Makamba ‘amvaa’ Sozigwa!

Mafuchila

JF-Expert Member
Apr 29, 2006
751
65
  • Ashangazwa na kauli yake dhidi ya CCM
  • Si maneno aliyoyatazamia yatoke kwake

Na Mwandishi Wetu
Septemba 15, 2006

KATIBU Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba, amesema kadri anavyomfahamu Paul Sozigwa haiwezekani maneno yaliyoandikwa katika gazeti la Rai wiki hii awe aliyasema na inawezekana alinukuliwa vibaya.

Sozigwa alinukuliwa na gazeti hilo la kila wiki lililotoka juzi akisema CCM imepoteza uwezo wake wa kutoa maamuzi kutokana na idadi kubwa ya wala rushwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi.

Makamba alisema Sozigwa ni kada wa CCM ambaye amekuwa kiongozi kwa muda mrefu na anaijua CCM kuwa ni imara kiitikadi, kimaadili na kioganaizesheni, na kwamba kutokana na hazina kubwa ya viongozi wake wenye hekima na busara, haijashindwa kufanyia uamuzi jambo lolote.

Alisema ana hakika Sozigwa, kupitia uzoefu wake alipokuwa mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, anayajua maamuzi mazito yaliyokwishashughulikiwa na CCM juu ya mstakabali wa nchi.

"Yeye mwenyewe amekuwa kiongozi kwa muda mrefu na anajua uwezo wa CCM katika kushughulikia mambo mbali mbali. Siamini kuwa maneno hayo kweli aliyasema Mzee Sozigwa. Bila shaka amenukuliwa vibaya," alisema Makamba.

Alisema Sozigwa kabla ya kustaafu utumishi katika CCM hivi karibuni ndiye alikuwa mkuu wa Kitengo cha Usalama na Maadili katika Chama na anafahamu vikao vya Chama vinavyosimamia masuala ya kimadili bila kuyumba.

Alisema Sozigwa anawajua kwa majina baadhi ya viongozi waliochukuliwa hatua kwa kukiuka maadili ya Chama, akieleza kuwa wapo waliopewa onyo, karipio na wengine kuachishwa uanachama.

Makamba alisema CCM katika kuthibitisha kuwa inachukia rushwa wapo wanachama ambao haikuwateua kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM licha ya kushinda kura za maoni, ilipofahamika kuwa ushindi wao uligubikwa na wingu la rushwa.

"Mzee Sozigwa akiwa mkuu wa Kitengo cha Usalama na Maadili hakuna hata siku moja alipeleka hoja juu ya wana-CCM fulani kukiuka maadili ya chama kisha vikao vya Chama vikaipuuza," alisema Makamba.

Katibu Mkuu wa CCM alisema kuwepo watu wachache wanaokiuka maadili ya Chama si kigezo cha kujenga hoja kuwa CCM imepoteza uwezo wa kufanya maamuzi kwani ushahidi unaonyesha kuwa watu wa namna hiyo wamekuwa wakidhibitiwa na vikao vya Chama kila wanapobainika.

Makamba ameonya wana-CCM kujiepusha na kauli juu ya mambo ambayo hawajayafanyia utafiti wa kutosha ili kutowakwaza wanachama wenzao na Watanzania kwa ujumla, ambao kimsingi wanaamini CCM ndiyo kimbilio la wanyonge.
 
Mzee Es tunaomba tathmini kuhusu hali jinsi ilivyo na inavyoelendelea ndani ya chama chetu, manake hii kauli na haya majibishano ya katibu mkuu na mzee Sozigwa nayachukulia kwa uzito eti.
 
Mzee Mafuchila,

Heshima yako mkuu, na wazee wote wa forum, Hiii habari ni kweli kama ulivyosema sio habari ndogo ni nzito sana kuliko ilivyopokelewa na public kwa ujumla, maana behind it kuna moto unawaka, kama nilivyosema siku chache zilizopita kuwa Mzee JK anajitayarisha kwa kitu kizito behind kuwafuta wajumbe wote wa kamati ya maadili ya CCM, ambayo huyu Mzee Sozigwa alikuwa ni mmoja wao,

INSIDE INFO (Kama ninavyoifahamu):
(1). Ni kwamba moja kati ya makubaliano between Mtandao na BM katika kumpitisha mgombea wao, ilikuwa ni pamoja na kumkabidhi mgombea wao huyo mafaili yote ya maadili yaliyotayarishwa na Mzee Mang'ula, kwa ajili ya wagombea urais wa CCM, na kweli akapewa,

(2). Mafaili mawili kati ya yote ndiyo yaliyokuwa "Mabaya" nayo ni ya JK na JM, na baada ya kuyaona kwa macho yangu, kwanza nimemdharau Mang'ula kumbe the man was a fraud na fake, sivyo kama nilivyokuwa ninamchukulia katika kipindi chake chote cha uongozi, na sio accident kuwa sasa the man is jobless. Baada ya kuyasoma hayo maneno ndio nimegundua kuwa Watanzania tutaendelea kufanyiana fitina na majungu mpaka mwisho wa dunia wakati hatuna jawabu la matatizo yetu, kimaisha, isipokuwa inapokuja kwenye majungu na fitina we are very creative,

(3). Ukweli ni kwamba Mang'ula alifikiri kuwa ili apate nafasi ya kugombea urais yeye mwenyewe, dawa ilikuwa ni kuwapikia majungu wenziwe, na kwamba huenda by luck CCM itaamua kuwa wagombea wote hawafai, na kumuomba yeye Mang'ula, awe mgombea wao, kwa kuitumia kamati ya maadili ya akina Sozigwa, kwa bahati Mtandao walishagundua hivyo wakambana BM, amkataze kuchukua fomu ambayo tayari alikuwa ameichukua kinyemela, na akairudisha kimya kimya,

(4). Katika siku za karibuni, Mzee JK aliamua kuwa wakati umefika wa kuitosa kamati nzima ya maadili, na makatibu wa CCM wa mikoa na wilaya lakini Mzee mmoja wa CCM akamuwahi na kumuomba kwamba awaache makatibu kwa sababu ni hao hao ndio watakao gombea upande wa upinzani, lakini maadili ni ok, sasa kati yaa maadili waliotoswa huyu mzee ni mmoja wao, Halafu sio siri kuwa Mzee JK, ana mpango wa kuwashughulikia viongozi wezi huko mbele ya safari na itaanzia hapa kwenye maadili,

Maoni yangu ni kwamba, Mzee Sozigwa I like your maneno, lakini tatizo ni kwamba yametolewa baada ya kuondolewa hivyo kuifanya hii message iwe suspect, kwa nini usiseme toka siku nyingi au CCM ndio kwanza imeingiwa na wala rushwa? Halafu Mzee kama Sozigwa kusema maneno mazito kama hayo public, ina maana ana ushahidi wa kutosha, hivyo baada ya Makamba kumjibu,

alitakiwa kumwaga ushahidi hadharani, badala ya kuwa kama Kitine kuchokoza na kubana kimya, Mzee Sozigwa has nothing to lose kwa nini asiweke mambo hadharani? Anaogopa kuwa mkono kinywani umekatwa? Ninasema mzee JK kwamba hiyo hatua ya kuwaondoa hao maadili ilikuwa ni nzuri sana maana sasa si unaona watu kama Sozigwa wanasema? Ina maana kisu kimegusa mfupa sasa, kwa hiyo Mzee JK, kwenye silegeze kamba lazima viongozi wezi watinge kwenye sheria hakuna huruma, na kama kuna wanaogopa na wameanza kuwatuma kina Sozigwa kujaribu kuuzima moto, ni lazima wajue kuwa kwenye hili wananchi hatuko na wezi, na kwa Mzee Sozigwa kwa mtu aliyefikia nafasi kama yake kitaifa kwenda kulia public bila kutoa ushahidi kamili ambao nina uhakika kuwa anao, basi ina maana huenda hana ukweli!

Lakini, all in all bado ninampa respect kwa kujikaza na kusema public, sasa ngoja tuone hii issue itaishia wapi,

Hayo ni maoni ynagu tu Wazee!
 
Mzee Es said:

Atapoishia is predictable:kulekule walikoishia akina Edward Moringe,Stan Katabalo na Horace Kolimba.Ukitaka ugomvi na watawala washtue kwamba wamejisahau kufunga zipu na utupu unaonekana hadharani.CCM ina demokrasia ya kutosha lakini ni dhmbi isiyosameheka ndani ya Chama hicho kutoa maoni yanayochafua CV za watu hata kama yana ukweli kiasi gani.Nadhani JK alitamka hadharani kutofurahishwa kwake na matumizi ya fedha katika kutafuta dhamana za uongozi.Nobody criticized him,for reasons we all know.Najua Makamba ni mwajibikaji lakini anajua mipaka yake,ikiwa ni pamoja na kufahamu kuwa akijifanya mwamba kutaka kupambana na rushwa ndani ya CCM ataondoka kbla ya siku zake.Anyway,someties ili mkono uende kinywani inabidi ufanye yale walokuwa wanafanya waliokutangulia.Afterall,kisa cha nini kupoteza sauti yako kukemea kitu ambapo matokeo yake ni kupoteza ulaji.Nadhani courage ya Mzee Sozigwa imetokana na ukweli kwamba he's got nothing to lose zaidi ya kuwa branded traitor,outcast na pengine kunyimwa fursa za kuwa mjumbe wa bodi wa taasisi flani ya umma.
 
Ukweli ni kwamba huyu mzee ana faults kama hao wala rushwa anaowasema, maana yeye alikuwa maadili na security ya CCM, kilichomshinda kuwaita wala rushwa wa CCM kwenye kamati ni nini?

Halafu kuna kamnong'ono betweeen viongozi wa juu wa CCM kuwa Sozigwa naye sio CLEAN, na yeye anahusika na rushwa kumbe ndio maana Makamba anshangaa lakini hakusema ukweli kuwa anashangaa mtu kama Sozigwa ambaye naye ni Mlarushwa kuwasema wengine,

The next thing nasikia Mzee ataitwa Chimwanga na kuulizwa kisha kufukuzwa CCM, halafu ataingia Chadema ambako nasikia kuna wazee wanajitayarisha kumlipa atoe hizo siri!

Lakini na yeye Sozigwa, ni mla rushwa pia!, sasa wazee wa CCM wamemsubiri kumwagia ya kwake kwenye kikao,

wallah! patamu hapo!
 
Mzee ES,
Heshima yako yako mkuu. Ni kweli kabisa kuwa habari hii ni nzito mno kuliko Umma wa wazalendo wanavyoichukulia nyumbani. Anyway, walisema "Mwanzo wa moto cheche". Kinachonitia wasiwasi hapa je wataachiana "demokrasia" ichukue mkondo wake kwa kile kinachoitwa uhuru wa 'kujieleza'. Kama ulivyosema Mzee ES "Walah patamu hapo" ngoja tusubiri.
 
Kwa habari hii unadhani Chadema watamkata tena ? Hivi Mzee Es unasema Chadema wamlipe aseme ili iwe nini baadaye ? Maana TZ watu serious wala rushwa hawaguswi na habari za aina hii huishia hewani na kukemewa kama ulivyosema basi .Haya wacha tuangalie na hasa mimi nangoja kuona JK kama kweli atasimama na kuwa face wala rushwa sasa na wengineo.Naona ulisema soon ataanza lakini leo umesema huko mbeleni.Sasa naona kama unanichanya.
 
Mzee Es said:
Ukweli ni kwamba huyu mzee ana faults kama hao wala rushwa anaowasema, maana yeye alikuwa maadili na security ya CCM, kilichomshinda kuwaita wala rushwa wa CCM kwenye kamati ni nini?

Halafu kuna kamnong'ono betweeen viongozi wa juu wa CCM kuwa Sozigwa naye sio CLEAN, na yeye anahusika na rushwa kumbe ndio maana Makamba anshangaa lakini hakusema ukweli kuwa anashangaa mtu kama Sozigwa ambaye naye ni Mlarushwa kuwasema wengine,

The next thing nasikia Mzee ataitwa Chimwanga na kuulizwa kisha kufukuzwa CCM, halafu ataingia Chadema ambako nasikia kuna wazee wanajitayarisha kumlipa atoe hizo siri!

Lakini na yeye Sozigwa, ni mla rushwa pia!, sasa wazee wa CCM wamemsubiri kumwagia ya kwake kwenye kikao,

wallah! patamu hapo!

At least Sozigwa got the guts to spill the beans FIRST,akiwa reprimanded kwenye kikao he could easily say kwamba wanamlipizia kisasi.
 
Just a note kuwa a colleague from Dar ameniambia kuwa Sozigwa ameback down on this na kusema kuwa alieleweka vibaya. Anasema Makamba ndie aliemuelewa!

Sijaiona in the news, you may need to reconfirm.
 
Duu uzee wakati mwingine kazi kweli kweli....sasa watu wakija na audio atakana sauti yake?
 
Ama kweli watu wanaona mbali. Hii si ndio kipindi kile mkulu anatembelea wizara kuwahabarisha cha kufanya? Hiki si ndio kipindi kile waliokuwa wanahusika na wizi ikiwa ni pamoja na wamagari walikuwa wakihaha.

Nakumbuka wakati huo ndio pia ilipekuliwa yadi ya Mahita iliyokuwa na magari karibia 50 vile. Kumbe ilikuwa sawazisha ili wazee wapate nafasi ya kunywa kisusio kwa mrija. Ama kweli, watu wanaona mbali vile!
 
Yani mkuu Nono nimeikumbuka hii nikakumbuka tulikotoka... Ilikuwa iwe ilivyo sasa, na huenda ikawa zaidi...!
 
Kweli mazee. Na kumbuka 2009 ndio ishayoyoma na punde si punde tutakuwa na miaka 4! Duh kweli muda unapaa (time flies)....
 
Yani mkuu Nono nimeikumbuka hii nikakumbuka tulikotoka... Ilikuwa iwe ilivyo sasa, na huenda ikawa zaidi...!

Ndio nasema watu wa kariba ya mzee Sozigwa taifa litaendelea kuwakumbuka kwa miaka mingi ijayo. Wakati Mzee Sozigwa anazungumza haya, ni kipindi ambacho watanzania wengi walishindwa kutoa maoni yao wazi wazi kwani umma ulikuwa bado umefumbwa macho na mtandao.
 
tatizo ktk ccm na serikali na nchi kwa jumla mafisadi wamewashikisha watu wengi fedha chafu ili ukisema , wanakurudi kwa hundi zao za shs 2,000 walizo mpa baadhi yao ilikuwafunga mdomo., wanachotofautiana ni kwamba wengine wamechukui kiasi cha mbogo, wengine wamekomba, sasa waliokomba ndio wanaondesha chama
 
Ndio nasema watu wa kariba ya mzee Sozigwa taifa litaendelea kuwakumbuka kwa miaka mingi ijayo. Wakati Mzee Sozigwa anazungumza haya, ni kipindi ambacho watanzania wengi walishindwa kutoa maoni yao wazi wazi kwani umma ulikuwa bado umefumbwa macho na mtandao.

Weekend hii nilikuwa napitia post mbali mbali zilizopita, nikaona si vibaya kama tutajikumbusha kwa mara nyingine suala hili.
By Mafuchila
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom