Makamba: Gesi ya Mtwara kuanza kuchimbwa 2025

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Waziri wa Nishati, January Makamba amesema Serikali imeanza mazungumzo na wawekezaji kutoka kampuni ya Equinor na Shell zinazotarajiwa kutekeleza mradi wa uchimbaji gesi asilia Kusini mwa Tanzania, mradi utakaogharimu shilingi trilioni 70

Waziri Makmba ameyasema hayo jijini Arusha akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema mpaka sasa hatua za awali zinaendelea vizuri hivyo Serikali inatazamia zoezi la uchimbaji wa gesi asilia kuanza ndani ya miaka minne

Ameongeza kuwa zoezi la uchimbaji na uchakataji wa gesi asilia lilitarajiwa kuanza mwaka 2016, hatua iliyokwamishwa na vikwazo ambavyo kwa sasa Serikali imeweka mipango madhubuti ya kuvitatua

Chanzo: TBC
 
Wait a minute 🤔🤔🤔 Mmmhhh okay.

Mkataba unasemaje? Sisi kama nchi tunapata % ngapi? So gharama tu ya uchimbaji ni tril 70? Eti? Gharama hizi kubwa mno wamezipataje kabla hata mradi haujamalizika? Yaani deni la Taifa tokea uhuru hadi sasa ni Tril 78. Sasa gharama za uchimbaji gesi hata pamoja na kujenga LNG plant zote ni tril 70? Hizi gharama kubwa sanaaa, something haiko sawa.

Jamani, nawaza tu, usikute waka zidisha gharama sana tukaanza kupigwa mapemaaaaaa. Nawaza tu, uuwiii, OMG.
 
Hii nchi kuna watu wameumbwa kulalamika na kuwa na mashaka dhidi ya watu fulani walioamua tu kuwa nao na mashaka milele daima. Hakuna kitakachopangwa kisiache miguno ya wasiwasi. Ajabu pia ni kuwa wahusika wakikaa kimya watu haohao haraka huja humu na mathreads, '.....atatembelea lini wananchi?', 'mbona hatuoni jipya?', 'hivi gesi ya asili itanufaisha lini wananchi?' n.k

Makamba piga kazi baba, kafaida kadogo utakachokapata wewe kama wewe ndiyo maana ya kuwa waziri.....kila mmoja angekapata kafaida hako, tena walalamikaji na wenye mashaka wa humu wangefanya jitihada ya kukapata kakubwa zaidi. Maana yake haya malalamiko na mashaka meeeengi ni matokeo ya wivu tu na husda. Ukisema uwasikilize wabongo basi utajikuta umesimama hapo hapo bila kupiga hatua yoyote ile
 
JPM aliiota nadhani, wala hakuiona, maana hata Rais alikuwa haruhusiwi kuiona, kwahiyo alihadithiwa tu, au sio?
Tuachane na JPM, ambaye alikuwa na nguvu ya kusema chochote alichotaka bila kuulizwa chochote na yeyote (mifano ipo kedekede ya mambo aliyoyasema. Dr malecela kuhongwa na mabeberu ili autangaze ugonjwa wa zika, ghorofa kubwa kujengwa kwa mil.500, tril 1.5 hazikuenda kusikojulikana, kwmb aliikuta sukari ikiwa na bei zaidi ya 5000 n.k), mi nakuuliza wewe km wewe ULIIONA hiyo mikataba?
 
Bila shaka taarifa inamaanisha uchimbaji na uchakataji, kwamba kutakuwa na plant ya LNG onshore

Kwa sababu kama ni uchimbaji tu, si unafanyika offshore na gesi inasafirishwa kuja Dar kwa bomba ya TPDC na lile la Pan African (Songosongo) kwa matumizi ya kufua umeme na nyumbani (kwa nyumba chache sanaaaaa)
 
Back
Top Bottom