Makamba atoa zawadi ya Nguruwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamba atoa zawadi ya Nguruwe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MaxShimba, Oct 13, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Kada Makamba alinukuliwa na gazeti la Msema Kweli Toleo Na. 040, hivi: "Makamba atoa zawadi ya nguruwe kwa shule".

  Licha ya Mwandishi wa gazeti hilo kushangaa kwa kitendo hicho cha kada huyu kutoa nguruwe ambayo imeharamishwa na Mungu ni kudhihirisha yale Waislamu waliyokuwa na shaka nayo kuhusu Uislamu wake wakati anafanya mambo kinyume, sio kwa bahati mbaya, ila ni kwa jeuri na kibri ya utawala wa dunia.

  Waislamu siku zote tumelalamika kuhusu kuzagaa kwa nguruwe na mabucha ya nyama ya nguruwe bila mafanikio, leo katudhihirishia kwamba kufuga nguruwe ni sera maalum. Vipi shule ambayo haifugi wewe uamue kutoa nguruwe halafu uhimize Waislamu kupeleka watoto wao waje. Siku wakipangiwa kusafisha zizi nani alaumiwe?

  Waislamu tumepata madhila mengi juu ya huyu Bwana tangu awe mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam. Mtume (s.a.w.) anasema Muislamu wa kweli ni yule ambaye Waislamu wenzake wanasalimika na ulimi wake na vitendo vyake.

  Yeye alikuwa mtu wa kwanza kuwatuhumu Waislamu kuiba bia wakati wa vurugu za Mwembechai, kasema tumekamata silaha Msikitini, kumbe ni vigingi vya jukwaa si hilo tu wakati anafungua Bia mpya aliwahi kusema kuwa Watanzania kunyweni Bia hii kwa wingi ili serikali ipate kodi kwa wingi.

  NASAHA: Ndugu Luteni amedai mtu asitawaliwe na dini bali yeye aitawale dini; watu wanasema ukistajaabu ya Musa utaona ya Firauni, lakini mimi nasema "ukistaajabu ya Firauni utaona ya Musa, kwanza yeye sio kiongozi wa dini yoyote wala si kiongozi wa taasisi ya dini kwa hiyo fatwa yake inamrejea yeye mwenyewe.

  Kama ni umaarufu wengi wameutafuta, lakini dunia wameiacha, uhai ni kama mvua, leo mafuriko kesho ukame, yeye adai tusitumie kigezo cha dini kujenga tofauti zetu.

  Je, mbona hawaambii chama tawala wasitumie chama kujenga tofauti na vyama vingine mbona amekuwa mstari wa mbele kuviponda vyama vya upinzani. Je, yeye haoni anazidisha tofauti? Je, mbona kama ni msuluhishi mzuri mbona haendi kuchangia vyama upinzani.

  Je, umoja unaletwa kwa kulazimishwa matakwa yako katika dini. Mungu anasema: "Na wanapokuwa na walioamini husema tumeamini na wanapokuwa peke yao kwa mashetani wao husema "Hakika sisi tu pamoja nanyi tunawacheza shere tu" (2:14)

  Usifikiri Mungu ameghafirika na yale wanayoyafanya watu madhalimu Hakika Yeye anawangojea siku yatakapotoka macho.

  Haki iko juu wala haikaliwi Mungu ndiye Mjuzi, mtambuzi, mwenye nguvu, mshindi, mfalme wa wafalme. Kwake hakuna kugeuka geuka haramu ni haramu na halali ni halali.
   
 2. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Dini inapochanganywa na siasa,
   
 3. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Kwani Makamba kutoa zawadi ya Nguruwe kwa shule ni kosa???
   
 4. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Ndiyo hapo!..nguruwe ni mradi jamani au kwa sababu yeye nimusilam so hatakiwi kutoa zawadi ya nguruwe...shem umenena la maana sana hapa...Bravo shem
   
 5. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2009
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hii habari yenyewe imekaa kienyeji enyeji tu.
   
 6. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  ndiyo waandishi wa habari wetu hao...ktoka TSJ!....
   
 7. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Kiti moto hakina dini wakuu,

  Si mnaona hata Makamba sasa anagawa mkuu wa meza.
   
 8. October

  October JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2009
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mnalalamika nini kuzagaa maduka ya vyakula? Nyie dhambi ni kula Nguruwe tu? Mbona dhambi nyingine mnazifumbia macho tu au mnawaonea wivu wanaofaidi kitimoto?

  By the way kutafuna kitimoto sio dhambi ndo maana akatoa zawadi ya chakula kwa shule, hii ni zawadi nzuri tu na haina tatizo lolote.

  Najua wengine wenu mtakua mmepata kisingizio cha kutokuwapeleka watoto wenu shule kwa sababu navyoona ndicho mnachotafuta hapa, miaka ijayo muanze kulalamika kama kawaida yenu....Acheni hiyo tabia haitawasaidia.

  Poleni sana wandugu kama mnaona mwenzenu kawasaliti, Nafikiri mkimsomea ile nanihii, labda itasaidia asirudie tena.
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Makamba anafuga Nguruwe Kibao kule kwake alipohamia Tegeta!
   
 10. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  mmh shem utasutwa shauri yako>!>!>>>>LOL!
   
 11. M

  Manitoba JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 240
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu nimemuuliza rafiki yangu ambaye ni jirani yake huko wazo na hasisikii harufu wala sauti za nguruwe ... au anawaficha underground?
   
 12. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Mgosi kweli anapenda "controversy", si angetoa ng'ombe tu?
   
 13. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Duh,

  No comments.
   
 14. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #14
  Oct 13, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Mgosi Makamba ni Mgumu kumuelewa......hata huo "Uislamu" wake ni ule Moderate,waliopata kuzungumza nae kwa ukaribu watakubaliana nami kuwa hata "Biblia" ameisoma sana,na katika Hotuba zake nyingi anajaribu kulinganisha maandiko ya Msahafu na Biblia.Suala hilo la Nguruwe naona kwangu si kitu kikubwa sana..Nafahamu kuwa hata Mke wa Mzee Makamba (Mama Januari) ni Mkristo!
   
 15. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #15
  Oct 13, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Mwawado kweli umenena huyu mzee kuna kipindi alikuwa mtu wa karibu sana kwangu, kipindi hicho wala sikujua huyu mzee Makamba ni dini gani.Maana kwenye islam hayupo kwenye ukristo hayupo. Maana kama bible anaijua kweli kweli, hata mie na ukristo wangu sijamfikia bado. Kila atakapoongea lazima aseme mstari wa kwenye bible.
  Hivyo si ajabu hata kama ametoa kweli zawadi hiyo nguruwe.
   
 16. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #16
  Oct 13, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Pia ifahamike CCM haina Dini sasa kwa hilo hakufanya makosa kutowa Nguruwe ,hata Rais Ali Hasani alisema anaetaka kula Nguruwe Ruhusa kutokea siku hiyo Tanzania ikawa biashara ya nguruwe na walaji wakazidi ,chakushangaza Julias na ukafiri wake hata siku Mmoja hajapatapo kusema watu wale nguruwe au kuhalalisha nguruwe.
   
 17. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #17
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Then yeye ni Pagan.....ila ana believe both sides (muslim and christinanity).....tupo wengi kumbe tuliopo kwenye Dilema za dini kama Makamba....i guess as long as you believe in both it's ok...
   
 18. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #18
  Oct 13, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
   
 19. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #19
  Oct 14, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  sasa hii ndio unatumainishia nini KIBUNANGO ?au ndio unataka kutwambia kuwa unayo mifungo ya HInziri? sasa unawakaribisha walaji wenzio kwa nyama choma na LAPINKUTA ?
   
 20. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #20
  Oct 14, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Ndugu Muse A Muse Umesema kweli lakini kuhusu huyu Kada Makamba sio kiongozi wa Dini ya kiislam huyu ni kiongozi wa Chama au lugha nyingine ni Mwanasiasa hausiani na mambo ya Dini hata kama kada Makamba aliwazawadia Punda wanafunzi wa shule Hatawadhuru Waislam kwani Dini ipo pale pale yey ni kiongozi wa mambo ya siasa sio kiongozi wa Dini tusichanganye Dini na Siasa kama alivyosema Baba wa Taifa Seriakali ya Tanzania haina Dini wala Haifuati Dini yoyote mtu yoyote ana uhuru wa kuabudu Dini aitakayo hakuna wa kulazimishwa kuingia Katika Dini kila mtu Atabeba mzigo wake mwenyewe siku ya hukumu mwache Kada Makamba Mwenyeezi Mungu anamwamngalia iko siku Mungu atamtia kada makamba mkononi ndio itakuwa mwisho wake.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...