini kubaki na fedha walau kidogo kwa maendeleo.
Sitaacha kufanya siasa kwa sababu ndio kazi yangu ambayo wananchi walinichagua kuifanya ya kuwawakilisha na kuisimamia Serikali ambayo yeye Makamba ni sehemu yake. Sitaacha kufanya siasa kwa sababu Mwalimu Nyerere alisema ili nchi yetu iendelee inahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora.
Ambacho sitafanya ni siasa chafu kama hizo ambazo Makamba amefanya za kusema uongo, kwa kuwa naamini anafahamu kabisa kwamba sijaanza kuongea kuhusu suala hili baada ya malalamiko ya wananchi bali jambo hili nilianza kulishughulikia bungeni mara baada ya Waziri wa Fedha kuwasilisha jedwali la marekebisho la kuanzisha kodi lukuki za simu ikiwemo hii. Katika mchango wangu bungeni, nieleza kwamba muswada huo wa sheria ya fedha kwa kupandisha kodi kwenye mafuta na simu ni muswada wa majanga ya kuwaongezea mzigo wa gharama za maisha kwa wananchi.
Aidha, sikuishia kusema tu kwa niaba ya wananchi bali nilichukua hatua kwa mujibu wa kanuni za Bunge nami kuwasilisha jedwali la marekebisho ya kupinga kodi ya umiliki wa kadi za simu pamoja na kodi nyingine zote zenye kuongeza mzigo wa gharama za maisha kwa wananchi sio kwenye sekta ya mawasiliano bali pia kwenye sekta zingine ikiwemo sekta ndogo (sub sector) nyeti ya mafuta.
Mlioniuliza kwa SMS katika simu na kwenye mitandao ya kijamii sasa ni wakati wa Makamba kuhojiwa kwa njia hizo hizo (Simu yake ya Mkononi ni 0767783996) kwa kuwa yeye ni sehemu ya Serikali na Serikali ndiyo ambayo iliingiza suala hili kwa mara ya kwanza ndani ya ukumbi wa Bunge kupitia hotuba ya Bajeti Serikali na ikalirudia kuliingiza kupitia jedwali la marekebisho ya Sheria ya Serikali; ni wakina nani hasa kwa majina ndani ya Serikali na Bunge walioingiza kodi hii? Na ni wakina nani hasa waliopigia kura ya ndio kuipitisha?
Aidha, amenukuliwa na gazeti la Mwananchi la leo tarehe 19 Julai 2013 akieleza kwamba hakubaliani na suala hili na kupita kwake ilikuwa na kuzidiwa nguvu. Hivyo, ataje kwa majina hayo waliozidi nguvu serikali kinyume na matakwa yake. Amenukuliwa akisema pia kwamba anajua kuwa suala hili haliwezi kutekelezwa na kwamba ni lazima litabadilishwa kwa kuangalia eneo lingine la kutoza kodi. Ni vizuri akahojiwa, ikiwa huo ni msimamo wa Serikali; mwenye mamlaka ya kusitisha kodi hiyo ni nani na kwanini hajitokezi kutoa agizo la kusitisha wakati maandalizi yakiendelea ya kupeleka muswada bungeni wa kuifuta kabisa kodi hiyo katika mkutano ujao?
Wakati Naibu Waziri akisema hayo, Waziri wa Fedha Dk William Mgimwa katika Serikali hiyo hiyo yeye ametoa kauli tofauti siku hii hii ya leo ambapo kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania amewataka watumiaji wa mitandao ya simu nchini na watanzania kwa ujumla kuwa na subira kuhusu tozo ya sh 1000 kwa mwezi kwa kila laini ya simu za kiganjani.
Na kwa kuwa amesema kwamba Serikali inaendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau, natoa mwito kwa wananchi kumtumia maoni kupitia namba zake za simu za mkononi 0754/0684-765644.
Aidha, ni vizuri aeleze subira hiyo ivutwe mpaka lini? Na ni wakina nani hasa kwa majina waliomfanya akaingiza kodi hiyo katika kitabu cha Hotuba yake aliyosoma bungeni kuhusu bajeti ya Serikali na wakina na hasa kwa majina waliomfanya arejeshe kodi hiyo ya kadi za simu kwenye jedwali la marekebisho ya muswada wa sheria ya fedha alilowasilisha bungeni.
Nasisiza kuwa kauli za ujumla za Serikali bila kuwataja kwa majina wahusika ni za kujivua mzigo wa lawama baada ya malalamiko ya wananchi kuhusu kodi hii na nyinginezo kwa kuhamisha mzigo huo kwa wabunge. Ni muhimu badala ya kutoa kauli za ujumla za kulaumu wabunge, Rais ama kiongozi mwingine mwenye mamlaka ajitokeze kusitisha kutozwa kwa kodi hiyo na kuanzisha mchakato wa muswada wa kufuta kodi hiyo kuwasilishwa katika mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza tarehe 27 Agosti 2013.
Majina ya wahusika yasipotajwa au mamlaka zinazohusika zisipotoa kauli katika mkutano wa hadhara nitakaoshiriki jumapili tarehe 21 Julai 2013 katika Uwanja wa Sahara kata ya Mabibo kuanzia saa 8 Mchana mpaka saa 11 Jioni nitatoa mrejesho kuhusu yaliyojiri katika mkutano uliopita wa Bunge na kueleza hatua zaidi zinazopaswa kuchukuliwa kuwezesha majina ya wabunge hao kutajwa hadharani na hatua za kuondoa kodi hiyo kuchukuliwa.
Uongozi bora na uraia mwema wenye uwajibikaji ni chimbuko na chachu ya ukuaji endelevu wa uchumi wa nchi na ustawi wa maisha ya wananchi. Twende kazi.
John Mnyika (Mb)
19 Julai 2013
Hivi Mnafiki ni nani kati ya hawa wawili? Makamba ambaye yuko serekalini na hoja ililetwa bungeni na serekali na ililetwa baada ya kubarikiwa na baraza la mawaziri ambaye yeye ni mjumbe au Mnyika ambaye yeye ni mbunge wa upinzani ambaye mara zote huwa hawakubali hoja za serekali lakini kwa sababu ya uchache wao wanazimwa?
Hivi Januari Makamba mpaka lini utagundua kuwa wananchi wa Tanzania wana uwezo wa kuchambua jema na baya? Makamba huna haja ya kuandika hapa, kawadanganye watu wa Bumbuli ambao hawajui chochote kuhusu jinsi mambo yanavyokwenda, sio watu wa kwenye mtandao. Nawewe Zitto, usijifanye una hekima kuliko wenzako. You were supposed call them and talk to them, usijitafutie cheap popularity.
Viva Mnyika